Tuwafahamu Watu Maarufu waliokuwa wanatajwa sana na Wanamuziki wa Band nchini Tanzania

Tuwafahamu Watu Maarufu waliokuwa wanatajwa sana na Wanamuziki wa Band nchini Tanzania

1.Fikiri Madinda
2.Pedeshee Mudi Nondo
3.Moris Mariaga
Hapa pedeshee kidogo ni #3,hao 1&2 walikua ni janja janja tu,tuliowahi kuishi nao Sinza_Madukani tunawajua vizuri
Huyo Mudi Nondo BSS aliyoshinda Jumanne Iddi,nafikiri ilikua ndio BSS ya kwanza,siku ya Fainali aligawa pesa hatari,cha kushangaza nyumba aliyopanga ilikatiwa umeme kwa kushinda kulipa bili kwa wakati(enzi hizo hakuna LUKU) [emoji38][emoji38][emoji38]
Fikiri Madinda aliishi kwenye upangaji na nyumba ya kawaida mno tofauti na jina alilokuwa nalo mjini.
[emoji23][emoji23][emoji23]Fikiri madinda kanichekesha sana
 
Kuna pedeshee mmoja alimtwanga mtu risasi mitaa ya Magomeni usalama kwa anaekumbuka alikua ni pedeshee yupi?
 
umenikumbusha late 90s nimemaliza O-Level, nipo home idol nasubiri majibu yatoke. mshua akanitafutia temporary job mitaa ya mjini posta kwenye ofisi ya rafiki yake.

ofisi ilikuwa mtaa wa jamhuri jirani na ile round about ambayo inakutanisha india street na mkwepu street, almaarufu mitaa ya azam take away.

ilikuwa kila ikifika mida ya saa tatu mpaka saa nne asubuhi, lile eneo walikuwa wanatokea mabroo smart kwelikweli kimuonekano. mkononi wamebeba vi-diary.

walikuwa wanavaa mashati nadhifu, surauli za kadeti na viatu safi vya ngozi. kwa ujumla walikuwa wanapendeza sana, mimi mwenyewe nilikuwa nawa admire.

siku moja nikamuuliza broo mmoja ambaye tulikuwa tunafanya kazi pale, kwamba hawa jamaa ni akina nani,mbona mda mwingi wanautumia kakaa kwenye vijiwe vya shoe shiners, hawana kazi ya kufanya?.

akanijibu ukisikia mission town ndio hao, na hapo kwenye vijiwe vya shoeshiners ndio sehemu zao za kupanga mipango na kupeana deals mbalimbali.

akaniambia kile kipande chote cha mtaa wa mkwepu kinachokatiza club ya billicanas mpaka kule kwenye maungio ya samora avenue, ni territory ya ma-mission town.

hata papaa msofe alianza kujifunzia upigaji mitaa hiyo.
Nshawah kumilik kiofis mitaa hio ikawa nikiwapa adress ya ofis clients wangu wanajua mimi ninja sometimes wananilitea michongo yao tata niwasaidie nikawa nashangaa inamaana ninamuonekano wa kininja? Ndio baadae nikaja kujua niko kwa empire ya maninja na mengine yashakua majamaa yangu since then huniambii kitu kuhusu huu mji
 
mziki wa dansi ulikuwa na mambo matatu

kwanza kulikuwa na mapedeshee hawa watuzaji
ndio hao aliowataja mtoa mada

halafu kulikuwa na mashabiki damu
kama hapo unemtaja
MAMA MINGOI CHESCO MAZEE WA MATUNDA kuna pia Kina MANKA MUSHI
ambao ndo waliikuwa navijiwe vyao au CAMP zao
karanga camp
HOME ALONE
VINGUNGUTI TIMBERLAND
DALADALA CAMP
SWAZI INTER
n CAMP nyingine nyingi sana
ambazo hizo CAMP zina mashabiki haswa na mapedeshee wajanjawajanja ndo zilikiwa maskani zao na watoto wa mjini na wakati mwingine hata wanamuziki wenyewe pia huweka vijiwe katika hizo CAMP
hizo CAMP kulikuwa na mashabiki WAZARENDO
nakumbuka kuna SHABIKI MMOJA wa VINGUNGUTI TIMBERLAND huyo Mdau alikuwa anaipenda sana TWANGA kiasi alikuwa mpk anapanda NDEGE kuifuata TWANGA ikiwa NJE ya MKOA haswa ARUSHA au MWANZA

halafu kundi Jingine sasa ni la wanaofanikisha BENDI kuwa na Mziki bora

mfano HUSSEIN MIUNDOMBINU
huyu alikuwa fundi mitambo(umeme)
Twanga popote itakapopiga huyu alikuwa anahakikisha mambo yote ya umeme yako sawa mziki unatoka vizuri

