Tuwataje "100 Greatest Tanzanian of all time"

Tuwataje "100 Greatest Tanzanian of all time"

Mimi nawaandika wafuatao:

1. Abushiri bin Salim el Harthi - huyu aliwapa tabu sana wakoloni wa Kijerumani walipokuja kuitawala nchi yetu

2. Hassan bin Omar Makunganya - alitoa upinzani mkali dhidi ya watawala dhalimu wa Kijerumani

3. Selemani Mambi - Chifu wa Wamwera aliyekuwa mwiba kwa Wajerumani. Huyu ndiye alimchoma mkuki yule Askofu Cassian Spiss aliyekuwa anajidai anaeneza dini kumbe anasaidia harakati za ukoloni

4. Chifu Mkwawa - Habari zake zinajulikana

5. Martin Kayamba - Huyu ni mwanaharakati ambaye ni madhulumu wa historia. Wakati sifa zote nchi hii akilundikiwa Nyerere kama yeye ni malaika, watu muhimu kama hawa wamesahauliwa. Mnamo mwaka 1919 miaka mitatu kabla Nyerere kuzaliwa kidume hiki kilianzisha chama cha kutetea maslahi ya watumishi wa umma wa Tanganyika (Tanganyika Territory African Civil Servants Association)

6. Sykes family
 
Umemsahau Ali Kiba, msanii wa kwanza kuimba na nguli wa dunia R. Kelly.
 
Kisiasa, tungeanza na orodha ile ya watu 17 waliosimama mstari wa mbele wa uhuru kisha tutaendelea na wengine.
Kwenye michezo muongeze Abdallah King Kibaden.

Huyu aliongoza Simba kama mchezaji kuifikisha nusu fainali mabingwa Afrika 1975, kisha akaiongoza tena Simba kufika fainali Kombe la CAF kama kocha.(Hakuna kocha mwingine aliyepata mafanikio kama hayo mpaka sasa)
Watetezi wa haki za binadamu, wahifadhi wa mazingira, watetezi wa demokrasia, wazalendo waliohatarisha maisha yao kupigania taifa hili akiwemo captain Mazula.

Lakini muorodheshe mtu aliyebuni mwenge wa uhuru. Ingawa hatukubalini nao lakini kitendo cha mwenge huo kuishi miaka 58 si jambo dogo.

Weka jina la Forojo Ganze, maana ubunifu wake ungalipo.
 
John Bocco mchezaji pekee aliefikisha magoli zaidi ya 100 ligi kuu Tz ,Hamorapa na baharia aliechomoa betri Morogoro
 
Marijani Rajabu
Joseph Haule
LADY JAYDEE
NAUYE
LISU
Suleiman NYAMBUI
Edward Lowasa
John Mongella
Juma Kaseja
IGP Sarakikya
Samuel sita
Pius Msekwa
Freeman Mbowe
Msuguli
 
DR REMMY  ONGALA.jpg
MARIJANI RAJABU.jpg
Dkt. Remmy Ongala na Mqrijani Rajab.
 
Laston Nazareth Mwaipopo aliyetengeneza mchanganyiko wa bia aina ya SAFARI LAGA 1977 na kuipa Breweries Tuzo mbali mbali za Kimataifa
 
Ina maana hiyo list haitambui 'wanaharakati huru'..! Mbona Musiba sijui Msuba simuoni?!
 
Laston Nazareth Mwaipopo aliyetengeneza mchanganyiko wa bia aina ya SAFARI LAGA 1977 na kuipa Breweries Tuzo mbali mbali za Kimataifa
Duh, Asante Sana mkuu kwa taarifa hii, huyo jamaa anastahili kuwemo ndani ya top 5
 
Statesmann,
Hii ni fikra nzuri sana lakini inahitaji umakini mkubwa sana.

Mathalan umewataja Abdul na Ally Sykes na hii nadhani katika kategori ya
wanasiasa.

Umemsahau baba yao Kleist Sykes.

Kleist Sykes anao wenzake waliofanya makubwa katika wakati wao kama
Martin Kayamba, Erika Fiah kwa kuwataja wachache.

Hapo hapo ikiwa utawataja Abdul, Ally na Nyerere lazima umtaje na Hamza
Mwapachu.

View attachment 1170796


Hamza Kibwana Mwapachu

Umemtaja mwanamuziki Diamond,,,

Itabidi uwataje wanamuziki ''pioneers,'' kama Frank Humplink, Salum Abdallah,
Ahmed Kipande, Mbaraka Mwinshehe, na wengine...

View attachment 1170795

Salum Abdallah na Cuban Marimba Cha Cha Band

Hii si kazi nyepesi itahitaji umakini wa hali ya juu sana.
Naunga mkono hoja.
 
Back
Top Bottom