Asilimia kubwa ya hawa watu kwanza ni watu wazima inaweza umri wao ni kuanzia miaka arobaini au kuanzia miaka hamsini kuendelea,
Tangu yatokee mauaji ya maelfu ya watanzania kuanzia Octoba 29 na kupendelea nimeona ID za platinum member nyingi zikitoa michango hapa JF kuliko wakati wowote ule tangu nimeanza kutumia JF,
Nimejua kwamba hawa watu wengi wao walijiunga JF miaka mingi iliyopita na wanauzoefu mkubwa na hili jukwaa la JF na inawezekana wengi wao wapo nje ya nchi.
Kwa hayo machache ni kwamba hawa jamaa wanauzalendo wa Hali ya juu na nchi hii sababu wamekua wakitoa michango chanya kupinga na kulaani mauaji ya maelfu ya watanzania na mengineo mengi maovu yaliyofanywa na utawala haramu uliopo Sasa nchini.
Najua watanzania sote kwa pamoja tumeungana kulaani na kupinga kwa dhati mauaji yaliyofanyika kwa ndugu zetu dhidi ya utawala huu haramu uliopo unaoongozwa na samia ila na hizi jitihada zisiishe bali tuendelee kupinga hayo maovu kwa kadiri ya akili na nguvu zetu zote ila kwa Leo niliona niwape pongezi zao Platinum member tulionao hapa JF.
Wachache ninaowakumbuka ni kama
Kiranga
Nyani Ngabu
Mshana Jr
Mzee Mwanakijiji
Salary Slip
Na Platinum Member wengineo ambao sijawataja hakika mnastahili pongezi kwa uzalendo wenu wa Hali ya juu, ninyi ni tunu ya JF na Tanzania kwa ujumla tuendelee kuwapambania watanzania.
Mapambano yanaendelea