Determinantor
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 59,045
- 94,974
Ni takribani mwezi na Kidogo tangu gari ya serikali ipate ajali mbaya sana na kuwamaliza abiria wote. Ilikua STL iliyoaminika kuwa ilikua ya Ofisi ya Waziri Mkuu.
Leo Tena gari ya serikali imeondoka na roho 14 za Watanzania ambao ni nyuma Yao wanategemewa na familia zao na ndugu zao.
Kuna tukio lingine (sikumbuki vyema) la gari la Jeshi kusababisha ajali.
Hii ni mifano michache tu inayoumiza saana maana tunavyoandika muda huu Kuna watoto tayari wameshakua yatima... inaumiza sana!
Chanzo Cha ajali nyingi za magari ya serikali ni mwendokasi na kutokujali alama za barabarani huku Askari waliokabidhiwa ada ya kusimamia Sheria na kanuni wakiishia kuwabana Maderava wa magari binafsi.
Magari ya Polisi, Serikali, Jeshi, Mahakama na wengine wa dizaini Yao ndio wanaongoza kwa kuvunja Sheria na kanuni za matumizi ya Barabara bila kuchukuliwa hatua.
Mfano, Leo ni gari ngapi za Polisi ambazo hazina usajili kamili? Zinatumia namba za Malaysia na nchi nyingine as if ni sahihi, mambo kama haya ndio wahalifu kama Akina Sabaya walitumia namba bandia kuvamia makazi ya Mbowe.
STL, STK, STJ, SU, JW na wengine hakuna anayeona kibao Cha 50km/hr Wala Zebra crossing 🚸. Wakitaka kupita Wala hawaangalii Wala kuchukua tahadhari yoyote matokeo yake ajali ikitokea Polisi wanakubebesha wewe, rejea ajali ya Tanga ambapo RTO Tanga aliandika maelezo ya uongo.
Wakuu, tumezika sana inatosha, tumelia sana inatosha! Polisi waache kuwaogopa, wasimamie haki.
Pia sio lazima misafara ya Viongozi iendeshwe kwa speed Hali Barabara zetu na magari yetu havina ubora huo. Rejea ajali ya DC wa Moro na yule Mkurugenzi Binti wa Morogoro sikumbuki wilaya.
Nyingi ni uzembe, TUANZE KUWARIPOTI POLISI AMBAO HAWAWACHUKULII HATUA MADEREVA WA SERIKALI wanaovunja Sheria ikiwa ni pamoja na abiria wao kutokufunga mikanda wawapo safarini.
Tujifunze kwa International NGOs Tena hapa bongo ambapo kama Boss au Abiria hajafunga belt dereva anaruhusiwa kutokuondosha gari Hadi ufunge.