Tuwafahamu Watu Maarufu waliokuwa wanatajwa sana na Wanamuziki wa Band nchini Tanzania

Tuwafahamu Watu Maarufu waliokuwa wanatajwa sana na Wanamuziki wa Band nchini Tanzania

Aaah enzi hizo post za kwenye mashirika ya umma na serikalini ulikua unapata direct kutoka chuoni ulivyochagua. Kuna sehemu hawa viongozi wameiharibu hio nchi, sie baada ya kumaliza tu UDSM tukapelekwa kibao customs na income tax kipindi ya Mwinyi. Basi ilikua ni full shangwe pesa za kumwaga.
Ndio hivyo tumekula maisha ila wengi wetu wameenda mbele za haki pia -RIP. Kipindi hichoo huyo papaa Msoffe alikua misheni town tu wa mjini anakakaa pale Salamanda na Empress Cinema, na alikua kapanga chumba kimoja hapo kinondoni mkwajuni. Sijui papaa Ndama nae alikua fala tu mtoto wa magomeni mapipa kule chini kama unaenda kigogo, mjini anakuja kavaa kandamili, wakija delux wanaomba bia. Uwa nacheka nikija bongo jinsi nchi ilivyotulia. Na misambwanda ya ukweli ilikua enzi hizo sio sasa kijimsambwanda kidogo tu kama cha Uwoya; watu wanameza mate. [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] Tumetoka mbali wahenga.
Mgahawa mzuri mwingine ulikuwa food world unaikumbuka

Ova
 
Mgahawa mzuri mwingine ulikuwa food world unaikumbuka

Ova
dah!...food world ulikuwa jirani na askari monument.

marehemu anko wangu alikuwa anafanya kazi TRA, akitusua tu madili yake alikuwa ananipeleka food world kupata lunch.
 
Juma Ngida Nyamihela alikua muajiriwa wa Wizara ya maliasili na utalii, kwa hio hapo sio rocket science kujua ukwasi wake ulitoka wapi. Jamaa tumekunywa sana pesa yake pale Delux Magomeni mapipa hapo ilikua sitting room ya watoto wa mujini karibu wote wakitoka mjini stop ya kwanza hapo. Deals zote za Long room zilipigiwa hapo. Daah Daslama ilikua ya moto sana enzi zetu.
Juma Nyamihela alikuwa na ndugu yake akiitwa Ramadan Kiombile alikuwa rafiki yangu.Siku moja tumeenda Naye kwake Mbagala Kibonde maji,tulikuta umati wa watu wamekuja kuomba pesa na misaada mingine.Inaonekana jamaa alikuwa na utu sana.
 
Mgahawa mzuri mwingine ulikuwa food world unaikumbuka

Ova
Haswaaa Food World na kuna ingine Jamaa Fast food, ilikua hapa upenuni na hio pharmacy karibu na Empress na ingine watu wa customs tuliienda sana ilikua hapa opposite na ofisi ndogo za immigration Dar.
Mzee Sheta-RIP tena hakuna mtu wa long room alikua hamjui, nae alikua pouwa sana ukifanya nae deal la bandarini na rafiki yake akiitwa Discuss nasikia yupo UK. Ndama siku zingine alikua anakaa kwenye kijiwe cha hapo Azam Jamhuri street kwa hio round about wakifanya udalali na akina Amani na Mlelwa.
 
Haswaaa Food World na kuna ingine Jamaa Fast food, ilikua hapa upenuni na hio pharmacy karibu na Empress na ingine watu wa customs tuliienda sana ilikua hapa opposite na ofisi ndogo za immigration Dar.
Mzee Sheta-RIP tena hakuna mtu wa long room alikua hamjui, nae alikua pouwa sana ukifanya nae deal la bandarini na rafiki yake akiitwa Dismass nasikia yupo UK. Ndama siku zingine alikua anakaa kwenye kijiwe cha hapo Azam Jamhuri street kwa hio round about wakifanya udalali na akina Amani na Mlelwa.
Nyie mnaelekea mlifanya sana vurugu florida bar town hapo [emoji1]

