Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tumia falsafa ya hali ya juu! Namna ya kumpinga mtu aliyeshikilia mpini wa kisu nawe umeshika makali. Hakika asipoachia mpini wewe wa makali utaumia. Ni muungano wa hali ya juu kumfanya aachie mpini.
Haki ya maoni ni haki ya kikatiba.
Anayedai katiba kuheshimiwa anastahili kuungwa mkono kikamilifu kwa mukthadha huo.
Polepole kupinga kunyamazishwa ni dai halali kwa mujibu wa katiba.
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
Pamoja na mapungufu yake kwa kutoa maoni yake, hili la watu wasiojulikana kumwandama ni la kupigiwa kelele hata kama yeye alidhani halimhusu:
View attachment 2042530
Leo ni TV na watu wasiojulikana kesho ya akina Ben, Lijenje na kina Mhina yatamhusu.
Ikumbukwe juzi ilikuwa kina Lijenje kesho nani aijuaye?
Tuupinge udhwalimu bila kujali mtendwa nani.