Tuwataje Madereva wa Mabasi wanaobet kwa kuendesha magari ovyo ili wawahi kufika Stendi wapewe 100,000

Tuwataje Madereva wa Mabasi wanaobet kwa kuendesha magari ovyo ili wawahi kufika Stendi wapewe 100,000

Na declare interest mimi ni mdau wa usafirishaji Tanzania.

Lengo la kuanzisha huu uzi sio kuharibu biashara au maisha/ajira za watu ila ni kuokoa maisha ya watanzania wanaokufa kila siku kama panzi kwa uzembe na ujinga wa hawa madereva.

Mimi ni mkazi wa Mkoa wa Mbeya na huwa nafanya kazi za usafirishaji na mara nyingi huwa nakuwa barabarani na muda mwingine huwa pale Uyole stendi, Nane nane stendi au kule Ipogolo Iringa na Msamvu stendi pale Morogoro.

Kumekuwa na tabia ya ushabiki wa wapiga debe kwenye hizi stendi zetu kuhusu nani anakua wa kwanza kufika akitokea sehemu gani. Mfano kwa mabasi ya Dar-Mbeya pale Uyole kumekuwa na ushabiki huo. Mara nyingi vijana hawa wapiga Debe humu katika hizi stend zetu huwa na "team" na hujichangisha pesa na kufikia kiwango fulani mfano Tsh 200,000/= au 300,000/= hivyo hukubaliana. Gari litakalo wahi kufika dereva atapewa 100,000/= na hiyo nyingine 100,000/= au 200,000/= itapewa timu ya Gari iliyobet kuwa litawahi kufika stendi.

Kitendo hiki kipo kila stendi nchi hii na nimekishuhudia kwa macho yangu katika stendi za Uyole na nanenane Mbeya, Igumbilo Iringa, Msamvu Morogoro naBabati Manyara. Hali hii husababisha madereva kukimbiza na kukimbizana barabarani bila sababu yoyote. Wamekuwa wanafanya overtaking za hovyo bila kujali usalama wao na wa abiria zao.

Kuna siku nilisafiri toka Iringa naenda Mbeya na nilikuwa kwenye gari binafsi, tulipitwa na Newforce na nyuma yake ikaja Sauli. Walikuwa wana kimbizana. Sauli akitaka kumpita Newforce, Newforce hampi nafasi ya kupita na kama kuna gari linakuja mbele itabidi lile gari la mbele likae pembeni ili wao wapite. Hali hii ni mbaya sana na vyombo vya usalama vipo na vinaona.

Leo nimeletewa dokezo hili ili wewe mtanzania mwenye nia njema ukataji madereva wa mabasi wanaofanya huo ujinga kwa kuendesha rough ili kuwahi Beijing za kwenye mastend. Naamini vyombo vya usalama vipo humu na vitasaidia kuchukua hatua na kama hawatachukua hatua, damu za watanzania wenzetu zinazomwagika hukunwao wanafurahia kukusanya elfu 5 ziwe juu yao.

1. Mi naanza kumtaja yule dereva mwarabu mwembamba wa Kapricon Coach toka Mbeya kwenda Arusha.

2. Wengine ni madereva wote wa Sauli na newforce za Dar-Mbeya/Songwe.
Na Mabasi Yao Ili watu wasipande

Sauli
Newforce
 
Nakumbuka kuna siku nilitoka tunduma to dar kampuni kapuni yani siitaji kuna jamaa alikuwa anapita kuchangisha mchango wa buku mbili mbili kwaajiri ya faini za toch nazile ela akakabiziwa konda yani tunduma to dar tuliingia saa11 niliflai sana
Wapumbavu ndio wanaweza kutoa huo ujinga,hiyo inafanyika sana Magari ya Tunduma, kampuni ni hao hao Newforce/Golden Deer
 
Shida sio gari kukimbia ila ni kukimbia kwa kufuata sheria na taratibu za barabarani ili kulinda hali za abiria na watumiaji wengine wa barabara husika.
Taratibu za barabarani hasa magari ya Abiria speed ni max of 80km/hr
 
Nyie mnaosema gari zimeundwa zitembee..sio kwa barabara hizi zetu ambazo sio rafiki barabara ambazo mashimo yamejaa..barabara ambazo zinakatisha mifugo..watu n.k..barabara za wenzetu kama ni high way ni high way kweli kweli hapo speed hata km 240/h yani wote wanakimbia hukuti wakatiza miguu au wafanyabiashara pembeni...sasa huku mnataka hizo speed kwa ubora upi? Mtatuua
Na speed ni 80-100 tu.
Masaa 6 anakabidhi kwa mwingine aendelee
 
Kwakweli nilichogundua raia hawajali,yaani juzi nilipanda gari toka arusha kuja dar,gari inakula kona balaa abiria wakiulizwa na askari wanasema tumeridhika na mwendo,nikaona watanzania wao wanasubiri ajali itokee ndo waanze lawama wao kama wao hawawezi kuchukua hatua.


