Utangulizi.
Kwa miaka mingi sana vijana wakiume walikua wakipewa kipaumbele katika nyanja tofauti tofauti lakini mambo yalianza kubadilika pale matukio ya unyanyasaji wa ulipoongezeka hasa kwa watoto wa kike. Hapa ndipo Serikali na asasi nyingine zisizo za kiserikali kuanzisha kampeni tofauti tofauti ambazo zilikua zinatetea na kupinga matukio ya unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake na hapa mbinu nyingi zilitumika ikiwa ni pamoja kuwawezesha watoto wa kike ili kupunguza utegemezi kwenye nyanja ya kiuchumi na kielimu.
Mikopo mingi na fursa nyingi zilianza kufunguliwa kwa wanawake na watoto wengi wa kike na kupelekea ukatili wa kijinsia mstulio ya unyanyasaji kupungua kwa kasi nchini. Kupewa mikopo ya 10% inayotolewa na halmashauri mbalimbali nchini kipaumbele kikiwa ni vikundi vya wanawake, wazee na watu wenye ulemavu.
Kutokana na hili sasa imepelekea kwa miaka 10 ya hivi sasa kuwaacha nyuma Vijana wa kiume na kupelekea kuanza kusahaulika hata katika shughuli za kiuchumi, kijamii na hata kisiasa. Mfano serikalini kupitia chombo chake cha Bunge.
Wabunge wa viti maalumu ni wanawake (watoto wa kike) na hata kwenye mikopo ya 10% inayotolewa na halmashauri vipaumbele kwa miaka ya hivi karibuni ni kwa wanawake, wazee na watu wenye ulemavu hali ya kuwa kuna kundi kubwa la vijana wa kiume wapo hapo nyuma. Hata kwenye kilimo hivi sasa mashamba mengi yamekua yakiongozwa na wanawake, katika ajira vivyohivyo wanawawake wamekua wakipewa kipaumbele kikubwa sana. Je, kwanini kusiwe hata kunausawa katika uteuzi wa wabunge wa viti maalumu kwa wanaume ili kuweza kuwazungumzia vijana wakiume serikalini.
Pichani ni idadi ya wabunge wa vitimaalumu kutoka Chama cha Demokrasia na maendeleo ( CHADEMA); (Picha kutoka tovuti ya serikali, 2023)
Hivyo basi kutokana na hilo kuna kundi kubwa sana la vijana wakiume huko nje ambao wamekua wakipata tabu sana kujikweza na kujiendeleza wao wenyewe na hata kama wakitokea kusaidiwa na serikali au asasi zisizo za kiserikali basi ni kwa kiasi kidogo sana na hii hupelekea hata kuzaliwa kwa makundi maovu yanayohatarisha amani na usalama wa raia wa Tanzania.
Ukiangalia kundi kubwa la wahalifu waliokua wanakamatwa na waliokua wakitafutwa na askari wa jeshi la polisi almaarufu Panya Road wengi wao walikua vijana wakiume na hata idadi kubwa ya wahalifu (majambazi) wanaouawa au kukamatwa kwa makosa ya unyang’anyi kwa kutumia silaa au kutokutumia silaa ni wakiume.
Picha kutoka wikipedia, 2023.
Picha hii inaonesha vijana wengi wa kiume wakijihusisha na uhalifu tofauti na vijana wa kike. Hivyo basi muandishi anaasa kwa sekta za kiserikali na zile zisizo za kiserikali kuwaunga mkono na kuwainua vijana wa kiume ili kupunguza matatizo ya kihalifu nchini.
