Tuungane kuupinga uonevu wa AzamTv App katika masuala ya kuonesha mechi za soka.

Louis II

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2018
Posts
3,030
Reaction score
4,647
Nipo kwenye gari safarini kuelekea Mbeya nikaamua kununua zangu GB5 za internet ili niweze kuangalia mechi ya watani zangu Yanga Vs Zesco, ila ghafla bin vuu hawa Azam Wameamua kuiondoa chaneli yao inayoonesha mechi hiyo mubashara Azam Sports 2.

Hakika nimesononeka sana kwani naona sasa Safari inaanza kuwa ndefu na nimeghafirika mno. This isn't fair, they should inform us earlier before kuliko kupoteza malengo ya pesa zetu kwa kununulia all these useless GB's.

NB: Nime-Uninstall App yao, daadeki. Tuungane kuipoteza hii App ya hawa washamba.
 
Nakupa pole umechelewa kuchukua hatua toka siku walipoikorofisha app yao makusudi ili tusione simba na yanga mpk leo sijawahi kuwaamini
 
.mi nlikasirika msimu wa Simba champions league nikaitoa. Stupid app
 
Katika app ya kishamba hiyo ni moja wapo, tena wanatoa channel itakayoonyesha game dakika kadhaa kabla ya game kuanza. Kama issue ni biashara, kwa nini umeweka app yenye channel zinazoonyesha mechi live.....weka machannel ya udaku na bongo movie usiwasumbue watu wanaopenda mpira then kwenye king'amuzi endelea na hizo za sports ili watu wanunue.

USHAMBA NI MZIGO
 
Nipo kwenye gari safarini kuelekea Mbeya nikaamua kununua zangu GB5 za internet ili niweze kuangalia mechi ya watani zangu Yanga Vs Zesco, ila ghafla bin vuu hawa Azam Wameamua kuiondoa chaneli yao inayoonesha mechi hiyo mubashara Azam Sports 2.

Hakika nimesononeka sana kwani naona sasa Safari inaanza kuwa ndefu na nimeghafirika mno. This isn't fair, they should inform us earlier before kuliko kupoteza malengo ya pesa zetu kwa kununulia all these useless GB's.

NB: Nime-Uninstall App yao, daadeki. Tuungane kuipoteza hii App ya hawa washamba.
wangese kweli azam na ki app chao yani wametoa sport 2 ambayo ina mechi wamerudisha zbc2 ambayo walishaitoa. nisha ki unstall ki app chao
 
Azam TV wangetuambia wanataka nini tufanye kunapokuwa na mechi muhimu. Na sio kuchomoa betriii dakika za mwisho kwenye Chanel husika. Jee wanataka tulipie app yao? Waweke utaratibu tuuelewe. Azam TV lioneni hili tafadhali
 
Katika app ya kishamba hiyo ni moja wapo, tena wanatoa channel itakayoonyesha game dakika kadhaa kabla ya game kuanza. Kama issue ni biashara, kwa nini umeweka app yenye channel zinazoonyesha mechi live.....weka machannel ya udaku na bongo movie usiwasumbue watu wanaopenda mpira then kwenye king'amuzi endelea na hizo za sports ili watu wanunue.

USHAMBA NI MZIGO
Yani mnafanyiwa free bila kujali una kisimbuzi chao au la bado mnabwabwaja ukuda?
.
DSTV, SKY SPORTS na SATARTIMES bila kuwa na namba ya kadi ya kisimbuxi chako sahau kuona chochote kwenye app zao!
.
Huoni kama huo ni upunjaji mkubwa sana wengine walipie kifurushi Azam Tv ili kutazama mechi wewe utazame bure kwa kununua MB za Voda? Hivi hiyo ni akili au matope

Soon hamtaipata kabisa kama huna namba za kadi hutaweza kuingia na kama hujalipia kisimbuzi hutaona chochote
 
Back
Top Bottom