Ova
 
Hivi hio Florida bar bado ipo?? ina juu na chini, kule juu ilikua chaka fulani hivi kuna giza kidogo mkiwa wenyewe na demu unajipigia quickie fasta fasta. [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787]
Sijapita kitambo hapo mara mwisho kupita nliona kama imejichokea
Hakuna amshaamsha kama zamani,sema pale palikuwa na utulivu
Watu wanaingia wanaongea mipango
Ila mbwa kala mbwa zanzibar hotel bado ipo hapo ndipo nlitongozaga dem wa kidosi alikuwa mchati na nkamlagaaa kwa mara kwqnza namla mhindi

Ova
 
Kuliko hiki kizaz cha wavuvi kemp mara barabeach na sehemu za starehe kibao [emoji2]
Siku hizi kuna makelele tu mkuu watu starehe hawajui [emoji1]
Enzi za ubaharia wangu nili3ndaga brazil nlikaaga huko miezi kama 14
Hilo bata na pipi nliyokula Acha tu
Fujo za copacabana hadi carnival ilinikuta huko .....Acha tu
Nashangaa bongo anakuja mtu anaanda kitu anaita carnival
Carnival ni hatariii aise,madem wakali aiseee
Kuna balaaa zinafanyika unasema hii dunia hiii

Ova
 
Awali ya yote nitangulize angalizo kwa vijana ambao maturity stage imewakuta miaka hii ya mitandao ya kijamii. Itabidi msome kimyakimya huku mkiwa mmeshika peni na karatasi kuchukua notes.

Huu uzi ni wa sisi ma-seniors, maudhui yake yatagusa zaidi vijana wenzangu ambao maturity stage iliwakuta kuanzia late 90s to early 2000s.

Mwaka 2002 mpaka 2012 mziki wa dansi ulikuwa upo kwenye prime time.

Kwa uchache tu, band zilizotamba ni FM Academia, Akudo Impact, Twanga Pepeta na Diamond Musica. Band nyingine zilikuwa zinaibuka na kupotea ndani ya muda mfupi.

Umaarufu wa hizi band ulienda sambamba na trend ya wanamuziki kutaja majina ya baadhi ya watu kwenye mashairi yao.

Majina ya hawa watu yalivuma na kuwa maarufu kuliko sura zao kwasababu miaka ile kulikuwa hakuna social platform za ku-share picha na video kama ilivyo hivi sasa.

Kutokana na kujichanganya kwangu ukijumlisha na ujanja wangu wa kimjini mjini wa miaka ile, nilifanikiwa kufahamiana na baadhi mapedeshee au wazee wa mujini ambao majina yao yalikuwa yanatajwa kwenye mziki wa dansi.

Nitataja ninaowakumbuka na wewe ongeza wa kwako.

Naandika majina yao kama yalivyokuwa yanatamkwa kwa mbwembwe na wanamuziki.

Kwa mfano kama mtu alikuwa anaitwa John, wanamuziki walikuwa wanatamka papaa John Young Millionaire Muzee ya ma-Range Rover[emoji3][emoji3].

Haya twende kazi:
Pedeshee Mychoice na kati ya Mbeya
:
huyu sijui alikuwa anapiga mishe gani huko Mbeya, watu wa Mbeya mtatusaidia.

Braza K na kati ya Tunduma:
Watu wa Tunduma mtatusaidia kutujuza kuhusu huyu jamaa, alivuma sana.

Mamaa Rukia Soloon:
Huyu bibie namfahamu, ana saloon yake ya kike mitaa ya Mikocheni barabara ya Rose Garden. Those days she was very pretty, kwa sasa utu uzima umemchukua.

Mamaa Dotnata Decoration:
Bila shaka wengi mnamkumbuka, aliwahi kuwa muigizaji maarufu kupitia ITV, baadae akaingia kwenye ujasiriamali wa kutoa huduma za decoration and catering. shughuli hizi zilimpatia mafanikio sana. sijui kwa sasa yupo wapi huyu mama. FM Academia waliwahi kumtungia wimbo wenye jina lake.

Mamaa Juddy Moshi:
Alikuwa mmiliki wa band ya Daimond Musica kwa financial support ya mshua mmoja ambaye alikuwa ni MD wa Yellow Pages, watu wa zamani wanaelewa. Juddy alikuwa mrembo si kitoto, kwa sasa umri wake umesonga mbele.

