Tuwafahamu Watu Maarufu waliokuwa wanatajwa sana na Wanamuziki wa Band nchini Tanzania

Tuwafahamu Watu Maarufu waliokuwa wanatajwa sana na Wanamuziki wa Band nchini Tanzania

Zamani nliuza sana sim za mkononi mitaa ya azam na salamander
Na sim nliwauzia sana mashuwa
Mabosi wa bandari,tra,mapolisi yaani vurugu mechi
Nlitengeneza sana faida kwenye sim
Mitaa ya azam kulikuwqga na fundi sim maarufu sana anaitwa yahaya hata solo thang alimuimba kwenye ngoma yake ya sim yangu,nkiwa na sm kimeo tunampelekea yahaya

I Ikajaga michongo ya international call kupiga mizazabe ttcl [emoji1]
Vijana wengi walingia
We kazi yako kuwaunganisha watu tu wanaongea nakumbka wateja wengi walikuwa wadosi tena wale heavyweight,we ukimaliza unapitia mpunga wako tu makwao

Sasa wakat wao wanaongea we maongezi yao unasikia yaani wanongea dili mwanzo mwisho
Hiyo ilinifanya nkajuana na wadau wengi,nakumbka nlipataga msala
Tuko kitega uchumi juu tukaisha
Kesi uhujumu uchumi lkn tulimaliza
Na sikutaka tena masuala hayo

Sasa sahv teknolojia imerahisisha mambo zamani kupiga sim nje mtihani

Ova
Umenikumbusha mbali, mbali, Mandela baada ya kupata Urais ilikuwa Telkom ukiomba huduma ya simu ndani ya wiki moja unaunganishiwa.

Kulikuwa na jamaa yupo Kuwait Wahindi wanapanga foleni kuanzia asubuhi mpaka usiku non stop mnawaunganisha kuongea na familia zao India kisha yeye anawatumia pesa kupitia western union na wala hamjuwani wala hata hujui anafananaje.
 
Siku moja nilikwenda Ngwasuma Heineken house, nilikuwa na katibu wa Wacongoman Tanzania, basi tulikula senene wa kutosha na mimi siku hiyo nilikuwa PDG, yule jamaa akawapa jina langu, basi nilivyokwenda kuwatunza nikashangaa wanalitaja jina langu halafu Nyoshi anasema baada ya Mungu ni wewe, kwakweli nilichoka aisee, hawa jamaa funga kazi.
Ha ha ha ha baada ya Mungu ni wewe! Wale jamaa kweli wehu
 
Kuna mdau alimuulizia Hemedi Bakayoko ambae alikua tajiri mkubwa Ivorycoast akimiliki viwanda na alikua waziri mkuu wa nchi yake, Na Omary Bongo ni Rais wa Gabon na Baba yake alikua Rais pia walianza bata kitambo na wacongoman waliitwa sana kwenye nchi zao na kulipwa pesa nyingi, lakini bakayoka alikua na Ukumbi paris ambapo akina koffi na wanamuziki wengine wengi wamepiga pale sana hivo anaheshima ya kipekee sana kwenye burudani hasa upande wa wazungumzaji wa kifaransa
Nashukuru sana mkuu, Mimi ndiye niliyeuliza swali ingawa juu hapo kuna watu wameleta ujuaji ila nashukuru kwa majibu yako,
 
Siku moja nilikwenda Ngwasuma Heineken house, nilikuwa na katibu wa Wacongoman Tanzania, basi tulikula senene wa kutosha na mimi siku hiyo nilikuwa PDG, yule jamaa akawapa jina langu, basi nilivyokwenda kuwatunza nikashangaa wanalitaja jina langu halafu Nyoshi anasema baada ya Mungu ni wewe, kwakweli nilichoka aisee, hawa jamaa funga kazi.
Maisha yako mbio sana, Nyoshi anaimba bado kwenye bar kadhaa Dar, ni kumfika bei tu, mara ya mwisho nilimuona alikuwa na Patcho Mwamba mitaa ya Goba pale sema wanaamsha bhana sio mchezo
 
Siku moja nilikwenda Ngwasuma Heineken house, nilikuwa na katibu wa Wacongoman Tanzania, basi tulikula senene wa kutosha na mimi siku hiyo nilikuwa PDG, yule jamaa akawapa jina langu, basi nilivyokwenda kuwatunza nikashangaa wanalitaja jina langu halafu Nyoshi anasema baada ya Mungu ni wewe, kwakweli nilichoka aisee, hawa jamaa funga kazi.
haaa,,,wacongo wanapaisha mbaya mbovu.
"Papaa Matola mutu ya watu,*mutu iko na pesa mingi sana"[emoji23].
hapo umetunza teni tu unapaishwa kama mwewe[emoji23][emoji23]
 
Manka Mushi kati ya Moshi sijui picha yake wala mishe zake.
 
