Tuwaache abiria wa daladala washuke kabla ya sisi kupanda

Ukipanda daladala unaweza kugundua jambo lilelile kila siku: kila daladala inapofika kituo chenye watu wengi mlango umeshazibwa na watu ambao hawawezi kusubiri kupambana kwa vile viti vichache. Mara nyingi watu wanapandaga hata kabla ya watu wote kushuka.

Aidha makondakta wanachangia kuongeza kero wakirudisha change mbele ya mlango kusababisha watu wanaosubiri change kuziba mlango. Hivi vitendo ni kero kwa watu wanaoshuka lakini pia inawachelewesha watu wote wanaotumia daladala pamoja na kuwa hasara kwa wazee, wagonjwa, wajauzito, nk. ambao hawana nguvu ya kupambana kupanda daladala.

Suluhisho ni rahisi: tuache ubinafsi na tuongeze utulivu.

Tuwape watu nafasi ya kutosha kushuka na kutoka halafu tukipanda tuheshimu wenzetu. Mwisho wa siku ni faida ya sisi wote; wanaoshuka wanaweza kushuka chap na bila kero na wanaopanda wanaweza kuwahi kupanda kuliko wakipanda kwenye ile fujo inayotokea mlango ukizibwa.
Wengine wezi.
 
Suala la ustaarabu kwenye kugombania siti sahau kabisaa.
 
Mnaotumia daladala mnatesekaee, nunueni magari jamani zipo Subaru za bei chee hadi mil 20
 
Ukiachana na ustaarabu,kingine ni ubinafsi,
Na sio tu kwenye Daladala,mfano hata kuingia mpirani unakuta kila mtu anataka yeye ndio aingie kwanza kabla ya mwenzake!

Hata kwenye Mabasi ambayo kila mtu ana tiketi yake na namba ya kiti,usishangae kuona watu wakigombania kuingia,na hii tabia imekua hata kwenye kushuka,watu hugambania hata wakati wa kushuka,kila mtu anataka ashuke kabla ya mwenzake!
Kuna siku nilikuwa na ndugu yangu tunasubiri daladala. Kituoni tuko kama 15. Daladala kuja watu wakaanza purukushani,nikamzuia ndugu yangu nikamwambia subiri. Baada ya ile vurugu kuisha tukaingia na tukapata viti na vingine vikabaki vitupu. Watu washazoea vurugu hata wakiwa watatu watagombea.
 
😀😀

Ni issue ya mindset pia,imekua ni kama tabia,
Hata kwenye sherehe yenye buffet,kila mtu atataka yeye ndio awe mbele kuchukua chakula hata kama ameona kuna chakula kingi na kitabaki.
 
Ukipanda daladala unaweza kugundua jambo lilelile kila siku: kila daladala inapofika kituo chenye watu wengi mlango umeshazibwa na watu ambao hawawezi kusubiri kupambana kwa vile viti vichache. Mara nyingi watu wanapandaga hata kabla ya watu wote kushuka.

Aidha makondakta wanachangia kuongeza kero wakirudisha change mbele ya mlango kusababisha watu wanaosubiri change kuziba mlango. Hivi vitendo ni kero kwa watu wanaoshuka lakini pia inawachelewesha watu wote wanaotumia daladala pamoja na kuwa hasara kwa wazee, wagonjwa, wajauzito, nk. ambao hawana nguvu ya kupambana kupanda daladala.

Suluhisho ni rahisi: tuache ubinafsi na tuongeze utulivu.

Tuwape watu nafasi ya kutosha kushuka na kutoka halafu tukipanda tuheshimu wenzetu. Mwisho wa siku ni faida ya sisi wote; wanaoshuka wanaweza kushuka chap na bila kero na wanaopanda wanaweza kuwahi kupanda kuliko wakipanda kwenye ile fujo inayotokea mlango ukizibwa.
Umesema kweli lakini kwa ufahamu wangu mdogo tamaduni ni mti uliyojikita mizizi yake mbali sana ndani ardhini kuuharibu unatakiwa urisk maisha. Hilo ulilosema kwa hapa ni kama tamaduni yetu kwa kila mpanda daladala. Tuishi humo tu kwakweli
 
Back
Top Bottom