Ukatili wa kijinsia kwa watoto ni kitendo chochote anachoweza kufanyiwa mtoto na kikasababishia madhara ya kimwili, kisaikolojia na kiafya. Ukatili wa kijinsia kwa watoto unaweza kusababisha madhara mengi ikiwemo mtoto kutengwa katika jamii, mtoto mwathiriwa wa ukatili kujiua na mateso mengine yanayoweza kutishia uhai kwa mtoto.
Pamoja na juhudi zote za Serikali, watu binafsi, mashirika mbalimbali ya kitaifa na kimataifa na jamii kwa ujumla katika kupambana na ukatili wa kijinsia kwa watoto, suala hili bado ni mwiba mkubwa katika jamii. Ni suala linaloonekana kuota mizizi kila uchwao badala ya kupungua au kuisha kabisa.
Mfano, ripoti ya jeshi la polisi ya 2021 nchini Tanzania inataja miongoni mwa ukatili dhidi ya watoto ulioripotiwa kwa kiwango kikubwa kuwa dhuluma za kingono ambapo katika mwaka wa 2020 kuliripotiwa visa 7263 ikiwa ni ongezeko la asilimia 26 ikilinganishwa na mwaka 2015 ambapo vilirekodiwa visa 5803, hii ikiwa ni sawa na visa 615 kwa mwezi.
Hili ni jambo linalohitaji muda, elimu, uwekezaji, ushirikishwaji wa jamii na uwajibikaji kwa viongozi na wasimamizi wa mamlaka ili kupambana na ukatili huu. Haiwezekani katika karne hii ya 21 ya ukuaji wa teknolojia mtoto anaendelea kufanyiwa ukatili.
Watoto ndio tunategemea wawe viongozi wetu katika Taifa, tunategemea wawe na familia yaani wazazi na walezi hivyo kama Taifa na jamii tunapaswa kushirikiana ili kuwalinda kwa juhudi na maarifa yote.
Katika Dunia hii ya teknolojia na utandawazi, kwa upande wangu tukifanya yafuatayo, tunaweza kukabiliana na kupunguza hili tatizo kama siyo kumaliza kabisa;-
𝗞𝘂𝗯𝗼𝗿𝗲𝘀𝗵𝗮 𝗺𝘁𝗮𝗮𝗹𝗮 𝘄𝗮 𝗲𝗹𝗶𝗺𝘂; Hii ikiwa na maana ya kwamba, watoto wafundishwe elimu ya kukabiliana na ukatili wa kijinsia kuanzia elimu ya awali hadi chuo kikuu. Yaani kwenye mtaala wetu wa elimu, kunaweza kukawa na somo la lazima linalohusu masuala ya jinsia na ukatili na namna ya kukabiliana nao ambalo kama siyo lazima, linaweza kufundishwa hata siku moja ya wiki ikiwa ni pamoja na maboresho ya mara kwa mara kuhusu sera ya elimu na hatimaye kulifanya somo rasmi. Hii itawafanya watoto shuleni kuweza kujitambua mapema na hata wakianza kuimba nyimbo wataweza kuelewa zaidi na wataweza kuripoti ukatili kabla au baada ya kutokea kwa wakati sahihi na wahusika waweze kuchukuliwa hatua kali za kisheria. Kama inawezekana kuongeza na kufanya mabadiliko ya tahasusi katika elimu ya sekondari, hili pia linawezekana.
