Tuwafahamu Watu Maarufu waliokuwa wanatajwa sana na Wanamuziki wa Band nchini Tanzania

Tuwafahamu Watu Maarufu waliokuwa wanatajwa sana na Wanamuziki wa Band nchini Tanzania

Nyoshi mselela
Hussein makabureta
Yussufu mbwana
Badi bakule
JONA MVAMBA(shabiki wa twaga pepeta)
Hadija mnoga kimobitel
 
Acha ubishi mzee mwenyeji wa Arusha wote hakuna asie mjua Hidaya tena alikua maarufu kwa jina la Hidaya Wa pepe kale kafariki mwaka jana , Hidaya ni miongon mwa wanawake matajiri wa Arusha enzi hizo, ameishi pia france ninavyo kueleza kafariki mwaka jana elewa hivyo
Alafu mi nazungumzia wimbo wa pepe kale Hidaya hiyo ya kwako ya Hedaya mimi siijui
jamaa amekaza fuvu kwa kitu kilicho wazi
 
Kuna kina Said Komolie sijui alikuwa nani huyu
saidi commorie alikuwa ni producer wa mziki.
kiasili jamaa kwao ni visiwa vya commoro.

kwa miaka ile, jamaa alikuwa ni mmoja wa maproducer wakali sana. studio yake ilikuwa inaitwa big town production, ofisi zilikuwa kananga street, mitaa ya kinondoni morroco.

kwa sasa anaishi ufaransa. kuna story inahusishwa na kuondoka kwake nchini, maana jamaa aliondoka ghafla sana kama kama mkimbizi.

wapo wanaodai jamaa alikuwa anatoka kimapenzi na mke wa kigogo mmoja wa wakati ule.

yule kigogo akamtishia kumfanya jambo baya sana ila akampa muda mfupi awe ameondoka nchini la sivyo atakumbana na hatari. jamaa akaondoka nchini kimyakimya bila kupenda na mpaka leo hajakanyaga tena.
 
1.Fikiri Madinda
2.Pedeshee Mudi Nondo
3.Moris Mariaga
Hapa pedeshee kidogo ni #3,hao 1&2 walikua ni janja janja tu,tuliowahi kuishi nao Sinza_Madukani tunawajua vizuri
Huyo Mudi Nondo BSS aliyoshinda Jumanne Iddi,nafikiri ilikua ndio BSS ya kwanza,siku ya Fainali aligawa pesa hatari,cha kushangaza nyumba aliyopanga ilikatiwa umeme kwa kushinda kulipa bili kwa wakati(enzi hizo hakuna LUKU) [emoji38][emoji38][emoji38]
Fikiri Madinda aliishi kwenye upangaji na nyumba ya kawaida mno tofauti na jina alilokuwa nalo mjini.
Fikiri Madinda Mimi ndiyo Boss wake hapa Kilimo na Ushirika Dodoma. Ni Dereva wa Wizara ya Kilimo na Ushirika, hataki kabisa umuite Papaaa Fikiri Madinda NI swahiba mkubwa Sana na RC wa DSM wa Sasa hivi
 
Fikiri Madinda Mimi ndiyo Boss wake hapa Kilimo na Ushirika Dodoma. Ni Dereva wa Wizara ya Kilimo na Ushirika, hataki kabisa umuite Papaaa Fikiri Madinda NI swahiba mkubwa Sana na RC wa DSM wa Sasa hivi
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
mziki wa dansi ulikuwa na mambo matatu

kwanza kulikuwa na mapedeshee hawa watuzaji
ndio hao aliowataja mtoa mada

halafu kulikuwa na mashabiki damu
kama hapo unemtaja
MAMA MINGOI CHESCO MAZEE WA MATUNDA kuna pia Kina MANKA MUSHI
ambao ndo waliikuwa navijiwe vyao au CAMP zao
karanga camp
HOME ALONE
VINGUNGUTI TIMBERLAND
DALADALA CAMP
SWAZI INTER
n CAMP nyingine nyingi sana
ambazo hizo CAMP zina mashabiki haswa na mapedeshee wajanjawajanja ndo zilikiwa maskani zao na watoto wa mjini na wakati mwingine hata wanamuziki wenyewe pia huweka vijiwe katika hizo CAMP
hizo CAMP kulikuwa na mashabiki WAZARENDO
nakumbuka kuna SHABIKI MMOJA wa VINGUNGUTI TIMBERLAND huyo Mdau alikuwa anaipenda sana TWANGA kiasi alikuwa mpk anapanda NDEGE kuifuata TWANGA ikiwa NJE ya MKOA haswa ARUSHA au MWANZA

