Tuwafahamu Watu Maarufu waliokuwa wanatajwa sana na Wanamuziki wa Band nchini Tanzania

Tuwafahamu Watu Maarufu waliokuwa wanatajwa sana na Wanamuziki wa Band nchini Tanzania

Kuna mdau alimuulizia Hemedi Bakayoko ambae alikua tajiri mkubwa Ivorycoast akimiliki viwanda na alikua waziri mkuu wa nchi yake, Na Omary Bongo ni Rais wa Gabon na Baba yake alikua Rais pia walianza bata kitambo na wacongoman waliitwa sana kwenye nchi zao na kulipwa pesa nyingi, lakini bakayoka alikua na Ukumbi paris ambapo akina koffi na wanamuziki wengine wengi wamepiga pale sana hivo anaheshima ya kipekee sana kwenye burudani hasa upande wa wazungumzaji wa kifaransa
Omary Bongo Ondimba =baba.Ally Benny Bongo=mtoto
 
Hatari sana, sasa hivi hawana kitu hao wote...

Tumebakia sisi tu...
 
mziki wa dansi ulikuwa na mambo matatu

kwanza kulikuwa na mapedeshee hawa watuzaji
ndio hao aliowataja mtoa mada

halafu kulikuwa na mashabiki damu
kama hapo unemtaja
MAMA MINGOI CHESCO MAZEE WA MATUNDA kuna pia Kina MANKA MUSHI
ambao ndo waliikuwa navijiwe vyao au CAMP zao
karanga camp
HOME ALONE
VINGUNGUTI TIMBERLAND
DALADALA CAMP
SWAZI INTER
n CAMP nyingine nyingi sana
ambazo hizo CAMP zina mashabiki haswa na mapedeshee wajanjawajanja ndo zilikiwa maskani zao na watoto wa mjini na wakati mwingine hata wanamuziki wenyewe pia huweka vijiwe katika hizo CAMP
hizo CAMP kulikuwa na mashabiki WAZARENDO
nakumbuka kuna SHABIKI MMOJA wa VINGUNGUTI TIMBERLAND huyo Mdau alikuwa anaipenda sana TWANGA kiasi alikuwa mpk anapanda NDEGE kuifuata TWANGA ikiwa NJE ya MKOA haswa ARUSHA au MWANZA

halafu kundi Jingine sasa ni la wanaofanikisha BENDI kuwa na Mziki bora

mfano HUSSEIN MIUNDOMBINU
huyu alikuwa fundi mitambo(umeme)
Twanga popote itakapopiga huyu alikuwa anahakikisha mambo yote ya umeme yako sawa mziki unatoka vizuri

THABITI MTOTO ILALA huyu alikuwa mkali wa kucheza na Keyboad

lakini pia kulikuwa na mkali mwingine wa KEYBOAD
ukisikia PROFESHENARI TARIBONARI VIctor mkambi huyu mkali wa KEYBOAD hata kama akifa inapaswa TWANGA wamjengee Sanamu lake maana alikuwa PROFESHENO haswa kaipaisha sana twanaga na UFUNDI wake wa KEYBOAD


Ukisikia MCD basi hapo anatajwa SUDI MOHAMED TIMBO(marehemu)
huyu alikuwa mpiga tumba matata sana

halafu ukisikia SHAKASHAKA SHAKUZURU hapa alikuwa anapaishwa MIRAJI SHAKASHIA huyu ni mpiga gitaa matata sana

halafu kulikuwa kulikuwa na mkung'uta DRUM hatari sana BABA DIANA BABAA SHARIFA BABAA ZAITUNI basi alikuuwa anatwaja ABUU SEMHANDO mpiga DRUM hatari

sasa utakuj kugundua kulikuwa na makundi matatu yalikuwa yanatwaja sana kwenye nyimbo ndio hao mapedeshee
wngine walikuwa mashabiki damu wa dansi
wengine ndio hao wenyewe wa wanamuziki
Umenikumbusha mbali sana,huyo profesheneri keyboard mwanaSumbawanga,duuh! sijui ni mtu wa huko,na huyo MCD chapa ngoma halafu kanasikika kasauti kangoma,daaah! aisee,kitambo sana.
 
mwenye asili ya kihayudi ni moise katumbi, mmiliki wa team ya mpira TP mazembe.

ila huyu bwana mdogo abed achour ni mwarabu mwenye asili ya Lebanon.

familia yake ilihamia congo miaka 50 iliyopita. yeye mwenyewe amezaliwa drc katikati au mwishoni mwa miama ya 80.

ndani ya congo, familia yake imewekeza ktk sector mbalimbali ikiwemo transportation, manufacturing na hospitality.

hapo kwenye hospitality wanamiliki hotel kubwa sana kinshasa. kiufupi dogo ni Don kwelikweli.

akina fally, ferre, innoss'B, heritier wakikutana na huyo dogo, wanahisi ni kama vile wamekutana na na tajiri namba moja duniani billionaire Elon Musk.
nimekusima vema mkuu
 
Umenikumbusha meddy kitendawili kwenye nyimbo ya jirani ya twanga pepeta
 
nani anamkumbuka pedeshee ali aurora?. maisha ya huyu jamaa yalitawaliwa na visa vingi vya utapeli na dhuruma.

halafu akaja kufariki kwa maradhi yaliyomtesa sana. inadaiwa aliowadhurumu walimpiga "msumali".
Aurora muzee ya Tanga
 
Hao Wanamuziki wa Congo wote break yao kuna Don wa Ki Ivory coast anaishi Paris anaitwa Hemed Bakayoko, huyu ndio funga kazi, hii treasure.

Huyu ndio hakauki mdomoni mwa Boss ya Mboka Koffi Ollomide then ndio anakula shavu Samuel Etoo, hizi ni international level.
Hemed Bakayokoo Le boss hatari sana huyu mtu.
 
Itakusaidia nini?
Huu Uzi utasaidia sana kutoa elimu kwa Rika mbali mbali kuhusu matumizi sahihi ya pesa. Tukiangalia huko nyuma Kuna watu walikuwa na hela Leo hata Mia hawana, na tunaweza pia pata mbinu za namna gani ya kupata pesa kupitia hao mapedeshee kwa shughuli walizokuwa wakifanya, pia kupata changel na maujanja ya mujini. Kwa mtazamo wangu huu Uzi no Kama SoMo tu la histora shuleni, Ila hapa umebezi na historian ya mapedeshee
 
Maisha Kitendawili, Dr Rama, Abdala Nyumba nyingi, Bitebo saloon, Songolo, Haji mbabe mwanamanyema, somebody Miundombinu, utajiju Camp, Daladala camp, Andrew Trader, Side Mkuluma,Freedom Camp, Salumu na Merelani, Home alone camp, Salum masim, Chikago matelephone nk
Hassan miundombinu kaa sikosei
 
Back
Top Bottom