Tuwafahamu Watu Maarufu waliokuwa wanatajwa sana na Wanamuziki wa Band nchini Tanzania

Tuwafahamu Watu Maarufu waliokuwa wanatajwa sana na Wanamuziki wa Band nchini Tanzania

duh..umenirudisha mbali sana mzee. nitaandika machache ninayoyakumbuka kuhusu huyo jamaa.

well, merey balhabou alikuwa ni mmiliki wa timu ya mpira ya moro united ya morogoro.

pia alikuwa ni mjasiriamali mkubwa tajiri aliyewekeza ktk sector ya nishati. ana undugu wa damu na tajiri namba moja nchini, salim bakhresa, nahisi anamuita mzee bakhresa mjomba(sina uhakika).

huyu jamaa ni mfaidika mkubwa yale mabilioni ya aliyewahi kuwa rais wa libya muamar ghadaf aliyokuwa anayatuma hapa tz ili kuwekeza ktk miradi mbalimbali.

yeye na wenzie waliokuwa kwenye system wakati huo ndio walikuwa wanayapiga yale mabilioni.

alifilisika baada ya kuwa na madeni mengi aliyoshindwa kulipa. pale tabata tioti zilizopo ofisi za azamtv, ilikuwa ni yard yake ya malori. alimuuzia mjomba wake mzee bakhresa ili kupata fedha ya kulipa madeni aliyokuwa anadaiwa.

kwa sasa sidhani kama yupo nchini, nahisi anaishi dubai au south africa.

hayo mengine sijui ya kulawiti wananume wenzie mimi siyajui, nilikuwa nayasikia tu. nawaachia wajuzi wa mambo watiririke.
Shabiby akiwa miongoni mwa wakurugenzi na mfaidika mkubwa kwenye hiyo kampuni.
 
John Cheyo ni wa masaki Dar, nyumbani kwake si mbali sana na ubalozi wa South Africa au sea cliff apartments, huko Bariadi makolo wake alikuwa akiwatumia tu kupata ubunge, hadi Magu wameshawahi kumpa Ubunge, ana mdogo wake anaitwa Isaack Cheyo pia alikuwa anapewa ubunge wa Bariadi Magharibi naye ni mtu wa Dar maskani yake Kinyerezi tulikuwa tuna kijiwe chetu enzi hizo tunapiga lager za kutosha.
Mzee mapesa nilishakutana nae Maisha club Dom akiwa amevaa heleni sikioni na pisi mbili kashikilia huku na huku.

Last time nimemuona kwny msiba wa mtoto wa Mabeyo akiwa kwny Ile Hummer yake lkn afya naona haijakaa poa sana.
 
umenikumbusha late 90s nimemaliza O-Level, nipo home idol nasubiri majibu yatoke. mshua akanitafutia temporary job mitaa ya mjini posta kwenye ofisi ya rafiki yake.

ofisi ilikuwa mtaa wa jamhuri jirani na ile round about ambayo inakutanisha india street na mkwepu street, almaarufu mitaa ya azam take away.

ilikuwa kila ikifika mida ya saa tatu mpaka saa nne asubuhi, lile eneo walikuwa wanatokea mabroo smart kwelikweli kimuonekano. mkononi wamebeba vi-diary.

walikuwa wanavaa mashati nadhifu, surauli za kadeti na viatu safi vya ngozi. kwa ujumla walikuwa wanapendeza sana, mimi mwenyewe nilikuwa nawa admire.

siku moja nikamuuliza broo mmoja ambaye tulikuwa tunafanya kazi pale, kwamba hawa jamaa ni akina nani,mbona mda mwingi wanautumia kakaa kwenye vijiwe vya shoe shiners, hawana kazi ya kufanya?.

akanijibu ukisikia mission town ndio hao, na hapo kwenye vijiwe vya shoeshiners ndio sehemu zao za kupanga mipango na kupeana deals mbalimbali.

akaniambia kile kipande chote cha mtaa wa mkwepu kinachokatiza club ya billicanas mpaka kule kwenye maungio ya samora avenue, ni territory ya ma-mission town.

hata papaa msofe alianza kujifunzia upigaji mitaa hiyo.
Mitaa hiyo hatari mpka Nkurumah, enzi hizo nikitumwa nyaraka flani naenda mitaa hiyo kuna Watu wananifahamu. Kuna rafiki yangu wa zamani yeye dili zake ilikuwa kuwa mdhamini kwa raia wa kigeni waliokuwa wanapewa dhamana na mahakama. Anajua ishu za kisheria utafikiri mwanasheria na ni darasa la saba tu.