halafu kundi Jingine sasa ni la wanaofanikisha BENDI kuwa na Mziki bora

mfano HUSSEIN MIUNDOMBINU
huyu alikuwa fundi mitambo(umeme)
Twanga popote itakapopiga huyu alikuwa anahakikisha mambo yote ya umeme yako sawa mziki unatoka vizuri

THABITI MTOTO ILALA huyu alikuwa mkali wa kucheza na Keyboad

lakini pia kulikuwa na mkali mwingine wa KEYBOAD
ukisikia PROFESHENARI TARIBONARI VIctor mkambi huyu mkali wa KEYBOAD hata kama akifa inapaswa TWANGA wamjengee Sanamu lake maana alikuwa PROFESHENO haswa kaipaisha sana twanaga na UFUNDI wake wa KEYBOAD


Ukisikia MCD basi hapo anatajwa SUDI MOHAMED TIMBO(marehemu)
huyu alikuwa mpiga tumba matata sana

halafu ukisikia SHAKASHAKA SHAKUZURU hapa alikuwa anapaishwa MIRAJI SHAKASHIA huyu ni mpiga gitaa matata sana

halafu kulikuwa kulikuwa na mkung'uta DRUM hatari sana BABA DIANA BABAA SHARIFA BABAA ZAITUNI basi alikuuwa anatwaja ABUU SEMHANDO mpiga DRUM hatari

sasa utakuj kugundua kulikuwa na makundi matatu yalikuwa yanatwaja sana kwenye nyimbo
wngine walikuwa mashabiki damu wengine ndi hao watu wa wanamuziki wenyewe
umetisha sana[emoji123]wewe mwenyewe kwanza ujengewe sanamu kuchambua vema hizi mambo[emoji120]
 
Nadhani hizi FM station kidogo zilishindwa ku promote muziki wa dance.

Mussa mzee wa korosho huyu ndio babake na Jux mwimbaji. Huyu maarehemu

Dr Ayoub siki hizi nadhani ni Profesa Ayoub wa magonjwa ya akili

Pedeshee Ndama Mtoto wa Ngombe aka Akayesu huyu bado tajiri sana

Papa musofe chuma cha reli mbongo wa kwanza mjanja kuvaa pure gold nyingi mkimya kwa haiba lakini ana akili za kimafia za hela hatari. Huyu kuna sehemu akifika na gari hashuki hapendi macho ya watu sana.

Papa Davis Mwangaba mzee wa Temeke huyu alikuwa anatembea na millioni kadhaa kwemye buti la gari. Kaka yake ndio mwenye mbumba ya hatari mzee Mwangaba tajiri wa Temeke

Papa Muddy mas mzungu wa roho kawasafirisha washikaji kibao kwenda ulaya waliokuwa wana hustle town na hawakuwa na uwezo wa safari kwenda kujilipua ulaya

Wazee wa TCC kuna mwamba mmoja walikuwa wanamuita Abrahamovich naye alikuwa na mbumba za kusumbua kiumeni TMK area.
Papaa Davis Mwangaba alikuwa cha mtoto Kaka ake aliitwa Enock Mwangaba, huyu Mzee ndiyo mmiliki wa Spice Hotel iliyopo Adjacent na Ofisi za CCM LUMUMBA, huyu Mzee alipata tenda ya ku-supply beer za TBL Enzi Hizo akiwa ni transporter wa malori Aina ya Fiat-Mbaula Sasa hivi anaishi white house, anayo pesa bado..!
 
Nje ya mada kidogo kulikuwa na mpiga kinanda maarufu sana anatajwa sana kuanzia miziki ya dansi mpaka taarabu. Huyu si mwingine bali ni Thabit mtoto wa Ilala
Andrew Sekidea mama yake alikuwa Mwalimu wa Shule ya Msingi Ubungo NHC huyu mwamba ndiyo nguzo ya Twanga Pepeta Enzi Hizo, alikuwa ni hatari sana
 
Back
Top Bottom