THABITI MTOTO ILALA huyu alikuwa mkali wa kucheza na Keyboad

lakini pia kulikuwa na mkali mwingine wa KEYBOAD
ukisikia PROFESHENARI TARIBONARI VIctor mkambi huyu mkali wa KEYBOAD hata kama akifa inapaswa TWANGA wamjengee Sanamu lake maana alikuwa PROFESHENO haswa kaipaisha sana twanaga na UFUNDI wake wa KEYBOAD


Ukisikia MCD basi hapo anatajwa SUDI MOHAMED TIMBO(marehemu)
huyu alikuwa mpiga tumba matata sana

halafu ukisikia SHAKASHAKA SHAKUZURU hapa alikuwa anapaishwa MIRAJI SHAKASHIA huyu ni mpiga gitaa matata sana

halafu kulikuwa kulikuwa na mkung'uta DRUM hatari sana BABA DIANA BABAA SHARIFA BABAA ZAITUNI basi alikuuwa anatwaja ABUU SEMHANDO mpiga DRUM hatari

sasa utakuj kugundua kulikuwa na makundi matatu yalikuwa yanatwaja sana kwenye nyimbo
wngine walikuwa mashabiki damu wengine ndi hao watu wa wanamuziki wenyewe
Umemsahau Andrew Sekedia
 
sijui kwanini huwa napenda sana stori za kitambo.za wajanja wa zamani na vituko vyao.
majamaa zamani walifaidi sana maisha.
Wakati huo mambo yalikuwa ni moto, pale Salender club pink coconut kuanzia ijumaa ni bolingo la kufa mtu, huku Radio one unakuta DJ Rankim Ramadhani Nyamka yuko hewani anaachia Bolingo za hatari.

Ukiwa na peugeot 504 umeifunga mziki mkubwa dunia yote ilikuwa ni yako na tiketi ya kuingia hadi kwa watoto wa kishuwa unawakula tu.

Ukumbuke kipindi hicho ukitaka kwenda Uingereza ni kama unaenda Kenya tu, unakata ticket unaruka tu unaenda kugongewa entry Heathrow London.
 
ila diamond amefanya mambo ya kutajana majina(shout out)kwenye nyimbo kuwa jambo rahisi sana. imagine siku hizi hata akina juma lokole majina yao yanasikika kutajwa kwenye nyimbo za bongofleva.

miaka ile haikuwa jambo rahisi, ilitakiwa lazima uwe financially stable ili uweze ku facilitate mahitaji muhimu ya wanamuziki.

mathalani,kuwalipia pesa studio wakati wa kurecord album, kuwalipia kodi pale wanapokwama, kuwajazia mafuta kwenye gari zao, kuwapa pesa ya matumizi yao binafsi, kutumia connection zako kurescue situation pale mwanamziki anapokuwa ameingia ktk matatizo na vyombo vya dola nk. hayo ndio maeneo mapeshee walikuwa wanachukua point tatu.

nje ya hapo, ili jina lako liwe linatajwa sana, ilitakiwa uwe shabiki kindakindaki(loyal fan)wa
mziki wa dansi na usiwe unakosa kwenye show za band kila zinapotumbuiza.
 
Nasikiliza Maria nyimbo ya Fali Ipupa sasa hivi mwisho naskia anamtaja Erick Mandala.
uyu Erick Mandala ni mwanasia,mfanya biashara ama nani kule Congo?
Hao Wanamuziki wa Congo wote break yao kuna Don wa Ki Ivory coast anaishi Paris anaitwa Hemed Bakayoko, huyu ndio funga kazi, hii treasure.

Huyu ndio hakauki mdomoni mwa Boss ya Mboka Koffi Ollomide then ndio anakula shavu Samuel Etoo, hizi ni international level.
 
Hao Wanamuziki wa Congo wote break yao kuna Don wa Ki Ivory coast anaishi Paris anaitwa Hemed Bakayoko, huyu ndio funga kazi, hii treasure.