Sent from my HUAWEI MLA-AL10 using JamiiForums mobile app
 
Basi zinazoenda mbio zinaongeza kasi ya uchumi kukimbia

Ndio maana kuna hadi ndege.ziendazo kasi
Mabasi yanatakiwa kuwa ndege za barabarani kwa kukimbia watu wawahi waendeko.Basi la safari sio gari ya Bwana na bibi Harusi inayoenda taratibu

Binafsi sipendi kupanda basi lisilokimbia sana

Msafara wa Raisi wenyewe hukimbia mwendo wa kufa mtu kwa nini mabasi yakataliwe Basi anzeni kuzuia msafara wa Raisi usitimue mbio za kufa mtu
Wewe kweli kiazi. Sasa umeshasema msafara wa rais wao barabara inakua nyeupe. Hakuna kizuizi. Naona kujichosha kukujibu kwa maelezo mengi. Cha kukusaidia soma post ya Kalpana #12 ili usiwe unadhihirisha ujinga.
 
Shida sio gari kukimbia ila ni kukimbia kwa kufuata sheria na taratibu za barabarani ili kulinda hali za abiria na watumiaji wengine wa barabara husika.
Mtanzania ataona kibao 50km/h yeye anaona walioweka hivyo mataahira ila yeye ndio mwenye akili ataenda 180.
Baadaye akikatika miguu aanze kusumbua ndugu hawamuhudumii au akiitwa tumbili na mwarabu au mzungu anakasirika 😬.
 
Mtanzania ataona kibao 50km/h yeye anaona walioweka hivyo mataahira ila yeye ndio mwenye akili ataenda 180.
Baadaye akikatika miguu aanze kusumbua ndugu hawamuhudumii au akiitwa tumbili na mwarabu au mzungu anakasirika 😬.
wana shida ya umeme kichwani unaingia mdogo.
 
Basi zinazoenda mbio zinaongeza kasi ya uchumi kukimbia

Ndio maana kuna hadi ndege.ziendazo kasi
Mabasi yanatakiwa kuwa ndege za barabarani kwa kukimbia watu wawahi waendeko.Basi la safari sio gari ya Bwana na bibi Harusi inayoenda taratibu

Binafsi sipendi kupanda basi lisilokimbia sana

Msafara wa Raisi wenyewe hukimbia mwendo wa kufa mtu kwa nini mabasi yakataliwe Basi anzeni kuzuia msafara wa Raisi usitimue mbio za kufa mtu
Chawa huna akili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani zinapitiliza spidi zilizoandikwa kwenye gari? Gari ikiwa na spidi 240 maana yake rukusa kuzifikia

Hazikuweka kama mapambo.Ni kuwa ukijisikia zifikie tu Haina shida hasa ukiwa safari ndefu

Hongereni madereva wa Mbeya,Tukuyu ns Kyela

Tatizo wengi wanaopinga mwendo mkali.wanaishi Dar es salaam ambako kutwa gari ukiendesha mwisho spidi 50.sababu ya msongamano wa magari.

Wanaleta woman wao kwenye gari za safari ndefu

Madereva wa Mabasi endesheni mbio.muwezavyo watu wawahi waendako
Unajua Tanzania speed ni 80kmh juu ya hapo ni umevunja sheria tena hiyo ni maporini.. Mjini top speed ni 60kmph na mtaani ni 30kmph

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wacha majungu,gari zimetengenezwa zikimbie.Watu wawahi waendako.Mimi sipendi.gari liendalo taratibu nataka linalokimbia hasa
Ndomana zikitokeq ajali watu wakavuta,wakaibiwa Mali zao
Wakati imetokea ajali wala sinaga huruma

Ova
 
Unajua Tanzania speed ni 80kmh juu ya hapo ni umevunja sheria tena hiyo ni maporini.. Mjini top speed ni 60kmph na mtaani ni 30kmph

Sent using Jamii Forums mobile app
Km speed max ni 80kmh basi wabadilishe vibati vya mabasi visome mwisho 80-90 b4 imported.tofauti na hapo wao wako wrong.ni sawa useme matumizi yako ya siku ni laki alafu nikwambie usitumie zaidi ya elf 40 kwasiku.
 
Back
Top Bottom