Musiba na willy Gamba "wake" alitukamata sana wengine miaka ile,mpaka eti tukawa tunamtengeneza willy gamba vichwani mwetu kwamba ni kijana fulani mtanashati hivi..shushushu hatari mwenye uwezo wa hali ya juu wa sanaa za mapigano.Nakumbuka willy gamba na ushujaa wake kwenye vitabu vya Elvis Musiba kama:
Njama
kikosi cha kisasi
Hofu
etc
17)John Rutahisingwa
Euphrace Kezilahabi
1. Roza Mistika
XP hivyo vyote uli visoma? You must be very rich! Riwaya zina utamu wake ingawa sidhani kama ukienda pale TPH Samora Avenue utavikuta hivyo vitabu
Vitabu ambavyo viko katika hazina yangu. TUTARUDI NA ROHO ZETU?, ROHO YA PAKA, SALAMU TOKA KUZIMU, MALAIKA WA SHETANI, PESA ZAKO ZINANUKA, LAZIMA UFE JORAM, DIMBWI LA DAMU vya BEN MTOBWA..NJAMA, KIKOMO, KIKOSI CHA KISASI vya ELVIS MUSIBA pia ninacho MASHIMO YA MFALME SULEIMAN. Na KIJASHO CHEMBAMBA, JOGOO LA SHAMBA NA MSAKO WA HAYANI vya EDIE GANZEL. Watunzi wote wazuri wamesha fariki.
Mzimu wa Watu wa Kale, Kisiwa cha Giningi, Duniani Kuna Watu, Siri ya Sifuri, Mke Mmoja Watume Watatu, Mwana wa Yungi Hulewa, By Muhammed Said Abdulla
Umenikumbusha mbaaali sana kuhusu mtunzi huyu Ammi Moh'd.
Hakika asiyesoma vitabu vake basi amekosa mengi sana. Siku zote nilikuwa namfananisha na Marhum Shaaban Roberts.
Mkuu hivyo vitabu vyote nilivisoma ndugu yangu... Mimi nilikuwa msomaji mzuri sana wa riwaya, na kwa bahati nzuri nilipokuwa shule ya msingi nilikuwa ndio mtunza maktaba ya shule, na Alhamdulillah shule niliyo soma ilikuwa na vitabu vingi sana, nadhani robo ya vitabu viliishia home kwangu... ah ah ah ah.
Nadhani tabia ya usomaji vitabu nimerithi kwa mzee wangu. Home kulikuwa na Novel za aina nyingi sana, nami nilikuwa siishi kumsumbua anisomee...! Na si vitabu tu hata nikiokota vijarida uko nje basi ilikuwa lazima nikipeleke home aidha mama au baba wapate kunisomea.... Hii ilipelekea nipelekwe shule ya vidudu kabla ya umri wangu kufika na ikasababisha mimi kujua kusoma haraka sana.
Hapa ningependa kumtambua Mtunzi na mfanya biashara maarufu sana kule kanda ya Ziwa.
Elistablus Elvis Musiba. yeye alitunga vitabu hivi
1. Kikosi cha kisasi
2. Njama
3. Kikomo
4. Hujuma.
Kabla sijaanza kusoma 'novel' za kiingereza k.m. James Hadley Chase na Nick Carter, huyu mwandishi mzalendo alikuwa ananivutia sana na hadithi zake hasa zile zilizokuwa zikitoka gazetini (sikumbuki ni gazeti gani). Kuna hadithi yake ilikuwa inasimulia kachero mmoja aliyekuwa anapambana na kundi la majambazi yaliyokuwa yanaitwa 'Vinyamkela'. Nilikuwa najificha chumbani ili nisome hizo hadithi bila bughdha, na mara nyingi tu nilikuwa natafutwa sionekani, hasa wakati wa chakula, kumbe nasoma hadithi za kusisimua za 'Vinyamkela'. R.I.P. Eddie Ganzel, you really made my days!.... KIJASHO CHEMBAMBA ! ................... Eddi Ganzel