Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jamaa si ndio alikuwa BOT? Anatoa zawadi za magari mekundu? Shigongo amepiga sana hela kwa kuandika habari zake kwenye magazeti yake kipindi kile hakuna smartphone [emoji23]Mkuu wangu,sijasikia kabisa story za Liyumba na mtoto wake Mose pale Magomeni plus mwanae aliyeshikwa na poda kule Lindi yule Linda
Ndio alikuwa anagawa magari mekundu [emoji23]Moreen alishatoka,alibaki bwana wake
Lyumba jinga tu yeye aliiinvest
Sana chini....
Ova
Asante sana Kwa hiliPDG= Pe De Gee (tamka Jee)
P= Presidente
D= Director
G= Geral
Waingereza wanamuita CEO
Nalog off Z
Watu wabishi tu, ni kweli huyu mama alikuwa mrembo haswa na utajiri wa kutosha. Watu hawataki kuamini kuwa Kazaa na Pepe kale ni wale wa mbali na Mkoa.Acha ubishi mzee mwenyeji wa Arusha wote hakuna asie mjua Hidaya tena alikua maarufu kwa jina la Hidaya Wa pepe kale kafariki mwaka jana , Hidaya ni miongon mwa wanawake matajiri wa Arusha enzi hizo, ameishi pia france ninavyo kueleza kafariki mwaka jana elewa hivyo
Alafu mi nazungumzia wimbo wa pepe kale Hidaya hiyo ya kwako ya Hedaya mimi siijui
Uko sahihi mkuu!Huyu si aliuwawa kwenye ujambazi Morogoro?
Vijana WA mikoani BanaLe Mutuz siyo mzee bhana.
Kuwapiga Waisrael wapenda dili napo ilikuwa thubutu kubwa. Kuna Waziri wa zamani Kenya anaitwa Nicholaus Biwott (merehemu kwa sasa), alikuwa na nguvu kubwa sana kwenye utawala wa Rais Moi na akiwa mfanyabiashara mkubwa aliwapiga Waisrael flani miaka ya mwanzoni 90, jamaa kuanzia wakati huo alikuwa hamuamini mtu yeyote mpaka anafariki, alikuwa anaweza kubadilisha hata magari matatu kwa siku. Yaani hata yeye mwenyewe hajiamini. Alijua iko siku jamaa watamrudia!!Inasemekana ni mke wa waziri mkuu wa Israel yule aliyekuwa kwenye koma mda mrefu ndio aliingizwa mjini
Kutokana na wao kuja kimagumashi msala ukawa hauna nguvu sana kwa kuchafua reputation ya nchii
Pia kuna wakili mmoja ndio alikuwa nyuma ya kina msofe ku endooze stamp na signature
Currently huyu wakili alisha rudisha namba kwa sir GOd
msofe alivuka mstari mwekundu. ila jamaa enzi zake alikuwa na uthubutu aisee, kuwapiga mpaka waisrael!!.Kuwapiga Waisrael wapenda dili napo ilikuwa thubutu kubwa. Kuna Waziri wa zamani Kenya anaitwa Nicholaus Biwott (merehemu kwa sasa), alikuwa na nguvu kubwa sana kwenye utawala wa Rais Moi na akiwa mfanyabiashara mkubwa aliwapiga Waisrael flani miaka ya mwanzoni 90, jamaa kuanzia wakati huo alikuwa hamuamini mtu yeyote mpaka anafariki, alikuwa anaweza kubadilisha hata magari matatu kwa siku. Yaani hata yeye mwenyewe hajiamini. Alijua iko siku jamaa watamrudia!!
Upigaji ni hatari sana, ni kama kujitoa mhanga. Bora mara mia upige mishe za magumashi kama connection za vibali, mihuri nk. Unaweza kupiga mahali na ikawa ndiyo safari yako ya milele, na vile pesa huwa inawasha! ukipiga unataka kila mtu akujue, hiyo kwa wengine ni kama dharau. Nairobi sasa hivi kuna kama trend, wapigaji kila siku wanaokotwa.