Pedeshee Akayesu Ndama Mutoto ya Ng'ombe:
Sina haja ya kumuelezea, ni mtu maarufu wa misimu yote. Wajanja wa mujini watamuelezea zaidi. Jina lake lilitajwa sana kwenye nyimbo za dansi zilizovuma.

Young Millionaire Bill gate Muzamir Katunzi:
Christian Bella aliwahi kutunga mpaka wimbo wenye jina hilohilo la Muzamir Katunzi. I don't know him personally, but it's told he was financially successful.

Papaa Msofe Chuma cha Reli hakishiki Kutu.
Sina haja ya kuandika mengi kuhusu umaarufu wa Papaa Msofe. Itoshe tu kusema jina lake liliimbwa sana halafu ni wachache waliokuwa wanajua sura yake. Walianza kuiona kwenye media alipokuwa anahudhuria viunga vya mahakama kujibu kesi yake.

Papaa Martin Kasianju.
Ni marehemu kwa sasa, huyu mshua ndio alikuwa mmiliki wa Band ya FM Academia. Nilikuwa namfahamu personally. licha ya kwamba alikuwa ni mjasiriamali na muajirwa Serikalini, pia alikuwa ni Senior Officer wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Andrew Traders na Kariakoo Big Supply: Jamaa alikuwa ni mfanyabiashara wa kuuza tairi za gari Mtaa wa Agrey Kariakoo huku akipiga michongo yake ya "general supply". Watu wa mujini wa zamani wanaelewa vizuri maana ya kampuni kusajiliwa kwa jina la general supply. Katika biashara ya kuuza tairi, alishirikiana na kaka yake, ila yeye akawa maarufu zaidi na akaaminika na wadau.

Kinje Mutoto wa Mujini:
Najua wengi mnamfahamu na zile deal zake alizokuwa anapiga. sina haja ya kumuelezea zaidi.

Pedeshee David Kabunga:
Sifahamu alikuwa ni nani, jina lake lilikuwa linatajwa sana.

Papaa Ally Kileo:
He was a prominent lawyer in town, jina lake lilikuwa linatajwa sana kwenye nyimbo za dansi.

Papaa Mutarika Mzee wa Mambo mengi:
Binafsi simfahamu, wajanja wa mujini wa zamani watajazia nyama kumuelezea.

Chef Justice Rugaibura:
Binafsi simfahamu, wajanja wa mujini wa miaka ile watajazia nyama kumuelezea.

Chief Kiumbe le Big Boss:
Anafahamika vizuri, jina lake lilitajwa na kuimbwa sana na wanamuziki wa band. wajanja wa zamani wa mujini watajazia nyama kumuelezea

Papaa Amos Makalla mzee wa Mvomero, Babaa na Gabriele:
Kwa sasa ni RC wa Dar, jina lake lilianza kuvuma kitambo sana kabla hata hajaingia kwenye siasa.

Fikiri Madinda Mukuu wa kazi: Anafahamika vizuri, wajanja wa zamani wa mujini watajazia nyama kumuelezea

Pedeshee Abdul Mkeketa:
Huyu wakati fulani aliwahi kuwa mbunge ktk Mkoa wa Morogoro, sikumbuki ni jimbo gani. kwa sasa ni marehemu.

Charles Mutawali Muzee ya Magari.
Binafsi simfahamu, wajanja wa zamani wa mujini watajazia nyama kumuelezea.

Saidi Mukuu wa lumumba:
Jamaa alikuwa dalali wa kuuza magari pande za Lumumba.

Meddy Kitendawili....?
Ben Mulokozi....?
Salim Chicago Matelefone...?
Kizaizai....?
Omary Tolu...?
Abduli Tolu...?
Joshua Limited...?
Muddy Nyamalonda mzee wa Pamba...?
China wa China...?
Shaibu Mapajero....?
Moris Mariaga Rais wa Sinza...?
Nteze wa Nteze....?
John Nzenze....?
Papaa Madenge....?
Muddy Nyambi....?
Jimmy Chokolete....?


