Tuungane mkono dhidi ya Kunyamazishwa

Hivi kweli Polepole ni mjinga kutaka huruma ya wananchi?
Hio huruma ya wananchi itamsaidia Nini?
Lisu imemsaidia Nini huruma ya wananchi?
Ongeza sauti hujasikika na haujaeleweka.
 
Kwanza ni vema sasa kuwa unakubaliana nasi kuwa pole pole ameshiriki sehemu kubwa kudhuru na kupora haki nyingi kwa namna mbalimbali.

Lakini pia unataka kutulazimisha kuwa tunawasapoti akina Nape na makamba we lengo lako ni kutaka kumpunguzia mizigo wa lawama unaomwandama pole pole.

Tunatambua wao wanayo yakwao na sikwamba hatuyajui ila kwa sasa acha pole pole avune alichopanda hii Ndiyo karma na ukome kujiona mjuaji na kujiona we una upepo kuliko wengine huku ukiwabambikia vyama vya siasa, zaidi jadili hoja bila mihemiko.
 
Mlikuwa wapi Magufuli alipowanyamazisha Watanzania? Leo imekula kwenu ndo mnataka "tuungane"? Unganeni wenyewe 😡
 
Mlikuwa wapi Magufuli alipowanyamazisha Watanzania? Leo imekula kwenu ndo mnataka "tuungane"? Unganeni wenyewe 😡

Ipo tofauti kubwa baina ya hoja na mtoa hoja lakini. Au nasema uongo?

Au ndiyo ile ya mchawi kulia zaidi msibani?
 
Polepole ni mtumishi wa tumbo. Asingeondolewa kutoka katika kile cheo cha uenezi asingefanya yote anayoyafanya kwa sasa.

Ni opportunist tu kama wengine unaowafahamu.
 
Polepole ni mtumishi wa tumbo. Asingeondolewa kutoka katika kile cheo cha uenezi asingefanya yote anayoyafanya kwa sasa.

Ni opportunist tu kama wengine unaowafahamu.

Mkuu hoja yake ni kuwa mnamnyamazisha asiseme. Hadi mmekwenda kumwibia TV.

"Wengine kina sisi ni kwenye uhalali wa kumnyamazisha mtu tu!"

Ya vyeo na matumbo yenu yatuhusu sisi wapi?
 
Mkuu hoja yake ni kuwa mnamnyamazisha asiseme. Hadi mmekwenda kumwibia TV.

"Wengine kina sisi ni kwenye uhalali wa kumnyamazisha mtu tu!"

Ya vyeo na matumbo yenu yatuhusu sisi wapi?
Huyo ni mnafiki tu anaangalia upepo wa kisiasa umekaaje, anaona mbili haisomi tatu haisomi. Anatafuta kuungwa mkono na 'silent majority' bado hana uzoefu wa kupambana na walio nyuma ya Rais wa sasa hajaiva kisiasa kuliko anavyojidanganya.
 
Ninapata ugumu kumjadili mtu.

Hatuwezi kujikita kwenye hoja?
 
Ninapata ugumu kumjadili mtu.

View attachment 2043085

Hatuwezi kujikita kwenye hoja?
Kupitia kwa mtu ndio unapoweza kuzijadili ideas kwa mapana yake. Labda wakati wa Reagan alipokuwa rais wa USA ulikuwa bado ni mdogo sana miaka ile ya 1980-88. Kulikuwa na Reaganomics, yaani sera za uongozi wa Reagan.

Ukizungumzia Magufulism unaongelea sera nzima za uongozi wa Magufuli kwa maana ya anasimamia nini katika masuala yapi.

Ukiongelea Samiasm unamuongelea Samia na nini anachokiamini katika uongozi wake. Ni ngumu kumtenga kiongozi mkubwa na kile anachokisimamia.
 
Ipo tofauti ya msingi baina ya hoja na mtoa hoja.

Hakuna asiyejua kuwa huyu:

Naye ni mhuni kama wale wengine wakiwamo wa maji na Tanesco au Magufuli mgonjwa na kuwa busy na mafaili.

Mnyonge mnyongeni kwanini kumziba mtu mdomo?

Hilo katiba inakataa. Hilo ni kharam kwetu kama lilivyo kharam kwake. Anayelifanya hilo kwa hakika ni mhuni kama yeye tu!

Ieleweke hoja zenye mashiko hatustahili zinakotoka. Mbona walikuwepo kina Slaa na kina Lowassa wenye hoja?

Hoja haipigwi rungu. Polepole ana hoja.

Ni hayo tu mheshimiwa.
 
Hana hoja ni mtu anayelilia apate support ya jamii nzima. Ni unafiki kwa maana ya kwamba asingenyanganywa cheo haya asingeyaongea.

Kashindwa kukumbuka ukweli kuwa kila kitu kina mwanzo na mwisho wake. Atulie mwisho wake umeshafika.
 
Hoja haipigwi rungu. Hoja hujibiwa kwa hoja. Ndiyo ustaarabu katika Tanzania mpya tunayoitaka.

Polepole sema nao!
 
Huyu jamaa aliyemuandalia hii kanzu mbingu ataisoma tu kwenye vitabu

Ila kama ni mafunzo hawa mabwana wameyatoa kwa jamii kwa vitendo 😁😁:

Your browser is not able to display this video.

Kuchukiwa hivi si bure bali ni kuvuna walivyopanda wao wenyewe.

Hangaya na Ka telephone nao kama kondoo wanaelekea huko huko.
 
Ila pana jambo linahitaji kupigwa jicho vizuri zaidi:

Tuwatambue wanaohaha kutusambaratisha kama Taifa

Hivi kwanini kuna watu wakiona hoja ya maana huwa mnang'aka kama mnataka kutokwa na roho vile?

Cc: Evarist Chahali
Huyu ni sehemu ya uongozi wa JPM ulio na sifa nyingi mbaya hapa jamiiforum kama kuuwa watu, kuteka watu na kufanya unyama wa kila aina.

Leo hii unaongea kama vile keshakuwa malaika aliyeshuka kutoka mbinguni. Wakati mwingine hoja nzuri ni kama maua yanayopamba juu ya kaburi, huwa yanavutia sana lakini kilicholala futi sita chini yake, Mungu ndio anajua.
 
Haya ni maneno muhimu sana kutokea kwako:

".... uongozi wa JPM ulio na sifa nyingi mbaya hapa jamiiforum kama kuuwa watu, kuteka watu na kufanya unyama wa kila aina."

Hapo tuko pamoja.

Kwamba kawa malaika? Wapi unayasoma hayo?

Ninakazia, tofautisha hoja na mtu:

1. Mtu ni huyu:

Your browser is not able to display this video.

2. Hoja yake leo ni kuwa mna mlazimisha kunyamaza ambako huko ni kujibu hoja kwa rungu!

#2 wapigania haki na hasa tunaopigania kuheshimiwa kwa katiba ndipo tunapoelewana.
 
"Kaaa Kimyaaaaaa".

Mwakiilishi wa wananchi unazurura zurura hoyvo una jimbo wewe? hivi hujui anayeruhusiwa kutembelea wapiga kura wake ni mbunge wa kuchaguliwa tena aende jimboni kwake tu.

ndiyo hivyo ndugu, "kaa kimya"

Wenzio sisi tumekaa kimya kwa miaka 7 sasa, wewe siku mbili tu hizi unalalamika? kweli ? "kaaa kimya".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…