#kataawahuni
Sumu haijaribiwi kwa kuilamba...nyie unganeni naye tu 😆View attachment 2042535
Mmhh!Heri kunyamaza, kama Magufuli alivyonyamaza enzi za Kikwete hatimaye kunyamaza kwake kukampatia urais.
... huu sio wakati wa kupiga siasa! ... ni wakati wa kuwaretea maendereo wanyonge!
NB: Polepole ni muasisi na muumini wa sera hiyo!
View attachment 2042549
Ngoja anyooshwe kwanza,tutamsaidia baadae.Haki ya maoni ni haki ya kikatiba.
Anayedai katiba kuheshimiwa anastahili kuungwa mkono kikamilifu kwa mukthadha huo.
Polepole kupinga kunyamazishwa ni dai halali kwa mujibu wa katiba.
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
Pamoja na mapungufu yake kwa kutoa maoni yake, hili la watu wasiojulikana kumwandama ni la kupigiwa kelele hata kama yeye alidhani halimhusu:
View attachment 2042530
Leo ni TV na watu wasiojulikana kesho ya akina Ben, Lijenje na kina Mhina yatamhusu.
Ikumbukwe juzi ilikuwa kina Lijenje kesho nani aijuaye?
Tuupinge udhwalimu bila kujali mtendwa nani.
Alisahau kuwa msumeno hukata kuwili... huu sio wakati wa kupiga siasa! ... ni wakati wa kuwaretea maendereo wanyonge!
NB: Polepole ni muasisi na muumini wa sera hiyo!
View attachment 2042549
Yes. Polepole atoe maoni yake, kuheshimu haki zako lazima uziheshimu pia unapoona wa upande wa pili anadhulumiwa haki kama yako bila kujali aliwahi kufanya au kusema nini nyuma, kinyume na hapo utakuwa mbinafsi usiejua unachokipigania, hata kama ni wa CCM wakinyimwa kile unachokipigania siku zote lazima uwe upande wa haki sio kuungana na madhalimu kumkandamiza.