Baada ya kuwafundisha watoto shuleni, tunaweza kufundisha pia jamii kuhusu matumizi ya alama za mikono kupitia matamasha, mikutano na semina mbalimbali ili kuweza kumsaidia mtoto kuokolewa pale anapokuwa kwenye hatari kupitia mitandao ya kijamii, katika maeneo ya umma au hata nyumbani na katika mazingira yoyote hatarishi kwake. Pia elimu zaidi inaweza kutolewa kwa jamii na wana usalama kuweza kutambua mtu anayepiga namba ya dharura kuhitaji msaada au kuripoti tukio la ukatili. Kwa mfano; mtu anaweza kupiga namba ya dharura akihitaji bodaboda ya usafiri kumpeleka sehemu husika kwa msisitizo
𝗠𝗮𝘁𝘂𝗺𝗶𝘇𝗶 𝘆𝗮 𝗺𝗮𝘁𝗮𝗻𝗴𝗮𝘇𝗼 𝘆𝗮 𝗸𝘂𝗹𝗶𝗽𝗶𝗮 𝗸𝗶𝗱𝗶𝗷𝗶𝘁𝗮𝗹𝗶 𝗸𝗮𝘁𝗶𝗸𝗮 𝗺𝗶𝘁𝗮𝗻𝗱𝗮𝗼 𝘆𝗮 𝗸𝗶𝗷𝗮𝗺𝗶𝗶(𝗦𝗽𝗼𝗻𝘀𝗼𝗿𝗲𝗱 𝗔𝗱𝘀); Kama ilivyo kwenye Televisheni, Radio, Magazeti, n.k, matumizi ya matangazo ya kulipia(Sponsored ads)katika mitandao ya kijamii kama 𝗬𝗼𝘂𝘁𝘂𝗯𝗲, 𝗚𝗼𝗼𝗴𝗹𝗲, 𝗙𝗮𝗰𝗲𝗯𝗼𝗼𝗸, 𝗧𝗶𝗸𝘁𝗼𝗸, 𝗶𝗻𝘀𝘁𝗮𝗴𝗿𝗮𝗺, 𝗫, 𝗬𝗼𝘂𝘁𝘂𝗯𝗲 𝗸𝗶𝗱𝘀, 𝗻.𝗸. yameongozeka sana. Na katika matumizi ya mitandao ya kijamii, jamii(watu wazima na watoto) wapo bega kwa bega katika kupata elimu, kufanya biashara, kuwasiliana na kujifunza stadi mbalimbali za maisha, hivyo basi; Serikali kupitia wizara husika inaweza kutumia nafasi hii kuelimisha jamii kwa ujumla(watu wazima na watoto) madhara, namna ya kukabiliana na kupinga ukatili wa kijinsia kwa watoto.
𝗞𝘂𝗮𝗻𝘇𝗶𝘀𝗵𝗮 𝘁𝗲𝗹𝗲𝘃𝗶𝘀𝗵𝗲𝗻𝗶(𝗧𝘃) 𝗻𝗮 𝗿𝗲𝗱𝗶𝗼 𝘇𝗶𝗻𝗮𝘇𝗼𝘁𝗼𝗮 𝗲𝗹𝗶𝗺𝘂 𝗸𝘂𝗵𝘂𝘀𝘂 𝘂𝗸𝗮𝘁𝗶𝗹𝗶 𝗸𝘄𝗮 𝘂𝗷𝘂𝗺𝗹𝗮; Hii inaweza kushangaza kidogo kutokana na mawazo yangu lakini naamini hii pia inaweza kuwa mojawapo ya njia zitakazosaidia kupunguza tatizo la ukatili wa kijinsia katika jamii. Hii ina maana kwamba, wanaharakati wa kutetea haki za binadamu, wanasaikolojia na wataalamu mbalimbali watatumia jukwaa hili kuelimisha jamii kuhusu kutambua, kujilinda na kuripoti aina za ukatili wa kijinsia. Waandishi wa habari wataibua aina mbalimbali za ukatili hasa kwa wazee, wanawake, walemavu, wanaume, watoto na jamii kwa ujumla na kuonesha mustakabali na hatua zilizochukuliwa kwenye matukio husika. Hii yote inapaswa kufanywa na serikali kupitia wizara husika kwa kushirikiana na mashirika mbalimbali ya Umma, haki za binadamu ya kitaifa na kimataifa na jamii kwa ujumla. Ni kama ilivyo sasa tunavyotumia 𝗦𝗮𝗳𝗮𝗿𝗶 𝗧𝘃 kueneza utalii wetu wa ndani ya nchi na kuvutia watalii wengi zaidi ndani na nje ya nchi.
Yote kwa yote, ukatili wa aina yoyote haupaswi kupewa nafasi kwa namna yoyote ile katika jamii. Ni vyema jamii ikaelimishwa zaidi na zaidi kuhusu ukatili wa kijinsia kwa kutumia kila mbinu.
Ukatili wa kijinsia hasa kwa watoto ni adui kama adui wengine i.e ujinga na umasikini. Ni kama tupo vitani, yatupasa kutumia medani zote za kivita ili kupambana na adui yetu ambaye ni ukatili wa kijinsia kwa watoto ili tuwe na Taifa lililo salama zaidi.
Wako;
Pmanga

Upvote
2