Tuungane mkono dhidi ya Kunyamazishwa

Itapendeza katika vita kutofautisha kwa dhati kabisa hoja kwa upande mmoja na watoa hoja hizo kwa upande mwingine.

"Mola wetu akatupatie nguvu na hekima ya mapambano."
Haki haipiganiwi kwa kuangalia sura ya mtu, ukifanya hivyo utakuwa hupiganii haki ya jamii kwa ujumla, bali utakuwa unajipigania haki yako binafsi kwasababu ukiona inavunjwa kwa mwenzako unakaa kimya simply because aliwahi kukusema/kutenda vibaya, ukiangalia sura ya mtu unaungana na wadhalimu kutenda maovu.
 
Kuku wamerudi nyumbani tu kulalia mayai yao waliyotaga.
 

Hapana kwa kweli, huwezi ingia vitani na mnafiki, maana akugeuka sekunde na kwenda kwa adui, waleeee wamejificha kwenye kichaka pale,

Siwezi mtetea pole pole popote, ajishindie tu vita yake mwenyewe. Hapo alipo anapigania tu tumbo lake baada ya kunyanganywa tonge mdomoni!!

Mbona alipokuwa anakula meza kuuu alikuwa anapangia wenzake mikakati hiyo hiyo miovu ya kuwanyamazisha!! Afadhali hata mwenzake Nape aliweza hata kukataa tonge meza kukuuu na kuusema uovu, hata kama hakuweza kusimama sawasawa angalau tu alijaribu,,

Sasa hv baada ya kuondolewa ndo aone kwamba mikakati ile ile aliyokuwa anapangia wenzake imemgeukia anataka huruma, big NO!

Karma is a bitch!! Na wote waliofanya maovu na kuchekelea yatawafika tu!!
 
Itapendeza katika vita kutofautisha kwa dhati kabisa hoja kwa upande mmoja na watoa hoja hizo kwa upande mwingine.

"Mola wetu akatupatie nguvu na hekima ya mapambano."
Kama alivyosema mjumbe mmoja atakapokiri amejifunza ni wapi alipokosea hadharani na kukiri kusimamia haki bila ubaguzi wowote tutamwonea huruma Kwa dhati ma tutasimama nae kuipigania haki Kwa dhati bila hofu ya kusalitiwa na watu aina yake katikati ya mapambano ya haki.kwani naamini wapenda haki hawajawahi kuwa katili kiwango Cha kishindwa kumwonea huruma anayeonewa.
 
Pole pole amejitengenezea tukio ili apate sympathy kwa wananchi.

Kama hajajitengenezea tukio, basi ni wezi wa kawaida tu ambao huwaibia watu wengine pia. Si kaibiwa Tv?

Wanaonyamazishwa huwa wanadhuriwa physically na siyo huu usanii wa kupeleka vibaka kufanya ransoms kwenye nyumba na kusema eti anataka kunyamazishwa.

Apambane na hali yake na kila mtu ashinde mechi zake mwenyewe.
 
watanzania uwa mna huruma Sana.
Ndo maana Wana siasa wanawapenda.
Usije ukashangaa pole pole akahamia chadema.
Walionyamazishwa ni Ben saa 8,lisu,mdude,lema,sugu n.k
Hao ndo unaweza ukasema walinyamazishwa.
Huo hata bega hawajamgusa.
Unasema ananyamazishwa ?
"ACHA MASIKHARA"
 
Yaani kuwa kwenye ubunge ni kuwa kwny dhiki!

Mbunge ana status na uchumi kuliko kuwa mwenezi wa ccm au chama chochote.

Hata huyo nape alienda kugombea ubunge, na kikanuni akawa amejitema uenezi automatically.
 
yaani kuwa kwenye ubunge ni kuwa kwny dhiki!

mbunge ana status na uchumi kuliko kuwa mwenezi wa ccm au chama chochote.

Hata huyo nape alienda kugombea ubunge, na kikanuni akawa amejitema uenezi automatically.