Mkuu undugu upo..mama yake merrey na islam bharabou ni dada wa damu wa mzee said salim bhakresa....mzee ally bharabou ndio baba yao na ndio shemeji wa bhakresa ...mengine nawachia wao.Balhabou hana undugu na azam
Wakina balhabou asili yao moro
Huyu alikuwa anachezea hela maana
Walikuwa na line ya mafuta ya trasit
Kuna mkubwa fulani walipozinguana nao akawakatia line
Ila kwa mate ndomana aliyokuwa anafanya merey hata warabu wenzake
Walikuwa wanamshangaa
Ova
upo sahihi ndg yangu, ni kweli merrey na bakhresa ni ndg wa damu. na huo ndio ukweli, mengine tuwaachie wenyewe.Mkuu undugu upo..mama yake merrey na islam bharabou ni dada wa damu wa mzee said salim bhakresa....mzee ally bharabou ndio baba yao na ndio shemeji wa bhakresa ...mengine nawachia wao.
Mwaka jana alikua anamuendesha mbunge wa kule loliondo now marehem, jamaa ni mzee wa totoz ngozi imechoka inaonekana kameza jiwe sema njugu zinamsaidia.Ni dereva Wizara flan hapa tz
Asia Hussein (Simjui),Wakati Mustahiki Meya wa Jiji Allan Mulumba Kashama anatuchezesha Dar es salaam kibinda nkoyi ndani ya Silent in Mwenge ulikuwa darasa la ngapi?
Unamjuwa Joseph Rwegasira?
Msofe nilikuwa naonana sana na Mpambe wake mmoja akiitwa Ally Kitobo mdogo wake Ally aliitwa Nuhuh huyu ndiye tuliyekua karibu sana tukiishi wote Magomeni Makuti Akachube Road kipindi bado pakiitwa Somanga pamoja na jamaa zangu Yahya na Danny Malumbo (Mungu amrehemu Yahaya tumemzika kwao Kondoa Feb mwaka huu alipata ajali Tanga na IST akielekea Holili) kila ijumaa pale makutano ya mitaa ya Livingston &Amani kuna bibi alikuwa anaitwa Bi Jang’ombe alikuwa mpishi wa biriani tamu sana so tulikuwa tunaenda kula biriani la offer kutoka kwa Msofe ila jamaa sikuwahi kumuona.Nadhani hizi FM station kidogo zilishindwa ku promote muziki wa dance.
Mussa mzee wa korosho huyu ndio babake na Jux mwimbaji. Huyu maarehemu
Dr Ayoub siki hizi nadhani ni Profesa Ayoub wa magonjwa ya akili
Pedeshee Ndama Mtoto wa Ngombe aka Akayesu huyu bado tajiri sana
Papa musofe chuma cha reli mbongo wa kwanza mjanja kuvaa pure gold nyingi mkimya kwa haiba lakini ana akili za kimafia za hela hatari. Huyu kuna sehemu akifika na gari hashuki hapendi macho ya watu sana.
Papa Davis Mwangaba mzee wa Temeke huyu alikuwa anatembea na millioni kadhaa kwemye buti la gari. Kaka yake ndio mwenye mbumba ya hatari mzee Mwangaba tajiri wa Temeke
Papa Muddy mas mzungu wa roho kawasafirisha washikaji kibao kwenda ulaya waliokuwa wana hustle town na hawakuwa na uwezo wa safari kwenda kujilipua ulaya
Wazee wa TCC kuna mwamba mmoja walikuwa wanamuita Abrahamovich naye alikuwa na mbumba za kusumbua kiumeni TMK area.
kuanza leo leo, huu uzi unakupa heshima kwa kupewa title mpya "Wewe ni Mwana dareslaam nyota 5, born town.Msofe nilikuwa naonana sana na Mpambe wake mmoja akiitwa Ally Kitobo mdogo wake Ally aliitwa Nuhuh huyu ndiye tuliyekua karibu sana tukiishi wote Magomeni Makuti Akachube Road kipindi bado pakiitwa Somanga pamoja na jamaa zangu Yahya na Danny Malumbo (Mungu amrehemu Yahaya tumemzika kwao Kondoa Feb mwaka huu alipata ajali Tanga na IST akielekea Holili) kila ijumaa pale makutano ya mitaa ya Livingston &Amani kuna bibi alikuwa anaitwa Bi Jang’ombe alikuwa mpishi wa biriani tamu sana so tulikuwa tunaenda kula biriani la offer kutoka kwa Msofe ila jamaa sikuwahi kumuona.
