Tuwaache abiria wa daladala washuke kabla ya sisi kupanda

Wengine wezi.
 
Suala la ustaarabu kwenye kugombania siti sahau kabisaa.
 
Mnaotumia daladala mnatesekaee, nunueni magari jamani zipo Subaru za bei chee hadi mil 20
 
Kuna siku nilikuwa na ndugu yangu tunasubiri daladala. Kituoni tuko kama 15. Daladala kuja watu wakaanza purukushani,nikamzuia ndugu yangu nikamwambia subiri. Baada ya ile vurugu kuisha tukaingia na tukapata viti na vingine vikabaki vitupu. Watu washazoea vurugu hata wakiwa watatu watagombea.
 
😀😀

Ni issue ya mindset pia,imekua ni kama tabia,
Hata kwenye sherehe yenye buffet,kila mtu atataka yeye ndio awe mbele kuchukua chakula hata kama ameona kuna chakula kingi na kitabaki.
 
Umesema kweli lakini kwa ufahamu wangu mdogo tamaduni ni mti uliyojikita mizizi yake mbali sana ndani ardhini kuuharibu unatakiwa urisk maisha. Hilo ulilosema kwa hapa ni kama tamaduni yetu kwa kila mpanda daladala. Tuishi humo tu kwakweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…