Hata wagonjwa wengi wa akili na wanosumbuliwa na magonjwa ya akili wengi wao ni wanaume hii yote inatokana na wengi wao kutokupata uwezeshwaji wa vile wanavyovihitaji ili kutimiza ndoto zao na matokeo yake wanaanza kuingia kwenye makundi ya ajabu na ya kihalifu. Msongo wa mawazo waathirika wengi ni watoto wa kiume na hii ni kutokana na wanume wengi kuachwa nyuma kwenye shughuli nyingi ikiwemo kisiasa, kiuchumi na kijamii. Mwaka 2018 tulikuwa na wagonjwa 357,799 waliokwenda kupatiwa matibabu, 2019 walikuwa 380,000, mwaka 2020 walifika zaidi ya 500,000,” (Dr. Omary ubuyu, 2021) kundi hilo la wagonjwa 500,000 asilimia kubwa ikiwa ni wanaume. Hivyo basi wanatakiwa kuzingatiwa ili kupunguza idadi yao.
Kitu kingine ukiangalia hata kundi kubwa la watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja wakijulikana kama Mashoga ni kwasababu ya kutaka urahisi wa maisha na kutaka kuendelea kiuchumi, lakini kundi hili kubwa lingeangaliwa kwa namna ya utofauti na kurudisha hali ya kuwa kumbuka vijana wakiume huenda wasingekuwepo au wangekuwepo kwa kiasi kidogo sana.
Picha imetolewa moja kwa moja mtandaoni.
Serikali na asasi zisizo za kiserikali zinatakiwa kurudisha nia thabiti ya kuwasaidia vijana wakiume kwenye nyanja tofauti tofauti ili kurudisha uwiano katika fursa za kimaendeleo.
Kwa muonekano tu, sababu kubwa ni kutokana na ugumu wa maisha na kutaka wepesi wa maisha na hii yote ni kwasababu ya kuachwa nyuma katika kuwezeshwa.
Kwenye swala la unyanyasaji wa kijinsia, kwa miaka ya nyuma ukisikia taarifa ya unyanyasaji wa kijinsia basi kundi tendewa huwa ni watoto wa kike lakini kwa miaka ya hivi karibuni ukisikia unyanyasaji wa kijinsia usistaajabu kusikia kundi tendwa ni watoto wa kiume ikiwa ni pamoja na kupigwa, kulawitiwa na hata baadhi yao kunajisiwa lakini kwa kuwa vitendo hivi ni nadra kuzungumzwa huwa havifiki ipo mikoa ambayo wanaume wanapigwa na kunyanyaswa lakini kwakua hakuna wakuwasemea na kuhisi unyonge vitendo hivi mara nyingi huwa haviripotiwi sana na hata serikali pia haijaweka nguvu kubwa katika kutetea haki zao.
Pia tukijakutazama hata kwenye afya hususani afya ya uzazi wahanga wengi ni vijana wa kiume, na hii hutokana na vinaja wengi wa kiume kutokujengewa mazingira thabiti ya kujiona wao ni vijana wenye weledi na wenye mchango mkubwa kwenye uzalishaji wa kitaifa. Ukiangalia madawa mengi ya uzazi ni kuongeza nguvu za kiume na si kitu kingine na hii inaashiria kwamba vijana wengi wa kiume wameachwa nyuma sana kwenye maswala haya ya uzazi ikiwa ni pamoja na vyakula, virutubisho na ushauri mbali mbaili hadi kupelekea kuingia kwenye wimbi la ukosefu wa nguvu kwaajili ya uzalishaji.
Hitimisho
Kutokana na haya, ili kuweza kuwasaidia vijana katika maendeleo ya jamii, uchumi na siasa na maendeleo ya taifa kwa ujumla serikali na asasi zisizo za kiserikali zinatakiwa kuwapa kipaumbele vijana wa kiume katika kuwaendeleza katika maendeleo ya taifa hususani kwenye masuala ya uchumi, siasa na jamii kiujumla ili kupunguza wimbi la vijana wa kiume ambao wanakua wa hovyo katika nchi yetu. Na kuna madhara mengi sana ya kuwafanya wanawake kuwa vipaumbele katika shughuli hizo ikiwa ni pamoja na kudharau yale yafanywayo na wanaume katika shughuli za kimaendeleo.

Attachments
Upvote
1