Umenikumbusha late 90s nimemaliza O-Level, nipo home idol nasubiri majibu yatoke. mshua akanitafutia temporary job mitaa ya mjini posta kwenye ofisi ya rafiki yake.
Ofisi ilikuwa mtaa wa jamhuri jirani na ile round about ambayo inakutanisha india street na mkwepu street, almaarufu mitaa ya azam take away.
Ilikuwa kila ikifika mida ya saa tatu mpaka saa nne asubuhi, lile eneo walikuwa wanatokea mabroo smart kwelikweli kimuonekano. mkononi wamebeba vi-diary.
Walikuwa wanavaa mashati nadhifu, surauli za kadeti na viatu safi vya ngozi. kwa ujumla walikuwa wanapendeza sana, mimi mwenyewe nilikuwa nawa admire.
Siku moja nikamuuliza broo mmoja ambaye tulikuwa tunafanya kazi pale, kwamba hawa jamaa ni akina nani,mbona mda mwingi wanautumia kakaa kwenye vijiwe vya shoe shiners, hawana kazi ya kufanya?.
Akanijibu ukisikia mission town ndio hao, na hapo kwenye vijiwe vya shoeshiners ndio sehemu zao za kupanga mipango na kupeana deals mbalimbali.
Akaniambia kile kipande chote cha mtaa wa mkwepu kinachokatiza club ya billicanas mpaka kule kwenye maungio ya samora avenue, ni territory ya ma-mission town.
Hata papaa msofe alianza kujifunzia upigaji mitaa hiyo.