Statesmann,
Hii ni fikra nzuri sana lakini inahitaji umakini mkubwa sana.
Mathalan umewataja
Abdul na
Ally Sykes na hii nadhani katika kategori ya
wanasiasa.
Umemsahau baba yao
Kleist Sykes.
Kleist Sykes anao wenzake waliofanya makubwa katika wakati wao kama
Martin Kayamba, Erika Fiah kwa kuwataja wachache.
Hapo hapo ikiwa utawataja
Abdul, Ally na
Nyerere lazima umtaje na
Hamza
Mwapachu.
Hamza Kibwana Mwapachu
Umemtaja mwanamuziki
Diamond,,,
Itabidi uwataje wanamuziki ''pioneers,'' kama
Frank Humplink,
Salum Abdallah,
Ahmed Kipande, Mbaraka Mwinshehe, na wengine...
View attachment 1170795
Salum Abdallah na Cuban Marimba Cha Cha Band
Hii si kazi nyepesi itahitaji umakini wa hali ya juu sana.