Ni wachache mno, wengi wao ni mkumbo tu na kufuata upepo wa fasheni. Elewa hakuna kitu kwa ajili ya kila mtu, chagua chako na ukubali. Kama ilivyo kwa wanaume, sio wote watavaa pensi.
Sketi na magauni yanawakaa poa sana, hata wale wenye maumbo ya kanda pendwa hupendeza.
Suruali sina ubaguzi. Zikigoma acha, unakuwa kituko. Tatizo watu hawatakwambia ukweli, na sio kweli kwamba hawajali eti watamaindi mambo yao.
Unajitekenya tu.
Basi sikia ushauri, au endelea kushupaza shingo ili utusaidie vichekesho vya bure tupunguze stress zetu.
Ncha Kali.