Ukatili wa kijinsia kwa watoto ni kitendo chochote anachoweza kufanyiwa mtoto na kikasababishia madhara ya kimwili, kisaikolojia na kiafya. Ukatili wa kijinsia kwa watoto unaweza kusababisha madhara mengi ikiwemo mtoto kutengwa katika jamii, mtoto mwathiriwa wa ukatili kujiua na mateso mengine yanayoweza kutishia uhai kwa mtoto.
Pamoja na juhudi zote za Serikali, watu binafsi, mashirika mbalimbali ya kitaifa na kimataifa na jamii kwa ujumla katika kupambana na ukatili wa kijinsia kwa watoto, suala hili bado ni mwiba mkubwa katika jamii. Ni suala linaloonekana kuota mizizi kila uchwao badala ya kupungua au kuisha kabisa.
Mfano, ripoti ya jeshi la polisi ya 2021 nchini Tanzania inataja miongoni mwa ukatili dhidi ya watoto ulioripotiwa kwa kiwango kikubwa kuwa dhuluma za kingono ambapo katika mwaka wa 2020 kuliripotiwa visa 7263 ikiwa ni ongezeko la asilimia 26 ikilinganishwa na mwaka 2015 ambapo vilirekodiwa visa 5803, hii ikiwa ni sawa na visa 615 kwa mwezi.
Hili ni jambo linalohitaji muda, elimu, uwekezaji, ushirikishwaji wa jamii na uwajibikaji kwa viongozi na wasimamizi wa mamlaka ili kupambana na ukatili huu. Haiwezekani katika karne hii ya 21 ya ukuaji wa teknolojia mtoto anaendelea kufanyiwa ukatili.
Watoto ndio tunategemea wawe viongozi wetu katika Taifa, tunategemea wawe na familia yaani wazazi na walezi hivyo kama Taifa na jamii tunapaswa kushirikiana ili kuwalinda kwa juhudi na maarifa yote.
Katika Dunia hii ya teknolojia na utandawazi, kwa upande wangu tukifanya yafuatayo, tunaweza kukabiliana na kupunguza hili tatizo kama siyo kumaliza kabisa;-
๐๐๐ฏ๐ผ๐ฟ๐ฒ๐๐ต๐ฎ ๐บ๐๐ฎ๐ฎ๐น๐ฎ ๐๐ฎ ๐ฒ๐น๐ถ๐บ๐; Hii ikiwa na maana ya kwamba, watoto wafundishwe elimu ya kukabiliana na ukatili wa kijinsia kuanzia elimu ya awali hadi chuo kikuu. Yaani kwenye mtaala wetu wa elimu, kunaweza kukawa na somo la lazima linalohusu masuala ya jinsia na ukatili na namna ya kukabiliana nao ambalo kama siyo lazima, linaweza kufundishwa hata siku moja ya wiki ikiwa ni pamoja na maboresho ya mara kwa mara kuhusu sera ya elimu na hatimaye kulifanya somo rasmi. Hii itawafanya watoto shuleni kuweza kujitambua mapema na hata wakianza kuimba nyimbo wataweza kuelewa zaidi na wataweza kuripoti ukatili kabla au baada ya kutokea kwa wakati sahihi na wahusika waweze kuchukuliwa hatua kali za kisheria. Kama inawezekana kuongeza na kufanya mabadiliko ya tahasusi katika elimu ya sekondari, hili pia linawezekana.
