Wasaidizi wa Rais naona wanaendelea kumpoteza tu kwa kila namna, walianza kwenye zile teuzi anateau leo kesho anatengua, naona mpaka sasa bado Rais anakosea mambo mengi, nadhani nae binafsi anastahili kubeba lawama.
Anatakiwa awe anajiuliza kama hayo anayokwenda kuyafanya yana maslahi kwa taifa au ndio yataligawa taifa, hilo jina chief Hangaya alipewa akalipokea naona amenogewa sasa anataka kuendeleza hiyo tabia kwa mikoa yote Tanzania.
Haya mambo hayana maana, tuna wakuu wa mikoa, wilaya, wakurugenzi nk hawa machifu wanaolazimishwa kuwepo sasa kazi yao ni ipi? au ni urembo tu, kwamba wanatambuliwa uwepo wao japo hawana kazi? mikoa ya Tanzania ina mchanganyiko wa makabila mengi sasa hivi, hii biashara anayoleta Rais ni kuturudisha nyuma tu kifikra wakati tulishatoka huko zamani.