GentleGiant
JF-Expert Member
- Sep 22, 2021
- 585
- 546
(Kijana)
Jioni ya leo siwezi kulala na njaa tena.Nitafanya kila namna nipate chakula. Nguvu nazo zimeanza kuniishia, sijui kama nitafanikiwa kutoka salama lakini siwezi kulala njaa na leo. Kuomba watu wameshanichoka, kazi hata za vibarua zimekuwa ngumu kupatikana nikae nife na njaa? Hapana. Mama yangu na wadogo zangu pia siwezi kuwaona wanalala na njaa na leo tena. Wacha nitoke nikatafute chochote kitakachokatiza mbele ya macho yangu.
(Baada ya masaa kadhaa)
Ni kweli wamenikamata nikiiba lakini wanajua kwanini nimefanya hivi?najaribu kuwaeleza hawataki kunisikia wanaendelea kunipiga.Watu wanazidi kuongezeka,wengine wanaonekana na hasira sana. Wanaokuja sasa hivi wanakuja na mapanga na mashoka,sijui kama leo nitatoka salama.Naanza kufikiri zile arobaini za mwizi ndo zimefika.Lakini mbona mimi hii ni mara yangu ya kwanza?
Ni kweli nilishawahi kuhusishwa na wizi hapa mtaani lakini hii ni mara yangu ya kwanza.Wananchi wanaendelea kunipiga wakisisitiza kuwa walikuwa wakinitafuta muda mrefu sasa leo wamenipata.Kwenye hili kundi wengine nawafahamu lakini na wao hawataki kunisaidia. Nguvu zinaniishia ,damu nyingi nimepoteza,nimepata majeraha makubwa na sasa nimeanza kukubali kuwa siku yangu imefika.
Namfikiria mama yangu atakavyojisikia atakapopata habari hii,sijui kama ataelewa kuwa nimefanya haya yote kwa ajili yake.Sijui atafikiri mwanaye ni mwizi wa siku zote au atahisi nimesingiziwa.Maumivu ninayopata kwa kufikiria haya yanazidi maumivu ya kipigo. Oh mama yangu nisamehe sana.Natamani ningeweza kukuhudumia kama wengine wanavyohudumia wazazi wao ila uwezo wa kufanya hivyo ndio sijajaliwa.Naahidi kama nikifanikiwa kutoka salama hapa nitatafuta namna nyingine ya halali ya kutafuta kipato ili nikuhudumie.
(Polisi)
Hii taarifa ya huyu mwizi aliyekamatwa inataka kuniharibia ratiba zangu.Kwanza hata nikienda saa hii nina hakika nitakuta washamuua.Hata hivyo wamuue tu ili iwe fundisho kwa wengine maana tumeshachoka kuhangaika na hawa watu. Ni kweli nina wajibu wa kumlinda na ni kweli natambua raia hawana haki ya kujichukulia sheria mikononi lakini hizi tabia zimezidi huko mitaani.Bila kuangamizwa hawa watu wataendelea kutusumbua na kuongezeka.
Acha raia mara moja moja waamue wenyewe. Hapa cha kufanya ni kuchelewa kufika eneo la tukio ili tukute washammaliza.Nafsi inaniambia ninachotaka kukifanya sio sahihi lakini kwani mimi ndiyo nilimtuma akaibe?kijana ana nguvu kwanini asijishughulishe na shughuli halali? Ngoja lipite kama lisaa limoja hivi kisha twende,kama akiwa hajafa mpaka muda huo basi itakuwa ndiyo salama yake,wametuchosha sana hawa vijana.
(Mama Mzazi)
Jana tumelala njaa ila leo kijana wangu ameahidi atapambana tupate chochote.Mwanangu ana moyo sana wa kujituma tatizo tu hakuna wa kumpa kazi. Mungu amlinde kwenye mihangaiko yake arudi salama maana barabarani kuna mambo mengi.Hebu ngoja nikajipumzishe barazani maana mwili hauna hata nguvu ya kufanya chochote.
