Natafuta Ajira
JF-Expert Member
- Mar 25, 2020
- 9,016
- 24,650
Soka ni mchezo unashabikiwa na kuangaliwa na watu wa rika zote wakiwemo watoto hivyo basi popote linapojitokeza jambo ambalo linaweza kushusha heshima ya mchezo huu ni lazima lipigwe vita kali.
Kuna habari kwamba kocha wa makipa wa timu kubwa hapa nchi amekutwa na mzigo wa madawa ya kulevya, hii biashara mnyororo wake ni mrefu inawezekana huyu kocha ana washiriki wa kibiashara na wateja wake hapo hapo klabuni hasa ukizingatia siku za karibuni wachezaji wengi hapo klabuni wamekua wakipatwa na majeruhi, kiafya madawa ya kulevya yanaathiri misuli kitu ambacho kinapelekea mwanamichezo anayoyatumia kuumia mara kwa mara.
Hizi taarifa za klabu husika kumkana kocha wao zisipewe uzito maana hakuna ambaye atakubali ushirika na mualifu pale dili linapobuma, ni vyema mamlaka husika zikawahoji pamoja na kuchukua vipimo vya management na wachezaji wote hii itasaidia kuwajua washirika wa huyu kocha hapo klabuni kama wapo.