Tuulize chochote kuhusu mbao na changamoto zake

Huu mnakasha una majibu ya maswali mengi. Pitia neno kwa neno.
 
Uzuri wake ni upi zaidi ya mkongo?
Fundi mmoja alinieleza kwamba mbao za mninga zinahimili sana jua na mvua unapotengenezea milango na madirisha (hiyo ni kabla ya madirisha na milango hii ya kisasa)
 
Mbao ya mwembe ni nafuu na nzuri kwa kutengenezea samani,lkn zinaliwa sana na wadudu,nifanyeje ili zisiliwe?
 
Nina wasiwasi lkn ukizitreat halafu ukaziranda si ile dawa itapotea?
Kuna namna nyingi za kufanya treatment mojawapo ni kuziloweka mbao kwenye dawa. Ubao unanyonya dawa mpaka ndani, hata ukiziranda dawa inabaki.
 
Natafuta machine ya kuchana mbao
 
Wewe lazima utakuwa multi-millionea, kuezeka nyumba kwa kutumia mbao za mninga? Unajua bei ya mninga?
Kwanza kupatikana ni shughuli, hata hizi furniture wanazotuuzia mpaka million kadhaa kwa kitanda huwa sio Mninga hasa, ni wanatuchota tu
 
Mkuu paa langu linaliwa na mchwa vip naweza pata suluhisho mkuu
Umeruhusuje hadi mchwa wafike kwenye paa?? Ulipaswa ufanye treatment ya msingi wako kuhakikisha hakuna mchwa anapanda kwenye paa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…