Baada ya kuwafundisha watoto shuleni, tunaweza kufundisha pia jamii kuhusu matumizi ya alama za mikono kupitia matamasha, mikutano na semina mbalimbali ili kuweza kumsaidia mtoto kuokolewa pale anapokuwa kwenye hatari kupitia mitandao ya kijamii, katika maeneo ya umma au hata nyumbani na katika mazingira yoyote hatarishi kwake. Pia elimu zaidi inaweza kutolewa kwa jamii na wana usalama kuweza kutambua mtu anayepiga namba ya dharura kuhitaji msaada au kuripoti tukio la ukatili. Kwa mfano; mtu anaweza kupiga namba ya dharura akihitaji bodaboda ya usafiri kumpeleka sehemu husika kwa msisitizo
๐ ๐ฎ๐๐๐บ๐ถ๐๐ถ ๐๐ฎ ๐บ๐ฎ๐๐ฎ๐ป๐ด๐ฎ๐๐ผ ๐๐ฎ ๐ธ๐๐น๐ถ๐ฝ๐ถ๐ฎ ๐ธ๐ถ๐ฑ๐ถ๐ท๐ถ๐๐ฎ๐น๐ถ ๐ธ๐ฎ๐๐ถ๐ธ๐ฎ ๐บ๐ถ๐๐ฎ๐ป๐ฑ๐ฎ๐ผ ๐๐ฎ ๐ธ๐ถ๐ท๐ฎ๐บ๐ถ๐ถ(๐ฆ๐ฝ๐ผ๐ป๐๐ผ๐ฟ๐ฒ๐ฑ ๐๐ฑ๐); Kama ilivyo kwenye Televisheni, Radio, Magazeti, n.k, matumizi ya matangazo ya kulipia(Sponsored ads)katika mitandao ya kijamii kama ๐ฌ๐ผ๐๐๐๐ฏ๐ฒ, ๐๐ผ๐ผ๐ด๐น๐ฒ, ๐๐ฎ๐ฐ๐ฒ๐ฏ๐ผ๐ผ๐ธ, ๐ง๐ถ๐ธ๐๐ผ๐ธ, ๐ถ๐ป๐๐๐ฎ๐ด๐ฟ๐ฎ๐บ, ๐ซ, ๐ฌ๐ผ๐๐๐๐ฏ๐ฒ ๐ธ๐ถ๐ฑ๐, ๐ป.๐ธ. yameongozeka sana. Na katika matumizi ya mitandao ya kijamii, jamii(watu wazima na watoto) wapo bega kwa bega katika kupata elimu, kufanya biashara, kuwasiliana na kujifunza stadi mbalimbali za maisha, hivyo basi; Serikali kupitia wizara husika inaweza kutumia nafasi hii kuelimisha jamii kwa ujumla(watu wazima na watoto) madhara, namna ya kukabiliana na kupinga ukatili wa kijinsia kwa watoto.
๐๐๐ฎ๐ป๐๐ถ๐๐ต๐ฎ ๐๐ฒ๐น๐ฒ๐๐ถ๐๐ต๐ฒ๐ป๐ถ(๐ง๐) ๐ป๐ฎ ๐ฟ๐ฒ๐ฑ๐ถ๐ผ ๐๐ถ๐ป๐ฎ๐๐ผ๐๐ผ๐ฎ ๐ฒ๐น๐ถ๐บ๐ ๐ธ๐๐ต๐๐๐ ๐๐ธ๐ฎ๐๐ถ๐น๐ถ ๐ธ๐๐ฎ ๐๐ท๐๐บ๐น๐ฎ; Hii inaweza kushangaza kidogo kutokana na mawazo yangu lakini naamini hii pia inaweza kuwa mojawapo ya njia zitakazosaidia kupunguza tatizo la ukatili wa kijinsia katika jamii. Hii ina maana kwamba, wanaharakati wa kutetea haki za binadamu, wanasaikolojia na wataalamu mbalimbali watatumia jukwaa hili kuelimisha jamii kuhusu kutambua, kujilinda na kuripoti aina za ukatili wa kijinsia. Waandishi wa habari wataibua aina mbalimbali za ukatili hasa kwa wazee, wanawake, walemavu, wanaume, watoto na jamii kwa ujumla na kuonesha mustakabali na hatua zilizochukuliwa kwenye matukio husika. Hii yote inapaswa kufanywa na serikali kupitia wizara husika kwa kushirikiana na mashirika mbalimbali ya Umma, haki za binadamu ya kitaifa na kimataifa na jamii kwa ujumla. Ni kama ilivyo sasa tunavyotumia ๐ฆ๐ฎ๐ณ๐ฎ๐ฟ๐ถ ๐ง๐ kueneza utalii wetu wa ndani ya nchi na kuvutia watalii wengi zaidi ndani na nje ya nchi.
Yote kwa yote, ukatili wa aina yoyote haupaswi kupewa nafasi kwa namna yoyote ile katika jamii. Ni vyema jamii ikaelimishwa zaidi na zaidi kuhusu ukatili wa kijinsia kwa kutumia kila mbinu.
Ukatili wa kijinsia hasa kwa watoto ni adui kama adui wengine i.e ujinga na umasikini. Ni kama tupo vitani, yatupasa kutumia medani zote za kivita ili kupambana na adui yetu ambaye ni ukatili wa kijinsia kwa watoto ili tuwe na Taifa lililo salama zaidi.
Wako;
Pmanga

Upvote
2