Nawasalimu kwa jina la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
Hizi siasa za Uchifu sio siasa salama kwa mustakabali wa nchi.
Kwanza yale maguo yenye ngozi za chui sijui wameyatoa wapi!
Niseme tu kwamba, Tanzania hakujawahi kuwa na machifu kwa muktadha wa uongozi wa kitaifa.
Machifu wa Tanzania walikuwa ni tawala chache tu ambazo zilikuwa huko kwa watu wa iringa zamani hizo.
Baadae wakoloni walipokuja, wakaunda vikundi vya wahuni wachache miongoni mwa watanzania kisha wakawavika uchifu for the benefit of white man. Hawa ndio waliohusika kuwauza wenzao utumwani.
Huu uchifu wa sasa wa Samia, sio uchifu haswa. Ni vikundi vya wachawi wanaomsimika Hangaya kwa kumpa mamlaka na utii. Ni power transfer ama alama ya utii katika mamlaka za wachawi.
Wachawi hawa wako nchi nzima. Wamejivika uchifu bandia ili kuficha sura zao halisi.
Kila mahali Rais anapopita wanamvika maguo ya kichawi.
Jamani, nchi hii inamuhitaji Mungu. Tuache kutegemea viumbe dhaifu kama mizimu.
Mungu wetu ni Mungu mwenye nguvu sana, lakini anahitaji watu wanyoofu.
Shida yenu nyinyi ni majizi na watu wa konakona, ndio maana mmemkimbia Mungu mkajikabidhi kwa viumbe wachafu na dhaifu kama majini na mizimu.
Mrudieni Mungu mwenye nguvu na mamlaka, mzitii amri zake na yeye awafanye kuwa wake.
Hayo maguo ya mizimu hayawezi kuwasaidia lolote. Mnajidaganya.