Huyo Ally dereva wake ndiye aliyekuwa mshika pesa ilikuwa siyo ajabu kumkuta anashuka na 2Mill kwenye gari kwa ajili ya matumizi mbalimbali,hela yake unaifadi akikupa kazi aisee nilikuwa naamkia shikamoo nyiingi mwisho naondoka na 50K maisha yanaenda kuna siku alinipa 100,000/= ya kununua Big G original kwa ajili ya kulia mirungi sasa packet sikumbuki exactly ilikuwa bei gani ila haikuzidi Tsh 12,000/= nikajiuliza ninunue ngapi sasa nikamuuliza mdogo’ake Nuhuh ninunue ngapi akaniambia chukua moja tu change tukagawana then hakuna aliyeuliza.
Jamaa hata kama hela zao zilikuwa chafu Ila mtaa waliuchangamsha kweli kweli,Msofe kabla hajang’ang’aniwa na mamlaka alikuwa na BMW X3 metallic gold kali sana haizimwi muda wote ipo on.
Kuna Said Janguo mzee....Saidi Janguo Muzee ya Texas😀Awali ya yote nitangulize angalizo kwa vijana ambao maturity stage imewakuta miaka hii ya mitandao ya kijamii. Itabidi msome kimyakimya huku mkiwa mmeshika peni na karatasi kuchukua notes.
Huu uzi ni wa sisi ma-seniors, maudhui yake yatagusa zaidi vijana wenzangu ambao maturity liwakuta kuanzia late 90s to early 2000s.
Mwaka 2002 mpaka 2012, mziki wa dansi ulikuwa upo kwenye prime time.
Kwa uchache tu, band zilizotamba ni FM Academia, Akudo Impact, Twanga Pepeta na Diamond Musica. Zingine zilikuwa zinaibuka na kupotea ndani ya muda mfupi.
Umaarufu wa hizi band ulienda sambamba na trend ya wanamuziki kutaja majina ya baadhi ya watu kwenye mashairi yao.
Majina ya hawa watu yalivuma na kuwa maarufu kuliko sura zao kwasababu miaka ile kulikuwa hakuna social platform za ku-share picha na video kama ilivyo hivi sasa.
Kutokana na kujichanganya kwangu ukijumlisha na ujanja wangu wa kimjini mjini wa miaka ile, nilifanikiwa kufahamiana na baadhi mapedeshee au wazee wa mujini ambao majina yao yalikuwa yanatajwa kwenye mziki wa dansi.
Nitataja ninaowakumbuka na wewe ongeza wa kwako.
Naandika majina yao kama yalivyokuwa yanatamkwa kwa mbwembwe na wanamuziki.
Kwa mfano kama mtu alikuwa anaitwa John, wanamuziki walikuwa wanatamka papaa John Young Millionaire Muzee ya ma-Range Rover[emoji3][emoji3].
Haya twende kazi:
Pedeshee Mychoice na kati ya Mbeya:
huyu sijui alikuwa anapiga mishe gani huko Mbeya, watu wa Mbeya mtatusaidia.
Braza K na kati ya Tunduma:
Watu wa Tunduma mtatusaidia kutujuza kuhusu huyu jamaa, alivuma sana.
Mamaa Rukia Soloon:
Huyu bibie namfahamu, ana saloon yake ya kike mitaa ya Mikocheni barabara ya Rose Garden. Those days she was very pretty, kwa sasa utu uzima umemchukua.
Mamaa Dotnata Decoration:
Bila shaka wengi mnamkumbuka, aliwahi kuwa muigizaji maarufu kupitia ITV, baadae akaingia kwenye ujasiriamali wa kutoa huduma za catering, shughuli hizi zilimpatia mafanikio sana. sijui kwa sasa yupo wapi huyu mama. FM Academia waliwahi kumtungia wimbo wenye jina lake.
Mamaa Juddy Moshi:
Alikuwa mmiliki wa band ya Daimond Musica kwa financial support ya mshua mmoja ambaye alikuwa ni MD wa Yellow Pages, watu wa zamani wanaelewa. Juddy alikuwa mrembo si kitoto, kwa sasa umri wake umesonga mbele.