Huyu ndio hakauki mdomoni mwa Boss ya Mboka Koffi Ollomide then ndio anakula shavu Samuel Etoo, hizi ni international level.
Kweli huyu bakayoko kwnye twanga fotoo nimesikia jina lake
 
Nshawah kumilik kiofis mitaa hio ikawa nikiwapa adress ya ofis clients wangu wanajua mimi ninja sometimes wananilitea michongo yao tata niwasaidie nikawa nashangaa inamaana ninamuonekano wa kininja? Ndio baadae nikaja kujua niko kwa empire ya maninja na mengine yashakua majamaa yangu since then huniambii kitu kuhusu huu mji
kuna siku nilishuhudia tukio la kusikitisha na kuchekesha pia.

tukio lenyewe lilitokea mtaa wa india street mkabala na jengo la haidary plaza jirani na bureau change moja maarufu wakati huo.

mission town walikuwa wamempiga mkenya vidollar vyake. walimuwahi nje akiwa anaelekea kuingia ndani ya ile bureau ku exchange dollar zake.

wakamwambia ndani ya bureau atapata pesa kidogo, ila wao watamfanyia exchange rate na atapata pesa nyingi za ktz.

mkenya akakubali. masikini hakujua kama zile fedha za ktz alizopewa na wale mission town zilikuwa fake.

baadae akarudi pale hakukuta mtu, akabaki anatukana tu hovyo hovyo. kajaa hasira huku jasho likimtoka, kalowa chapachapa.

watu wanamtazama tu, wengine wanamcheka.
 
kuna siku nilishuhudia tukio la kusikitisha na kuchekesha pia.

tukio lenyewe lilitokea mtaa wa india street mkabala na jengo la haidary plaza jirani na bureau change moja maarufu wakati huo.

mission town walikuwa wamempiga mkenya vidollar vyake. walimuwahi nje akiwa anaelekea kuingia ndani ya ile bureau ku exchange dollar zake.

wakamwambia ndani ya bureau atapata pesa kidogo, ila wao watamfanyia exchange rate na atapata pesa nyingi za ktz.

mkenya akakubali. masikini hakujua kama zile fedha za ktz alizopewa na wale mission town zilikuwa fake.

baadae akarudi pale hakukuta mtu, akabaki anatukana tu hovyo hovyo, jasho la hasira linamtoka kalowa chapachapa.

watu wanamtazama tu.
Huo ni uzembe wa mtu binafsi, angalau enzi za Nyerere na Mwinyi pale Empress Cinema wazungu walipigwa sana kwenye kuchange Dollar maana zamani maduka ya kubadili pesa za kigeni yalikuwa yamebaniwa.

Mimi mwaka 1996 mara yangu ya kwanza kufika Jiji la Johannesburg nilikutana na changamoto hiyo hakukuwa na Bereau de change nilielekezwa dukani kwa muhindi Carton Center karibu na holiday inn hotel nikachenjiwa hapo, dollar moja kwa Rand 4.

Kuna vitu hata kama siyo rasmi ni lazima uangalie unafanya katika mazingira gani.
 
Hao Wanamuziki wa Congo wote break yao kuna Don wa Ki Ivory coast anaishi Paris anaitwa Hemed Bakayoko, huyu ndio funga kazi, hii treasure.

Huyu ndio hakauki mdomoni mwa Boss ya Mboka Koffi Ollomide then ndio anakula shavu Samuel Etoo, hizi ni international level.
hamed bakayoko is no more, alifariki last year kwa Covid . koffi olomide aliomboleza sana msiba wake. yeye na koffi walikuwa ni marafiki wa karibu sana.

bakayoko alikuwa ni raia wa ivory coast. a politician, rich businessman, music promoter, influencer and prominent figure in francophone countries.

nilikuwa nafatilia sana habari zake wakati angali hai.


IMG_20220627_002743.jpg
 
Jasmine alikuwa full package mguu mjazo. Ule mguu lazma hakuwa mchaga!
Lakin ile show aliyekuwa hot girl ni Mboni! Hata fally alicheza nae kwa hisia na adabu za matamanio na kale ka suti ka kung'aa bei mbaya kitovu nje km halagi chips!
Mboni popote ulipo pole. huwez kurudsha nyuma saa!
Nadhan watu maarufu wanaotoaga vitabu vya maisha yao, mboni atatusimuliaga walifanya nini na Fally thereafter!
Mkuu Mboni alitisha nashindwa kuamini kama ndio huyu Mboni wa sasa kwenye runinga au yule wa fally Ipupa ni Mboni mwingine, sidhani kama siku ile alienda kulala kwao au kwake..
 
Back
Top Bottom