Note of Appreciation
.
sikufikiria kama huu uzi ungepata wafuatiliaji wengi kiasi hiki. niwashukuru wote mnaoufatilia na mnaochangia maoni yenu. asanteni sana wadau.[emoji1431][emoji1431][emoji1431][emoji1431]
Kwanza umesahau msondo ngoma na sikinde. Walikuepo na hadi leo wapo ila hawakua na tabia kuwataja mapedeshee.
Christian bella juzi kwenye interview moja kasema kutaja mapedeshee ilikua pesa. Yaani ni mtaji ukiwataja wanakupa pesa.
Halafu pedeshee neno limetoholewa kutoka kifarannsa PDG, wanatamka pedejee. Ni sawa na CEO, yaani mkurugenzi mkuu wa kampuni. Kule congo ni watu noti sana. Ukiwataja kwenye wimbo enzi hizo wanakujaza manoti. Sijui siku hizi.
 
Siku hizi kuna makelele tu mkuu watu starehe hawajui [emoji1]
Enzi za ubaharia wangu nili3ndaga brazil nlikaaga huko miezi kama 14
Hilo bata na pipi nliyokula Acha tu
Fujo za copacabana hadi carnival ilinikuta huko .....Acha tu
Nashangaa bongo anakuja mtu anaanda kitu anaita carnival
Carnival ni hatariii aise,madem wakali aiseee
Kuna balaaa zinafanyika unasema hii dunia hiii

Ova
Wewe ulieenda huko ambako starehe zilipozaliwa lazm huku uone hamna kitu aisee kweli 😁
 
Ina maana hawa jamaa wamekula bata kuliko vijana wa sahv 😁
Sasa hivi hamna kitu, hamna raha yoyote au sie ndio tunaoona hivyo labda vijana wenyewe wanafurahia zaidi. Mimi nimekuja bongo naenda hizo bar zao hamna kitu naona zimepoa sana. Sijui kwa sababu nimekua muhenga na kunywa sinywi. Muziki sasa hivi daah siwezi kabisa hayo matamasha yao vurugu tupu. enzi zile tunaenda kumbi mbali mbali ziko vizuri sana.
 
Sasa hivi hamna kitu, hamna raha yoyote au sie ndio tunaoona hivyo labda vijana wenyewe wanafurahia zaidi. Mimi nimekuja bongo naenda hizo bar zao hamna kitu naona zimepoa sana. Sijui kwa sababu nimekua muhenga na kunywa sinywi. Muziki sasa hivi daah siwezi kabisa hayo matamasha yao vurugu tupu. enzi zile tunaenda kumbi mbali mbali ziko vizuri sana.
Wanasema kila zama na mambo yake 😃
 
Ni kweli unaweza kuta vijana wanafurahi bata zao, sema mitaa ya mjini ikifika saa za jioni inapoa sana watu wote wanarudi makwao huko sijui tegeta, kimara, mbagala etc. zamani hio mida ni ya vurugu mjini watu wanarejea huko giza tayari wanaanzia Florida bar au Georgis pale. daa vijiwe vya mjini vingine nimevisahau sasa kuna kingine kilikua huku karibu na lumumba ilikua hotel ya mzee wa kichaga ikiitwa Happy hotel ina mpaka summit bar., na ingine Keys Hotel na pale Railway station juu kulikua na ki bar hivi.
 
Ni kweli unaweza kuta vijana wanafurahi bata zao, sema mitaa ya mjini ikifika saa za jioni inapoa sana watu wote wanarudi makwao huko sijui tegeta, kimara, mbagala etc. zamani hio mida ni ya vurugu mjini watu wanarejea huko giza tayari wanaanzia Florida bar au Georgis pale. daa vijiwe vya mjini vingine nimevisahau sasa kuna kingine kilikua huku karibu na lumumba ilikua hotel ya mzee wa kichaga ikiitwa Happy hotel ina mpaka summit bar., na ingine Keys Hotel na pale Railway station juu kulikua na ki bar hivi.
Newhappy kulikua na mbuzi choma nzuri sana,pia kulikua na fastfood zahir mitaa ya kitumbini...pia kulikua na mbuzi choma hapo mnazi mmpja jirani na nbc bank
 
Back
Top Bottom