Kulikuwa na kijiwe kingine hapo extelecom, kulikuwa na vibanda vya stationery, humo ni dili za TRA tu.
 
Ustadhi Juma Namusoma, huyu Hadi alikuwa meneja wa wasanii, Kuna mama Sakina Trans alimiliki bendi ya mashujaa na midaladala mingi hapa Ukraine town pia yupo jamaa anaitwa Respect Chief Kiumbe, huyu ata huko Kanda ya ziwa wanamfahamu vizuri
Huyo Ustaadhi Juma Namusoma mara ya mwisho nilimuona Dubai ila sikuwa na time na Wabongo.
 
Hyu ndy alikuwa nguzo kubwa tanga
Rip baba Diana

Ova
Yeye ndio alikuwa katibu wa bendi.

Ila uzi bila kumtaja dada yetu Asha Baraka basi uzi utakuwa una mapungufu makubwa.

Asha Baraka Sugu, huyu ndio alimpeleka marehemu Kanumba Uingereza kwa mara ya kwanza Kanumba akiwa mpole kabisa, mwana mmoja wa Kinondoni wakuitwa Mtambo yupo USA kwa sasa ndio ananitambulisha kwa Kanumba.

Tulikutana kwenye viofisi vyetu vya mazabe wote tunajaza fomu za kuingia ubalozini na kupiga passport size quality.
 
Yupo mlevi tu analewa sana Juliana pub na bar nyingine za Mbezi kule Target, Amsterdam, Jangwani Sea breeze etc..
Yule Dada pisi kali mwenye Amsterdam yupo? Au yupo mbele na mzungu wake?
 
chacho ombala
anaitwa tchatcho mbala kashogi.
ni mfanyabiashara tajiri wa congo aliyejikita katika biashara ya vito vya dhahabu na almas.

anamiliki maduka makubwa ya kuuza vito jijini kinshasa, luanda angola, paris ufaransa na brussels ubeligiji.

kwa mda mrefu amekuwa ni rafiki wa wanamuziki na mfadhili wa project zao mbalimbali. ndio maana jina lake linatajwa sana na wanamuziki hao.

jina lake limesikika kwenye nyimbo za madilu system, werrason, jb mpiana,koffi olomide, fally ipupa and the likes.

vyanzo vinadai utajiri wake ulikuja baada ya kujenga urafiki wa ukaribu na kiongozi wa UNITA marehemu jonas savimbi.

naam, kwa ufupi huyo ndio le bilionea, le patro, tajiri papaa tchatcho mbala mutu ya pakee.[emoji16]
IMG_20220627_161453.jpg
IMG_20220627_161523.jpg
IMG_20220627_161424.jpg
 
anaitwa tchatcho mbala kashogi.
ni mfanyabiashara tajiri wa congo aliyejikita katika biashara ya vito vya dhahabu na almas.

anamiliki maduka yake makubwa ya kuuza vito jijini kinshasa, luanda angola, paris ufaransa na brussels ubeligiji.

kwa mda mrefu amekuwa ni rafiki wa wanamuziki na mfadhili wa project zao mbalimbali. ndio maana jina lake linatajwa sana na wanamuziki hao.

limesikika likitajwa kwenye nyimbo tchatcho mbala na urafiki wake wa karibu na kiongozi wa UNITA marehemu jonas savimbi.

naam, huyo ndio tchatcho mbala kwa ufupi.

View attachment 2274394View attachment 2274395View attachment 2274396
Huyu ndiyo pedeshe sasa

Ova
 
Yeye ndio alikuwa katibu wa bendi.

Ila uzi bila kumtaja dada yetu Asha Baraka basi uzi utakuwa una mapungufu makubwa.

Asha Baraka Sugu, huyu ndio alimpeleka marehemu Kanumba Uingereza kwa mara ya kwanza Kanumba akiwa mpole kabisa, mwana mmoja wa Kinondoni wakuitwa Mtambo yupo USA kwa sasa ndio ananitambulisha kwa Kanumba.

Tulikutana kwenye viofisi vyetu vya mazabe wote tunajaza fomu za kuingia ubalozini na kupiga passport size quality.
Asha kweli alipambana sana kuhusu twanga,wakati wa show kuna wakati alikuwa anakomaa mlangoni,vingilio
Mimi mwenyewe twanga nlikuwa mdau kwelikweli
Bendi ina raha yake bana

Ova
 
Kuna Mzee mmoja mmasai alikua chuga,pesa alikua nayo yakutosha sana,alikua ana miliki timu ya mpira wa miguu ya Parison ya Arusha,Mzee alikua anapanda juu ya ghorofa anaanza kugawa pesa! Sasa hivi sijui yuko wapi,pesa ilikata!

