Tuwafahamu Watu Maarufu waliokuwa wanatajwa sana na Wanamuziki wa Band nchini Tanzania

Mkuu wangu,sijasikia kabisa story za Liyumba na mtoto wake Mose pale Magomeni plus mwanae aliyeshikwa na poda kule Lindi yule Linda
Jamaa si ndio alikuwa BOT? Anatoa zawadi za magari mekundu? Shigongo amepiga sana hela kwa kuandika habari zake kwenye magazeti yake kipindi kile hakuna smartphone [emoji23]
 
Watu wabishi tu, ni kweli huyu mama alikuwa mrembo haswa na utajiri wa kutosha. Watu hawataki kuamini kuwa Kazaa na Pepe kale ni wale wa mbali na Mkoa.
 
Kuwapiga Waisrael wapenda dili napo ilikuwa thubutu kubwa. Kuna Waziri wa zamani Kenya anaitwa Nicholaus Biwott (merehemu kwa sasa), alikuwa na nguvu kubwa sana kwenye utawala wa Rais Moi na akiwa mfanyabiashara mkubwa aliwapiga Waisrael flani miaka ya mwanzoni 90, jamaa kuanzia wakati huo alikuwa hamuamini mtu yeyote mpaka anafariki, alikuwa anaweza kubadilisha hata magari matatu kwa siku. Yaani hata yeye mwenyewe hajiamini. Alijua iko siku jamaa watamrudia!!

Upigaji ni hatari sana, ni kama kujitoa mhanga. Bora mara mia upige mishe za magumashi kama connection za vibali, mihuri nk. Unaweza kupiga mahali na ikawa ndiyo safari yako ya milele, na vile pesa huwa inawasha! ukipiga unataka kila mtu akujue, hiyo kwa wengine ni kama dharau. Nairobi sasa hivi kuna kama trend, wapigaji kila siku wanaokotwa.
 
msofe alivuka mstari mwekundu. ila jamaa enzi zake alikuwa na uthubutu aisee, kuwapiga mpaka waisrael!!.
 
Mkuu undugu upo..mama yake merrey na islam bharabou ni dada wa damu wa mzee said salim bhakresa....mzee ally bharabou ndio baba yao na ndio shemeji wa bhakresa ...mengine nawachia wao.
 
Silent inn haukuwa ya muhaya mmiliki alikuwa mchaga nl
 
Wakati Mustahiki Meya wa Jiji Allan Mulumba Kashama anatuchezesha Dar es salaam kibinda nkoyi ndani ya Silent in Mwenge ulikuwa darasa la ngapi?
Unamjuwa Joseph Rwegasira?
Asia Hussein (Simjui),
Wapi General La Boucha (King Dodoo). Allen Mulumba Kashama alikua mtu sana. Kwa Marapa wa Dance sijaona kama yeye bado.

Hapo usikilize Kimalumalu, Neema, etc bonge la burudani.
 
Msofe nilikuwa naonana sana na Mpambe wake mmoja akiitwa Ally Kitobo mdogo wake Ally aliitwa Nuhuh huyu ndiye tuliyekua karibu sana tukiishi wote Magomeni Makuti Akachube Road kipindi bado pakiitwa Somanga pamoja na jamaa zangu Yahya na Danny Malumbo (Mungu amrehemu Yahaya tumemzika kwao Kondoa Feb mwaka huu alipata ajali Tanga na IST akielekea Holili) kila ijumaa pale makutano ya mitaa ya Livingston &Amani kuna bibi alikuwa anaitwa Bi Jang’ombe alikuwa mpishi wa biriani tamu sana so tulikuwa tunaenda kula biriani la offer kutoka kwa Msofe ila jamaa sikuwahi kumuona.

Huyo Ally dereva wake ndiye aliyekuwa mshika pesa ilikuwa siyo ajabu kumkuta anashuka na 2Mill kwenye gari kwa ajili ya matumizi mbalimbali,hela yake unaifadi akikupa kazi aisee nilikuwa naamkia shikamoo nyiingi mwisho naondoka na 50K maisha yanaenda kuna siku alinipa 100,000/= ya kununua Big G original kwa ajili ya kulia mirungi packet sikumbuki exactly ilikuwa bei gani ila haikuzidi Tsh 12,000/= nikajiuliza ninunue ngapi nikamuuliza mdogo’ake Nuhuh akaniambia chukua moja tu change tukagawana then hakuna aliyeuliza.

Jamaa hata kama hela zao zilikuwa chafu Ila mtaa waliuchangamsha kweli kweli,Msofe kabla hajang’ang’aniwa na mamlaka alikuwa na BMW X3 metallic gold kali sana haizimwi muda wote ipo on.
 
kuanza leo leo, huu uzi unakupa heshima kwa kupewa title mpya "Wewe ni Mwana dareslaam nyota 5, born town.

umefunguka vizuri sana.umetaja mpaka mitaa[emoji91][emoji91][emoji91][emoji91]
 
Kuna Said Janguo mzee....Saidi Janguo Muzee ya Texas😀
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…