Huyo Baraka kapuya full boss sasa hivi yuko Urambo kaliua tabora huko kuna lodge ana simamia
Inasemwa Akudo ni kifupi Cha ATHUMANI...KULWA NA DOTTO (AKUDO)
Pamoja na kua profesa....kapuya Hana mtoto mwenye akili wala mtoto msomi....(Brainy)

Inasemekana malezi ya kuwalea watoto kama mayai zimechangia kuwaharibu

Ni wababe sana watoto wake nasikiaga baraka alikua anatembezea Rungu wake za watu hapo kaliua........

Wajuvi wataongezea....
 
Awali ya yote nitangulize angalizo kwa vijana ambao maturity stage imewakuta miaka hii ya mitandao ya kijamii. Itabidi msome kimyakimya huku mkiwa mmeshika peni na karatasi kuchukua notes.

Huu uzi ni wa sisi ma-seniors, maudhui yake yatagusa zaidi vijana wenzangu ambao maturity liwakuta kuanzia late 90s to early 2000s.

Mwaka 2002 mpaka 2012, mziki wa dansi ulikuwa upo kwenye prime time.

Kwa uchache tu, band zilizotamba ni FM Academia, Akudo Impact, Twanga Pepeta na Diamond Musica. Zingine zilikuwa zinaibuka na kupotea ndani ya muda mfupi.

Umaarufu wa hizi band ulienda sambamba na trend ya wanamuziki kutaja majina ya baadhi ya watu kwenye mashairi yao.

Majina ya hawa watu yalivuma na kuwa maarufu kuliko sura zao kwasababu miaka ile kulikuwa hakuna social platform za ku-share picha na video kama ilivyo hivi sasa.

Kutokana na kujichanganya kwangu ukijumlisha na ujanja wangu wa kimjini mjini wa miaka ile, nilifanikiwa kufahamiana na baadhi mapedeshee au wazee wa mujini ambao majina yao yalikuwa yanatajwa kwenye mziki wa dansi.

Nitataja ninaowakumbuka na wewe ongeza wa kwako.

Naandika majina yao kama yalivyokuwa yanatamkwa kwa mbwembwe na wanamuziki.

Kwa mfano kama mtu alikuwa anaitwa John, wanamuziki walikuwa wanatamka papaa John Young Millionaire Muzee ya ma-Range Rover[emoji3][emoji3].

Haya twende kazi:
Pedeshee Mychoice na kati ya Mbeya
:
huyu sijui alikuwa anapiga mishe gani huko Mbeya, watu wa Mbeya mtatusaidia.

Braza K na kati ya Tunduma:
Watu wa Tunduma mtatusaidia kutujuza kuhusu huyu jamaa, alivuma sana.

Mamaa Rukia Soloon:
Huyu bibie namfahamu, ana saloon yake ya kike mitaa ya Mikocheni barabara ya Rose Garden. Those days she was very pretty, kwa sasa utu uzima umemchukua.

Mamaa Dotnata Decoration:
Bila shaka wengi mnamkumbuka, aliwahi kuwa muigizaji maarufu kupitia ITV, baadae akaingia kwenye ujasiriamali wa kutoa huduma za catering, shughuli hizi zilimpatia mafanikio sana. sijui kwa sasa yupo wapi huyu mama. FM Academia waliwahi kumtungia wimbo wenye jina lake.

Mamaa Juddy Moshi:
Alikuwa mmiliki wa band ya Daimond Musica kwa financial support ya mshua mmoja ambaye alikuwa ni MD wa Yellow Pages, watu wa zamani wanaelewa. Juddy alikuwa mrembo si kitoto, kwa sasa umri wake umesonga mbele.

Pedeshee Akayesu Ndama Mutoto ya Ng'ombe:
Sina haja ya kumuelezea, ni mtu maarufu wa nyakati zote. Wajanja wa mujini watamuelezea zaidi. Jina lake lilitajwa sana kwenye nyimbo za dansi zilizovuma.