Mwanza kulikua na Pedeshee Mteka teka, Mhasibu wa Polisi Mwanza,jamaa alikua anakula wanawake balaa
Alijulikana almaarufu kwa jina la askofu,jina lake lilikua Ni Thomas Mollel na Alifariki akiwa Dom alipoenda kwny kuapishwa kwa mbunge wa Meru Mashariki mwaka 2019.
 
hahahahaha.....dunia ili iwe dunia lazima iwe na watu wa namna hii......kizazi hiki kinawauza nyago wengi sana, wengi sio watu wa pilikapilika.....

Naona mnamkanyagia swahiba wangu Kizaizai.....

Mmemsahau big bosi, Mzee wa SA, Alex.
Madenge sijamuona humu, wengine sio mapapa ila wazee wa mipango mjini at low key, wakiwa behind....
 
Dah enzi zike za Twanga na Msondo Jmosi jukwaa moja leaders, usiku tunahamia Mango....

Hivi Dallaz Dala yuko wapi siku hizi, dah enzi zile Wolper bado wamoto mjini hahaha...
 
Yeye ndio alikuwa katibu wa bendi.

Ila uzi bila kumtaja dada yetu Asha Baraka basi uzi utakuwa una mapungufu makubwa.

Asha Baraka Sugu, huyu ndio alimpeleka marehemu Kanumba Uingereza kwa mara ya kwanza Kanumba akiwa mpole kabisa, mwana mmoja wa Kinondoni wakuitwa Mtambo yupo USA kwa sasa ndio ananitambulisha kwa Kanumba.

Tulikutana kwenye viofisi vyetu vya mazabe wote tunajaza fomu za kuingia ubalozini na kupiga passport size quality.
sahihi kabisa Asha Baraka ni mwanamke wa shoka bila kumsahau aliyekua mumewe pedeshee Hamis Bwela.
kwakweli siku hazigandi ndugu zangu.
 
anaitwa tchatcho mbala kashogi.
ni mfanyabiashara tajiri wa congo aliyejikita katika biashara ya vito vya dhahabu na almas.

anamiliki maduka makubwa ya kuuza vito jijini kinshasa, luanda angola, paris ufaransa na brussels ubeligiji.

kwa mda mrefu amekuwa ni rafiki wa wanamuziki na mfadhili wa project zao mbalimbali. ndio maana jina lake linatajwa sana na wanamuziki hao.

limesikika likitajwa kwenye nyimbo za madilu system, werrason, jb mpiana,koffi olomide, fally ipupa and the likes.

vyanzo vinadai utajiri wake ulikuja baada ya kujenga urafiki wa ukaribu na kiongozi wa UNITA marehemu jonas savimbi.

naam, huyo ndio tchatcho mbala kwa ufupi.
View attachment 2274394View attachment 2274395View attachment 2274396
huyu pedeshee ni waukweli kitambo sana.
nilianza kumsikia kwenye nyimbo za Kofii miaka ya tisini huko,Nyimbo kama Mico,,Kofi alikua akiimba anaanza na jina la Chaaaachoooo.
 
hahahahaha.....dunia ili iwe dunia lazima iwe na watu wa namna hii......kizazi hiki kinawauza nyago wengi sana, wengi sio watu wa pilikapilika.....

Naona mnamkanyagia swahiba wangu Kizaizai.....

Mmemsahau big bosi, Mzee wa SA, Alex.
Madenge sijamuona humu, wengine sio mapapa ila wazee wa mipango mjini at low key, wakiwa behind....

mrangi kamsagia sana kunguni kizaizai [emoji1787][emoji1787]

huyo madenge unayemzungumzia wewe ni yupi, ni yule jamaa mfupi mwenye kichwa kikubwa?,mjanja mjanja anaongea sana.

dress code yake anapenda kuvaa kaunda suti, cheni kubwa shingoni na mapete vidoleni. halafu ally choki alikuwa anamtaja sana kwa kibwagizo cha "papaa madenge".

kuna wakati nilikuwa nakutananae mitaa ya temeke wailes na mitaa ya mkwepu street, posta mpya.
 
Back
Top Bottom