Kuna upotoshaji mkubwa dhidi ya hoja za wanaoitisha kurejelewa kwa mchakato wa kupatikana kwa katiba mpya.
Mama wamemfanya kuamini kuwa hizo ni chokochoko.
Katiba ni haki ya raia. Kudai katiba mpya dhidi ya iliyopo yenye mapungufu hakuwezi kuwa ni chokochoko.
Hoja hupingwa kwa hoja.
Katiba bora haiwezi kupatikana kama hisani toka kwa watawala ambao ni wanufaika wa iliyopo na wenye vingi vya kupoteza kwa kuja kwa mpya.
Tuzifahamu tabia za wapotoshaji hawa, kwa maslahi ya mwendelezo wa kudai katiba mpya iliyoboreshwa kama jambo la haki:
1. Wengi wao ni wakereketwa wa awamu ile
2. Wengi wao ni wale wale waliokuwa wakimzunguka JPM na kutaka apewe mitano tena kinyume cha katiba
3. Wengi wao ndiyo hao hao wanaomzunguka mama leo
4. Ajenda yao kuu ni kuendeleza ya JPM bila kuwapo JPM
5. Ndiyo walio waasisi wa ile salamu yetu pendwa "kwa jina la JMT"
6. Ndiyo walio waasisi wa kuwa Samia = JPM
7. Misingi ya hoja zao ni ile ile ya JPM, rejea misimamo kuhusu Corona, Chanjo, na hata mahusiano ya kisiasa ndani ya nchi
8. Wote ni CCM
9. Nk
Hawa ndiyo waliotufikisha hapa kwenye chokochoko:
Kuwafahamu wanyoa viduku hawa kunatuweka katika hatua bora zaidi za kuyasimamia mahitajio yetu ya kupata katiba mpya sasa.