Kwani pole pole alienda kugombea ubunge wapi? Huo ubunge wake ni kupewa na mwendazake anaweza kunyang'anywa mda wowote tu,
 
Pole pole habaguliwi kwa sababu ya ya chama chake wala sura yake bali alishiriki kudhurumi hiyo haki kwa wengi na hana uhalali wa kutetea hiyo hakini badala yake huyu ni mbwa mwitu anayetaka kujivisha ngozi ya kondoo kwa hakika lazima apigwe vita vikali maana ndio hao wanaotuchelewesha kuipata katiba kwa njaa njaa zao
 
Haya mawazo yenu yanawakilisha kundi la wapinzani walioamua kubakia kwenye upinzani forever, lakini kama mna ndoto ya kuongoza serikali mnatakiwa kubadilika ASAP.

Mbowe alivyokuwa anaitafuta reconcilliation mbele ya Magufuli aliona mbali, lakini wote mliobaki mlimpuuza na ndio mnaendeleza haya mawazo yenu mpaka sasa.

Kuendelea kumshambulia Polepole huku mna ndoto za kushika dola CCM sio wajinga, mnaonesha wazi mlivyo na visasi na siku ikitokea mkaipata hiyo nafasi hakuna mtakaemuacha, mtawatafuta wote muwachape viboko, naamini kwenu wengi waliopo CCM sasa waliwatendea mabaya.

From hiyo mentality mliyomo, sidhani hata kama mnaelewa maana ya kuidai Katiba Mpya, inaonekana huwa mnaimba tu muipate kwa ajili ya kutimiza matakwa yenu, na kwa akili zenu hizi, siamini kama kuna siku CCM watajichanganya wawape, itatafutwa mpaka uzeeni huku mkiendelea kuamini Karma kwa specific individuals isiyo na impact yoyote kwa upinzani kwa ujumla.
 
Ni nani ndani ya CCM ambaye hajawahi kuwanyan'ganya haki zenu? naona mnaimba ngonjera msizozijua.

Hata hao kina Nape na Makamba mnaowapa support sasa hivi bila kujielewa waliwahi kushiriki "bao la mkono" ile nayo ilikuwa ni haki iliyoporwa.

Lakini kwa uwezo wenu mdogo wa kutafakari na tabia ya kufuata mikumbo mmeamua kujitumbukiza kwenye kumshambulia Polepole huku madhalimu wengine wametulia tu wanawatazama mnavyakausha makoo yenu kuwatetea bila kujua.

Mnatakiwa kuficha hizi emotions zenu mjue namna ya kucheza hili game, vinginevyo hakuna namna zaidi ya kubakia wapinzani milele.
 

Kushika dola ni zaidi ya uana harakati.

Mandela aliridhiana na makaburu.

Kwetu hata Zitto na Mbatia kuna watu hawataki kuwasikia.

Mwamba Mbowe anajua tofauti ya hoja na watoa hoja. Yumkini ndiyo sababu wanamhofia zaidi.
 
Kwani tundu lisu alifanya nini?? Si alikuwa anatoa maoni yake???? Si mnamuita msaliti hapa jamvini??? Alimsaliti nani? Adhabu yake ni risasi zote zile????
 
Bora kubaki na hiyo mentality kuliko ukigeugeu na usaliti wa kuunga juhudi baada manunuzi🤔.
 
Heri kunyamaza, kama Magufuli alivyonyamaza enzi za Kikwete hatimaye kunyamaza kwake kukampatia urais.
Hio sio kanuni SAHIHI ya kujenga nchi,
Wengi wamenyamaza na hawajapata cheo chochote
Na huo ni unafiki wa kupenda vyeo badala ya kupambania nchi
 
Kwani nyie ni wapigania haki?
Mlipigania haki ya Nani?
Mbowe yupo ndani, piganieni haki yake!
 
Hivi kweli Polepole ni mjinga kutaka huruma ya wananchi?
Hio huruma ya wananchi itamsaidia Nini?
Lisu imemsaidia Nini huruma ya wananchi?
 
Kwani nyie ni wapigania haki?
Mlipigania haki ya Nani?
Mbowe yupo ndani, piganieni haki yake!
Hata ya unae mtetea sharti akubali alipokiuka haki za wengine na utayari wakuacha ukigeugeu ama Kwa maslahi binafsi au Yale ya kisiasa au wale anaowapigania🤔.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…