Tuwafahamu Watu Maarufu waliokuwa wanatajwa sana na Wanamuziki wa Band nchini Tanzania

Luiza alikuwa machine
Sema mm bado naliaga na aisha

Ova
AISHA ulimbukeni wa uzuri ulimzuzua
alivyokuwa mnenguaji TWANGA kila pedeshee alimtaka yeye sas alivyoingia kwenye madawa ndio kabisa akaanza kupoteza
analetwa MWANANYAMALA HOSPITAL hoi taabani hakuna pedeshee hata mmoja aliyekuja hata wanamuziki pia mana walimsaidia mpk wakamchoka mpaka KIFO kikamchuka ni cha kudhadhalilika sana
sema nini MUNGU ndio anapanga KIFO
ingekuwa EDHI ya sasa kunywa madawa kidogo ingekuwa ahueni na hili la kunywa madawa ndio lilimsaidia RAY C ama sivyo angekufa KIFO KIBAYA sana kama cha AISHA

ila watoto wa siku hizi ukiwaambia Edhi zetu za dansi
wanenguaji walikuwa wanasajiriwa na kuhama kwa DAU kubwa la uhamisho kama wachezaji mpira
na MNENGUAJI aliyewahi kuvunja RECORD kwa dau kubwa la uhamisho ni QUEEN SUZY
hio ilikuwa ni jeuri ya mapedeshee bwana
 
Ndama mtoto ya ng'ombe maisha haya yana leo na kesho
 
yeah uncle wangu rip ndo zilikua mishe zake, yeye mtu wa nje lakini ndo anadirect mtu wa wizarani kama fungu liliwe au la moto limetegeshwa hahaha.. kipindi hicho hamna control number kaka..risiti za njanoo..
Hata watu wa clearing nao zamani wanamkadiria tu mteja
Mzigo wako unatakiwa kulipia tsh kadhaa,wajinga walipiga hela sana
Wengi ndomana ngwengwe iliwaondoa
Sahv kila kitu kipo kwenye system,uramchomekeaje mtu sasa

Ova
 
Qeen suzy umenikosha mzee

Yah aisha akili za kushikiwa ttz

Ova
 
Alikuwepo yule jesca
Alikuwa smart sana alikuwaga
Na bwana mzungu

Ova
mpaka NOW kaolewa yupo mbele
JESCA aliwahi simulia yule mzungu walikuwa wanakutana sana HOTELINI
sasa siku 1 mzungu akamuambia nataka twende kwako JESCA akamuambia kwangu wewe hupawezi akamjibu nimekupenda hvyohvyo na maisha yako
JESCA akaona sio kesi baada show kuisha wakaenda GHETO kwa AISHA mwananyamala kisiwani mitaa mchangani kma sikosei
kimbembe asubuhi mzungu anataka KUNYA kakutana na choo cha shimo dadeki hawezi na mavi yamembana
ebwana eeeh muda huo akamuambia BIDADA tafuta NYUMBA haraka me narudi HOTERINI hadi JIONI ipatikane akampangishia ushuani mikocheni kama sikosei
ndio ikawa NJIA YA KUTUSUA JESCA mpak now yupo mambele huko
 
Haha nakumbuka alimpangishiaga mitaa jirani kanisa kwa pinda
Nlikaa naye jirani wkt fulani
Jesca alikuwa anajielewa sana
Ukiongea naye anaongea kma dada,ushauri kibao

Ova
 
Mkuu wewe lazima ni msomi mbobezi katika fani ya uandishi hongera san
mimi ni mkulima tu huku rufiji ndg yangu. sina usomi wowote, elimu yangu ya kuunga unga tu.

again, let me thank you for your words of encouragement, i'm humbled my brother.
 
Wasanii waliishi kwa kubweteka

Ova
 
Du umenikumbusha nimepiga sana simu za nje za michongo pale Magomeni Mikumi palikuwa na ukumbi wa dansi sijui Dar one nimeshasahau kitambo , pia namkumbuka fundi Yahaya maarufu sana miaka ile ya BlackBerry kufungua zilizokuwa locked ili kujiunga kwa mwezi, pia wafanyakazi wa TTCL Extelcome walikuwa kama ndio wa TRA walipiga sana dili za simu za kupiga nje, shukrani kwa kunikumbusha mengi ya nyuma.
 
Ilikuwa balaa
Nliwaunganisha sana
Mdosi gani nsiyemjua mjini
[emoji1] wakati ule

Ova
 
Twanga ya Mango! jamani we acha tu, miuno ya akina Aisha Madinda,Jesca likiisha dansi saa kumi lazima utafute kimeo kwenda kulipiza... na vimeo vilikuwa vya kumwaga.
Burdan ilikuwa

Ova
 

michongo yote ambayo hawa mapedeshe na wajanja wa mujini wa zamani walikuwa wanapiga ilikuwa inafahamika vizuri tu na vijana wa Tiss.

shida ni kwamba kwa utawala ule wa JK ilikuwa hakuna mtu wa kumfunga paka kengele kwasababu the whole system was corrupt.

halafu hawa mapedeshee kwa kugundua weakness hiyo, wakajipenyeza mpaka kwa wakubwa wa hao vijana wa Tiss na jeshi la polisi. wakipiga madeal yao, mgao ulikuwa unaenda kwa wakubwa.

kwa mfano afande alfred tibaigana wakati huo akiwa RPC wa dar es salaam, alifaidika sana na matukio ya upigaji ya hao majamaa.

kuna kisa kimoja niliwahi kusimuliwa, msofe aliwapiga waisrael mamilioni ya fedha baada ya kuwauzia almas fake.

wale waisrael walihangaika sana kutafuta haki yao. hilo suala lilipofika mezani kwa tibaigana likafia hapo. jamaa wakarudi kwao kichwa chini.
 
Huyo Moris Mariaga Rais wa sinza sikuhizi amefulia Ile mbaya anapanda daladala dili zake zilibuma baada ya jiwe kushika hatamu alikuwa akishirikiana na wafanyakazi wa mabenki na makampuni kufoji nyaraka
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Hawa wapiga dili ndio walifurahi kifo cha hayati
 
Ni vema tukajikita kwenye uzi , ambao unataka mapedeshee wa kibongo , mkitaka hivyo tutaanza kutaja akina JOKHA KABENGELE wa Kinshasa .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…