Tuungane mkono dhidi ya Kunyamazishwa

Tuungane mkono dhidi ya Kunyamazishwa

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Haki ya maoni ni haki ya kikatiba.

Anayedai katiba kuheshimiwa anastahili kuungwa mkono kikamilifu kwa mukthadha huo.

Polepole kupinga kunyamazishwa ni dai halali kwa mujibu wa katiba.

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.

Pamoja na mapungufu yake kwa kutoa maoni yake, hili la watu wasiojulikana kumwandama ni la kupigiwa kelele hata kama yeye alidhani halimhusu:

Leo ni TV na watu wasiojulikana kesho ya akina Ben, Lijenje na kina Mhina yatamhusu.

Ikumbukwe juzi ilikuwa kina Lijenje kesho nani aijuaye?

Tuupinge udhwalimu bila kujali mtendwa nani.
 
Sumu haijaribiwi kwa kuilamba...nyie unganeni naye tu 😆
images (43).jpeg
 
Yeye si alikuwa bingwa wa kupanga mikakati ya kunyamazisha waliokuwa wanakosoa serikali ya mwendazake, hakujua huko aliko kuna siku aashushwa chini?

Nani ataungana na mnafiki kama pole pole? Angekuwa mwenye haki angepigania haki kuanzia kipindi yupo n maveite, anakula bata, siyo kwenye dhiki tuwe wote, kwenye raha mimi siwajui ninyi!!

Kila mtu ashinde mechi zake mwenyewe!!!
 
Haki ya maoni ni haki ya kikatiba.

Anayedai katiba kuheshimiwa anastahili kuungwa mkono kikamilifu kwa mukthadha huo.

Polepole kupinga kunyamazishwa ni dai halali kwa mujibu wa katiba.

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.

Pamoja na mapungufu yake kwa kutoa maoni yake, hili la watu wasiojulikana kumwandama ni la kupigiwa kelele hata kama yeye alidhani halimhusu:

View attachment 2042530

Leo ni TV na watu wasiojulikana kesho ya akina Ben, Lijenje na kina Mhina yatamhusu.

Ikumbukwe juzi ilikuwa kina Lijenje kesho nani aijuaye?

Tuupinge udhwalimu bila kujali mtendwa nani.
Ngoja anyooshwe kwanza,tutamsaidia baadae.
 
Yes. Polepole atoe maoni yake, kuheshimu haki zako lazima uziheshimu pia unapoona wa upande wa pili anadhulumiwa haki kama yako bila kujali aliwahi kufanya au kusema nini nyuma, kinyume na hapo utakuwa mbinafsi usiejua unachokipigania, hata kama ni wa CCM wakinyimwa kile unachokipigania siku zote lazima uwe upande wa haki sio kuungana na madhalimu kumkandamiza.
 
Itapendeza katika vita kutofautisha kwa dhati kabisa hoja kwa upande mmoja na watoa hoja hizo kwa upande mwingine.

"Mola wetu akatupatie nguvu na hekima ya mapambano."
 
Back
Top Bottom