Young Millionaire Bill gate Muzamir Katunzi:
Christian Bella aliwahi kutunga mpaka wimbo wenye jina hilohilo la Muzamir Katunzi. I don't know him personally, but it's told he was financially successful.

Papaa Msofe Chuma cha Reli hakishiki Kutu.
Sina haja ya kuandika mengi kuhusu umaarufu wa Papaa Msofe. Itoshe tu kusema jina lake liliimbwa sana halafu ni wachache waliokuwa wanajua sura yake. Walianza kuiona kwenye media alipokuwa anahudhuria viunga vya mahakama kujibu kesi yake.

Papaa Martin Kasianju.
Ni marehemu kwa sasa, huyu mshua ndio alikuwa mmiliki wa Band ya FM Academia. Nilikuwa namfahamu personally. licha ya kwamba alikuwa ni mjasiriamali na muajirwa Serikalini, pia alikuwa ni Senior Officer wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Andrew Traders na Kariakoo Big Supply: Jamaa alikuwa ni mfanyabiashara wa kuuza tairi za gari Mtaa wa Agrey Kariakoo huku akipiga michongo yake ya "general supply". Watu wa mujini wa zamani wanaelewa vizuri maana ya kampuni kusajiliwa kwa jina la general supply. Katika biashara ya kuuza tairi, alishirikiana na kaka yake, ila yeye akawa maarufu zaidi na akaaminika na wadau.

Kinje Mutoto wa Mujini:
Najua wengi mnamfahamu na zile deal zake alizokuwa anapiga. sina haja ya kumuelezea zaidi.

Pedeshee David Kabunga:
Sifahamu alikuwa ni nani, jina lake lilikuwa linatajwa sana.

Papaa Ally Kileo:
He was a prominent lawyer in town, jina lake lilikuwa linatajwa sana kwenye nyimbo za dansi.

Papaa Mutarika Mzee wa Mambo mengi:
Binafsi simfahamu, wajanja wa mujini wa zamani watajazia nyama kumuelezea.

Chef Justice Rugaibura:
Binafsi simfahamu, wajanja wa mujini wa miaka ile watajazia nyama kumuelezea.

Chief Kiumbe le Big Boss:
Anafahamika vizuri, jina lake lilitajwa na kuimbwa sana na wanamuziki wa band. wajanja wa zamani wa mujini watajazia nyama kumuelezea

Papaa Amos Makalla mzee wa Mvomero:
Kwa sasa ni RC wa Dar, jina lake lilianza kuvuma kitambo sana kabla hata hajaingia kwenye siasa.

Fikiri Madinda Mukuu wa kazi: Anafahamika vizuri, wajanja wa zamani wa mujini watajazia nyama kumuelezea

Pedeshee Abdul Mkeketa:
Huyu wakati fulani aliwahi kuwa mbunge ktk Mkoa wa Morogoro, sikumbuki ni jimbo gani. kwa sasa ni marehemu.

Charles Mutawali Muzee ya Magari.
Binafsi simfahamu, wajanja wa zamani wa mujini watajazia nyama kumuelezea.

Saidi Mukuu wa lumumba:
Jamaa alikuwa dalali wa kuuza magari pande za Lumumba.

Meddy Kitendawili....?
Ben Mulokozi....?
Salim Chicago Matelefone...?
Kizaizai....?
Omary Tolu...?
Abduli Tolu...?
Joshua Limited...?
Muddy Nyamalonda mzee wa Pamba...?
China wa China...?
Shaibu Mapajero....?
Moris Mariaga Rais wa Sinza...?
Ntenze wa Ntenze....?
John Nzenze....?
Papaa Madenge....?

Note of Appreciation
.
sikujua kama huu uzi ungewavutia watu wengi kiasi hiki. niwashukuru wote mnaoufatilia na mnaochangia maoni yenu. asanteni sana wadau.[emoji1431][emoji1431][emoji1431][emoji1431]
Daah! Mkuu umenikumbusha mbali sana aisee. Sijajua umetumia muda gani kuandaa huu uzi ila hongera sana..

Hawa jamaa zamani walikuwa na majina sana na nilikuwa nawa admire sana. Sema baadhi yao wamekuja kupatwa na vipengele sana

Big up sana[emoji122][emoji122][emoji122]
 
Daah! Mkuu umenikumbusha mbali sana aisee. Sijajua umetumia muda gani kuandaa huu uzi ila hongera sana..

