Tuwaepuke wanasiasa wanataka kutuletea ukabila kupitia uChifu

Tuwaepuke wanasiasa wanataka kutuletea ukabila kupitia uChifu

Wazee wa ambush nawaona mnavizia kila event mpinge na kukosoa tuu, hatari sana hii.
Kwani hili jambo lina umuhimu gani kwenye hii nchi?.maana yako mambo mengi ya msingi yametushinda leo tunafanya ubadhirifu wa pesa kwa jambo ambalo halina chochote cha maana kwa maendeleo ya nchi na wananchi.usifikiri wanaokosoa wanakua hawana hoja ya msingi.ila pia ata wewe hujakatazwa kusifia kila kitu.uzuri nikwamba wewe unayesifia iko siku utakuja kulalamika kwa jambo flani litakalokugusa.Mapambio hayana nafasi kwenye nchi inayopambana kujikomboa.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Sidhani kama Rais analeta issue za ukabila ila nachokiona mimi ni kuwa kwakua aliingia madarakani bila kuwa na msingi wake wa kisiasa.

Muda huu ndio anautumia kujenga msingi wake.

Hivyo tumzoee na kuzoea events kama hizo.
Msingi wakisiasa wa nini,msingi wakisiasa ni kupambana kulikomboa taifa sio kufuja pesa bila ulazima.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Kwani kwasbb ni utaratibu wa tangu enzi km unavyosema ndo unaondoa ukweli kuwa ni ,uchawi,ushirikina,mizimu?
Hii haiondoi ukweli huu,haijalishi uliwekwa na kufuatwa na nani!
Haufai kenye nchi,tunamhitaji Mungu muumba wa mbingu na nchi sio machifu

Tusiwahukumu wala kuwabeza wale waliokuwa wanaishi kwenye mfumo huo. Ulikuwa na mfumo ambao uliweka utaratibu wa mambo katika maisha yao. Hivi kwamba jamii zao zilikuwa zikiishi kwa amani na utulivu kutokana na mifumo hiyo. Lingine ambalo nataka ujue, ni kwamba wale walioishi kabla ya dini hizi kuingia wataokolewa wengi kwenye kiama, kuliko watu walioishi baada ya dini hizi mpya kuja. Maana wale walikuwa wakiabudu dini zao za jadi na Mungu alikuwa akiwasikiliza. Yeye hakuwabeza kama ilivyo sasa. Hata mtume Paulo kuna sehemu alipita na kuwakuta watu waliokuwa wakiwa katika kanisa lao lililoandikwa Kwa Mungu Asiye Julikana. Maandiko yanasema, alivyofika hapo hakuwabeza wala kuwahukumu, badala yake aliwapongeza na kuwaambie yeye amekuja kufunua kile kisichojulikana. Labda kwa kuhitimisha, watu wa dini za jadi hatupaswi kuwabeza. Ukisoma comparative religion, kuna religion family of the world. Kuna wengine wanaabudu ng'ombe kama waHindi, kuna waChina na watu kadha wa kadha. Wote hao wana dini ambazo Mungu anaziona na kuzitambua.
 
Chadema azeni na ninyi kuweka machifu kila eneo ambalo ccm kwa kivuli Cha rais inaweka
 
Ni hatari sana kiongozi kuonyesha itikadi za kikabila au kidini.
Mwanasiasa asipothivitiwa na taasisi ni zaidi ya bomu la nyuklia kwa nchi.
Niliwahi sikia marehemu alikuwa na mpango wa kuwaweka machifu kwenye pay roll rasmi; labda mrithi wake anaendeleza pale mipango ilipoishia.
 
Kwenye uongozi wa nchi Kuna mengi Sana, tusije tukajiona tunajua sana. Mpaka rais kuamua kufanya alichofanya basi ujue kuna kitu kinawekwa sawa.
Uongozi sio rahisi tumtie Moyo mama atufikishe kwenye maendeleo

Sio kwamba tunajiona tunajua sana bali tunataka kujua tu
Basi kama ni hivyo wapelekwe Bungeni wakawakilishe makabila

Na uvaaji wa ngozi huo
Ndio maana nasema wanasiasa huwa wanabadilika kabisa na kuacha dini zao
 
Kwani hili jambo lina umuhimu gani kwenye hii nchi?.maana yako mambo mengi ya msingi yametushinda leo tunafanya ubadhirifu wa pesa kwa jambo ambalo halina chochote cha maana kwa maendeleo ya nchi na wananchi.usifikiri wanaokosoa wanakua hawana hoja ya msingi.ila pia ata wewe hujakatazwa kusifia kila kitu.uzuri nikwamba wewe unayesifia iko siku utakuja kulalamika kwa jambo flani litakalokugusa.Mapambio hayana nafasi kwenye nchi inayopambana kujikomboa.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
No hard feelings, I respect your opinion Boss.
 
Tanzania ya Mwl Nyerere ilijengwa katika misingi ya umoja na ndio sababu kubwa ya kufuta uchifu.

Leo taifa letu lina zaidi ya miaka 60 tangu tupate uhuru anatokea mwanasiasa mmoja anaenzi uchifu.

Mataifa kama Uganda na Nigeria ambayo yaliendelea na uchifu yalijikuta yakipata matatizo makubwa ya ukabila kwasababu yalishindwa kumaliza tawala za kichifu.

Mungu saidia taifa letu liepukane na hili tatizo la ukabila ambalo wanasiasa wanataka kulizalisha,kulipalilia na kulikuza.

Wasalamu Ngongo kwasasa Uru Kushumundu.
Nahisi ana lengo la utamaduni zaidi kuliko uchifu. Itakuwa ni matunda ya wale wamarekani walioanda kipindi maalum, mojawapo ya masharti itakuwa ni kufufua masuala ya utamaduni.
 
Ukabila uliletwa na mwendakuzimu. Watu walianza kujitambua Kwa makabila yao badala ya utanzania wao.

Hawa machifu wapo lakini ukiachana na kupandia kwenye vuchuguu uchi wakiomba mvua, hawana chochote kwenye maamuzi ya makabila! Wala huko makwao hawatambuliki hata kwenye kutatua migogoro ya ardhi.
Chifu wa wasukuma makazi Dar, chifu wa wachagga makazi Dar, chifu wa wahehe makazi Dar. Hivyo vyeo ni ceremonial ka baadhi ya vyeo vikubwa nchini. Majoka ya kibisa hayana meno wala sumu!
 
Sidhani kama Rais analeta issue za ukabila ila nachokiona mimi ni kuwa kwakua aliingia madarakani bila kuwa na msingi wake wa kisiasa.

Muda huu ndio anautumia kujenga msingi wake.

Hivyo tumzoee na kuzoea events kama hizo.

Lakini anaujenga vibaya huo msingi maana ili kuondoa ukabila Nyerere alilazimika kufuta uchifu sasa anapouanzisha maana yake anaanzisha ukabila na anafanya hivyo sababu ndani ya chama chake kuna moto sasa anataka kutambuliwa kiukabila. Hivi hilo neno Chief si limeletwa na wakoloni waliowatumia kwenye biashara ya utumwa. Kwanini hatujiulizi hivi viongozi wetu wankimila kwanini watumie neno la kizungu na siyo maneno kama Mtwa ya wahehe kwa mfano. Hapo ni mwanzo wa ukabila utaliangamiza taifa letu. Nyerere alisema tukatae viongozi wanautumia ukabila udini na kuandaa kama njia ya kukubalika.
 
Back
Top Bottom