(Baada ya muda mchache )
Wamemuua?Mwanangu sio mwizi jamani,mwanangu hana hizo tabia.,wamemsingizia na kumuua mwanangu.Nitakuwa mgeni wa nani mimi?mwanangu ndo alikuwa tumaini letu hapa nyumbani sasa tutafanya nini sisi? Oh mwanangu,wamekusingizia na kukuua,uliniaga unaenda kutafuta kumbe ulikuwa unaenda kutafuta kifo, oh Mungu wangu mbona unanitenda hivi?Kosa langu ni lipi mpaka kustahili kupitia haya.Mwanangu alikuwa na ndoto nyingi sana ila watu wameamua kuzikatisha kwa ukatili wao.Hapana siwezi kuamini mpaka nione mwili wake.Pengine sio yeye wamemfananisha.Kwanza mitaa ya huko mwanangu haendagi mara kwa mara. Mwanangu sio mwizi,watu walivumisha hizi habari lakini alinithibitishia yeye sio mwizi. Oh Mungu wangu naomba hii iwe ni ndoto mbaya ambayo muda si mrefu nitaamka.
(Mwananchi)
Wametuchosha hawa,hii ndio dawa yao.Sasa hivi ukikamata unamaliza kabisa. Hatuwezi kuwa tunatafuta hela kwa tabu halafu wao wanakuja kutuibia.Hakikisha unachoma kabisa na moto maana ukimuacha anaweza akaamka akaja kutusumbua. Huyu kijana tulishasikiaga habari zake leo ndio tumemkamata.Na huu ni mwanzo tu yeyote atakayekamatwa ataishia kama huyu.Vijana shule hawataki,kazi hawataki halafu wanataka maisha mazuri.Hakuna vya bure maishani. Hapa hapafai tena acha niondoke polisi wasije wakanikuta eneo la tukio nikajikuta naingia matatani.
Ni jukumu la wote
Pamoja na jitihada za kuendelea kupambana na uhalifu lakini matukio ya uhalifu bado yameendelea kushika kasi kwenye jamii zetu. Baadhi ya raia kutokana na kero zinazotokana na uhalifu huu na wenyewe wameamua kuchukua sheria mkononi kukomesha vitendo hivi. Kwa mwaka 2020 pekee palikuwa na matukio 443 ya raia kujichukulia sheria mkononi. Vitendo hivi vimekuwa vikipingwa vikali kwa sababu kisheria mtu si mkosaji mpaka itakapoamuliwa na mahakama kuwa amekosa na kujichukulia sheria mkononi kunamuondolea haki ya kujitetea. Raia wamekuwa wakilalama kuwa wanapowapeleka wahalifu polisi baada ya siku chache wanawaona mitaani hivyo kwa wao wanaona ni sahihi kuchukua sheria mkononi.
Katika kutengeneza jamii zinazofuata utawala wa sheria ni wajibu wa kila mmoja kufuata sheria zilizopo ili kupata jamii inayozingatia haki na utawala bora.Kufuata sheria sio jukumu la wanasiasa,watumishi wa serikali au vyombo vya usalama pekee bali ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha haki za kila mmoja zinaheshimiwa. Polisi wamekuwa wakilalamikiwa kutofuata taratibu,wanasiasa wamekuwa wakilalamikiwa kutokufuata sheria na watumishi wa umma pia lakini jamii inapoamua kumpiga mwizi au mwalifu yeyote inakuwa haipunguzi idadi ya watu wanaovunja sheria bali inaongeza.Hii ni kwa sababu kitendo walichokifanya ni kinyume cha sheria.
Nini kifanyike?
Jamii inatakiwa kuhakikisha malezi ya pamoja kwa watoto na vijana ili kuwajengea uwezo wa kujitegemea wanapokuwa wakubwa ili kupunguza uwezekano wa kujihusisha na vitendo vya kihalifu.Polisi wazingatie haki ya kuishi na kulinda usalama wa kila mmoja hata kama atahusishwa na uhalifu na kwa mantiki hiyo wafike kwenye maeneo ya matukio kwa wakati ili kuweza kuokoka uhai na majeraha yanayoweza kusababishwa na kushambuliwa.Lakini pia serikali iendelee kuboresha mazingira ambayo yatapelekea uzalishwaji wa ajira,watengeneze mazingira mazuri ya biashara ili vijana wanaojaribu kujiajiri basi wasikutane na vikwazo na kushindwa kuendelea.
Takwimu zilizotajwa ni Takwimu za hali ya uhalifu Januari mpaka desemba 2020 Tanzania.

Upvote
0