Hawa jamaa zamani walikuwa na majina sana na nilikuwa nawa admire sana. Sema baadhi yao wamekuja kupatwa na vipengele sana

Big up sana[emoji122][emoji122][emoji122]
[emoji1431][emoji1431][emoji1431]
 
Huyu Ndama mtoto wa ng'ombe nae kaanzia hapo hapo kwenye kijiwe cha Azam kwa shoe shiner, alikua mshamba tu tunamtia makwenzi enzi zetu. kakulia kule magomeni mapipa ukitoka mjini kushotojuu kule kama unaenda kigogo. Alitoka huko kwao kigoma mdogo kaja sijui kwa ankali wake basi tukicheza mpira tunamtia mikwenzi tu. Na mtu aliemleta mjini kwenye kile kijiwe ni jamaa mmoja nimemsahau jina lake(alikua na anaweka Culkit) yeye kijiwe chake Empress pale na kina Masudi-marehemu. eti Ndama baadae akawa pedeshee daah maisha haya acha tu. Ila deals iliomuinua nasikia walimzika myahudi kumuuzia dhahabu fake. Pedeshee ndama!!!😂😂 Ila nasikia ndama baadae alivopata pesa akamuoa mnenguaji wa kikongo wa FM academia akiitwa Mirayesa na ndio wako nae mpaka sasa.
mirayesa alikuwa muimbaji pekee wa kike kutoka fm academia
 
Msofe nilikuwa naonana sana na Mpambe wake mmoja akiitwa Ally Kitobo mdogo wake Ally aliitwa Nuhuh huyu ndiye tuliyekua karibu sana tukiishi wote Magomeni Makuti Akachube Road kipindi bado pakiitwa Somanga pamoja na jamaa zangu Yahya na Danny Malumbo (Mungu amrehemu Yahaya tumemzika kwao Kondoa Feb mwaka huu alipata ajali Tanga na IST akielekea Holili) kila ijumaa pale makutano ya mitaa ya Livingston &Amani kuna bibi alikuwa anaitwa Bi Jang’ombe alikuwa mpishi wa biriani tamu sana so tulikuwa tunaenda kula biriani la offer kutoka kwa Msofe ila jamaa sikuwahi kumuona.

Huyo Ally dereva wake ndiye aliyekuwa mshika pesa ilikuwa siyo ajabu kumkuta anashuka na 2Mill kwenye gari kwa ajili ya matumizi mbalimbali,hela yake unaifadi akikupa kazi aisee nilikuwa naamkia shikamoo nyiingi mwisho naondoka na 50K maisha yanaenda kuna siku alinipa 100,000/= ya kununua Big G original kwa ajili ya kulia mirungi sasa packet sikumbuki exactly ilikuwa bei gani ila haikuzidi Tsh 12,000/= nikajiuliza ninunue ngapi sasa nikamuuliza mdogo’ake Nuhuh ninunue ngapi akaniambia chukua moja tu change tukagawana then hakuna aliyeuliza.

Jamaa hata kama hela zao zilikuwa chafu Ila mtaa waliuchangamsha kweli kweli,Msofe kabla hajang’ang’aniwa na mamlaka alikuwa na BMW X3 metallic gold kali sana haizimwi muda wote ipo on.
Dunia uwanja w fujo
 
Duuh..
Yaani kama najikumbuka nimemaliza O level miaka ile, naeda kuegesha kwa mshikaji mitaa ya Samora, karibu na R.I.P Mzee wa Pazi basketball alikuwa na Clearing/Forward kawapa wachezaji wote dili za mishemishe za bandarini , nilikuwa nikipita sana mitaa ya Salamander.
Mzee malay nlifanya kazi kwake
Za kutumwa hapa na pale upande wa dokomaa....enzi hzo nlikuwa dogo nasoma natafuta pesa
Umenikumbusha aise,alikuwa smart sana ila kuna wakat fulani nlimuona
Alikuwa tofauti nlijisikia vibaya sana

Ova
 
Sio Mchezo..
Halafu miaka hiyo, sio muda mrefu kurudi nyuma ilikuwa kwenda UK na nchi kadhaa ni "viza free"
Nimewapeleka sana wasomali kwa wazeewa bandika bandua na vifo na vizazi halafu hao wanakwea pipa na dili linasawazishwa mpaka airport wanakuwa wameshatonywa wanapitishwa hapo ni mpaka UK.
Lyatonga si ndy alituchomesha akawaribia wabongo viza UK
Entry
Bandika bandua watu walizipiga sana

Ova
 
Back
Top Bottom