Joined
Sep 6, 2026
Posts
58
Reaction score
44
Tukiacha Mihemko, Ukiangalia Tanzania ya leo, kuna mambo mengi yanaendelea. Kuna miradi inajengwa, huduma zinaendelea kuboreshwa na mipango ya maendeleo inaendelea kuwekwa kwa ajili ya miaka ijayo. Hakuna mradi uliosinama

Tukumbuke pia maendeleo ya nchi si jukumu la Serikali pekee. Sisi wananchi tuna nafasi kubwa sana.
Usikae tu ukisubiri mambo yafanywe na mtu mwingine. Kama wewe ni mfanyabiashara, fanya biashara yako kwa uaminifu. Kama wewe ni mkulima, tumia fursa na maarifa yanayopatikana. Kama wewe ni kijana, jenga ujuzi wako na jitafutie fursa.

🇹🇿 Tanzania ni yetu sote. Kila mmoja ana nafasi na kila mmoja ana mchango.
Tushiriki. Tufanye kazi. Tusaidiane. Tulinde amani. Na kila mmoja afanye sehemu yake kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu.

Tusiseme tu “nchi ijengwe.” Tujiulize, “mimi nitafanya nini?”

Hapo ndipo uzalendo unaonekana.
Tuanze na sisi wenyewe.

Tuuombee uongozi wetu wa juu utuvushe salama, katika vipindi vyote vyenye changamoto
 
Nenda kamuunge mkono kwa kukae nae Eda pale Kizimkazi.
 
Shetani muuaji hasafishiki hata kidogo, ananuka damu za watu wasio na hatia
 
Urais wake ulikoma tarehe 29 Oktoba 2025.

Huyu unayemtaja ni mhaini kwa mujibu wa Ibara ya 8 Katiba ya JMT
 
Kwa hiyo umejiunga tarehe 6 September 2026 ili kuongeza nguvu ya kumsafisha muuaji. Huyo hasafishiki, ni swala la muda tu anaenda kulipia damu za watanganyika alizozimwaga. Damu za watanganyika ninamlilia na zitamfuata popote alipo hadi zipate haki
 
Wewe zezeta hiyo miradi anajenga Samuya na pesa zake mfukoni?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…