Tuwafahamu Watu Maarufu waliokuwa wanatajwa sana na Wanamuziki wa Band nchini Tanzania

Tuwafahamu Watu Maarufu waliokuwa wanatajwa sana na Wanamuziki wa Band nchini Tanzania

Michongo yote ilikuwa inaletwa na wahusika wenyewe kama ni bandari,tra,ttcl nk
Sasa watoto wa mjini kazi kwao
Ni kama wanatumika tu

Mjini kuna mambo mengi
Unaweza ukawa sehem au ukapatwa
Na shida fulani hujuwi wapi uanzie

Nakumbuka kulikuwa na watu wao kazi yao ni mambo ya dhamana ya kesi yyt ila syo ya kuua au bunduki
Mjini mipango

Ova
Ni kweli mkuu
Kuna wazee wana hati mkononi kwa ajili ya bond ya mahakama
Ni wewe na pesa yako tuu
Mahakama kama kisutu ndio kilikuwa kilinge chao
 
Ahsante kwa masa
Uncle Saleh huyo sidhani kama ni Ali Saleh mwandiahi wa habari. Huyu alikuwa akiitwa Saleh Jabir??, (kama nimepatia jina la ubini wake) maarufu uncle Saleh mtangazaji wa TVZ enzi hizo akitangaza kipindi cha miziki na dada mmoja akiitwa princess Selme.
👏👍
 
Mamaa Dotnata:
Bila shaka wengi mnamkumbuka, aliwahi kuwa muigizaji maarufu kupitia ITV, baadae akaingia kwenye ujasiriamali wa kutoa huduma za catering, shughuli hizi zilimpatia mafanikio sana. sijui kwa sasa yupo wapi huyu mama. FM Academia waliwahi kumtungia wimbo wenye jina lake.
Hapa umechapia: Dotnata ni mapacha, anayefanya cataring ni mwingine na aliyekuwa msanii ni mwingine
 
last week nilipita ile mitaa, aisee mitaa imepooza sana. zile mishemishe za miaka ile hakuna tena.zile vurugu za mission town hazipo tena.

nadhani imetokana na mji kutanuka na kusambaa kwa kuduma za kiserikali mpaka huku chini kwenye kata.

siku hizi baadhi ya huduma sio lazima uzifate mjini posta kama zamani. hususan huduma za kupata vibali, leseni za biashara, passport nk. kila kitu kinapatikana kwenye ngazi za wilaya.
Na kuondoa malipo ya cash serikalini kumesaidia sana, halafu siku hizi nyaraka za kawaida zinapatikana mpaka mtandaoni. Mambo ya mihuri nk hayana dili siku hizi.
 
uzi nimeufurahia umenikukusha mbali
1.chalz mtawali nilikutana nae ofisini kwake yard ingine ilikuakama unatoka kinondoni unaenda morroco ile yard ingine ya kule morroco haikua ofisi yake tulifanya kazi poa sana jamaa mtu poa sana
2.judy moshi ni mshkaji wangu sana sa hv anakaa goba na ana mishe zake nyingi
 
baraka kapuya alikuwa anatajwa sana na wanamuziki wa kundi la akundo sound.

mmiliki wa akudo alikuwa ni prof. juma kapuya ambaye wakati fulani aliwahi kuwa waziri wa elimu na mbunge.

inawezekana huyu baraka ni family member au mtoto wa mzee kapuya. wajuzi wa mambo watajazia nyama.
Huyo Baraka kapuya full boss sasa hivi yuko Urambo kaliua tabora huko kuna lodge ana simamia
 
1.Fikiri Madinda
2.Pedeshee Mudi Nondo
3.Moris Mariaga
Hapa pedeshee kidogo ni #3,hao 1&2 walikua ni janja janja tu,tuliowahi kuishi nao Sinza_Madukani tunawajua vizuri
Huyo Mudi Nondo BSS aliyoshinda Jumanne Iddi,nafikiri ilikua ndio BSS ya kwanza,siku ya Fainali aligawa pesa hatari,cha kushangaza nyumba aliyopanga ilikatiwa umeme kwa kushinda kulipa bili kwa wakati(enzi hizo hakuna LUKU) [emoji38][emoji38][emoji38]
Fikiri Madinda aliishi kwenye upangaji na nyumba ya kawaida mno tofauti na jina alilokuwa nalo mjini.
Kulikuwa na daladala zinaitwa Madinda Trans je zilikuwa zake? Halafu jamaa nadhani alishadanja. Aliwahi kuishi na Aisha Mbegu (Aisha Madinda) ila walikuja kuachana
 
Huyu gwiji (RIP) ni pedejee pekee kutokea pande za TMK alikuwa na gereji Temeke kisha akawa na daladala zinaitwa Kitendawili. Baadae alihamia Sinza Morina kumuoa Amina Chifupa wa Mpakanjia
Aisha alikuwa pisi kweli
Sema ngada tu ilimuaribu

Ova
 
Kuna mwamba wankuitwa Bosco mitaa ya akina Ntimizi, ukitaka pass ya kusafiria ni ndani ya siku tatu tuu, ukitaka kwenda ulaya ni pesa yako tu,akatangaza kwenye daily news kuwa Kuna scholarship kusoma marekani foarm 20k, kakusanya izo 20k then akakimbia, nasikia alikuwa mganda jamaaa.
Wapi Ras D mtoto wa Sinza, Wapi fransisi moshua Mzee wa madini Arusha?
 
Huyo ni wa kizazi cha sasa cha machawa.

ni aina ya vijana ambao majina yao yamefahamika kwa msaada mkubwa wa social media hususani instagram.

bila mitandao ya kijamii, hakuna ambaye angewafahamu.

Wakati akina Msofe wanasumbua mjini, yeye alikuwa primary may be.
Msofe ni zulumati
 
Back
Top Bottom