Pedeshee Akayesu Ndama Mutoto ya Ng'ombe:
Sina haja ya kumuelezea, ni mtu maarufu wa nyakati zote. Wajanja wa mujini watamuelezea zaidi. Jina lake lilitajwa sana kwenye nyimbo za dansi zilizovuma.
Young Millionaire Bill gate Muzamir Katunzi:
Christian Bella aliwahi kutunga mpaka wimbo wenye jina hilohilo la Muzamir Katunzi. I don't know him personally, but it's told he was financially successful.
Papaa Msofe Chuma cha Reli hakishiki Kutu.
Sina haja ya kuandika mengi kuhusu umaarufu wa Papaa Msofe. Itoshe tu kusema jina lake liliimbwa sana halafu ni wachache waliokuwa wanajua sura yake. Walianza kuiona kwenye media alipokuwa anahudhuria viunga vya mahakama kujibu kesi yake.
Papaa Martin Kasianju.
Ni marehemu kwa sasa, huyu mshua ndio alikuwa mmiliki wa Band ya FM Academia. Nilikuwa namfahamu personally. licha ya kwamba alikuwa ni mjasiriamali na muajirwa Serikalini, pia alikuwa ni Senior Officer wa Idara ya Usalama wa Taifa.
Andrew Traders na Kariakoo Big Supply: Jamaa alikuwa ni mfanyabiashara wa kuuza tairi za gari Mtaa wa Agrey Kariakoo huku akipiga michongo yake ya "general supply". Watu wa mujini wa zamani wanaelewa vizuri maana ya kampuni kusajiliwa kwa jina la general supply. Katika biashara ya kuuza tairi, alishirikiana na kaka yake, ila yeye akawa maarufu zaidi na akaaminika na wadau.
Kinje Mutoto wa Mujini:
Najua wengi mnamfahamu na zile deal zake alizokuwa anapiga. sina haja ya kumuelezea zaidi.
Pedeshee David Kabunga:
Sifahamu alikuwa ni nani, jina lake lilikuwa linatajwa sana.
Papaa Ally Kileo:
He was a prominent lawyer in town, jina lake lilikuwa linatajwa sana kwenye nyimbo za dansi.
Papaa Mutarika Mzee wa Mambo mengi:
Binafsi simfahamu, wajanja wa mujini wa zamani watajazia nyama kumuelezea.
Chef Justice Rugaibura:
Binafsi simfahamu, wajanja wa mujini wa miaka ile watajazia nyama kumuelezea.
Chief Kiumbe le Big Boss:
Anafahamika vizuri, jina lake lilitajwa na kuimbwa sana na wanamuziki wa band. wajanja wa zamani wa mujini watajazia nyama kumuelezea
Papaa Amos Makalla mzee wa Mvomero:
Kwa sasa ni RC wa Dar, jina lake lilianza kuvuma kitambo sana kabla hata hajaingia kwenye siasa.
Fikiri Madinda Mukuu wa kazi: Anafahamika vizuri, wajanja wa zamani wa mujini watajazia nyama kumuelezea
Pedeshee Abdul Mkeketa:
Huyu wakati fulani aliwahi kuwa mbunge ktk Mkoa wa Morogoro, sikumbuki ni jimbo gani. kwa sasa ni marehemu.
Charles Mutawali Muzee ya Magari.
Binafsi simfahamu, wajanja wa zamani wa mujini watajazia nyama kumuelezea.
Saidi Mukuu wa lumumba:
Jamaa alikuwa dalali wa kuuza magari pande za Lumumba.
Meddy Kitendawili....?
Ben Mulokozi....?
Salim Chicago Matelefone...?
Kizaizai....?
Omary Tolu...?
Abduli Tolu...?
Joshua Limited...?
Muddy Nyamalonda mzee wa Pamba Kali...?
China wa China...?
Shaibu Mapajero....?
Moris Mariaga Rais wa Sinza...?
Ntenze wa Ntenze....?
John Nzenze....?
Note of Appreciation.
sikujua kama huu uzi ungewavutia watu wengi kiasi hiki. niwashukuru wote mnaoufatilia na mnaochangia maoni yenu. asanteni sana wadau.[emoji1431][emoji1431][emoji1431][emoji1431]
Said alikua na kesi ya mauaji sema ameshatoka