Tuwe makini na pombe, zinaua

Tuwe makini na pombe, zinaua

Karibun NIPA
 

Attachments

  • D491DE9C-78F3-449E-8A8C-1DABCABB597F.jpeg
    D491DE9C-78F3-449E-8A8C-1DABCABB597F.jpeg
    653.4 KB · Views: 3
Mimi swala la pombe zinazotengenezwa hazina viwango siliafiki sana,ninachojua mimi itakuwa ni unywaji wa hizi pombe kwa kupitiliza.Nilikaa vijijini kipindi flani watu wanakunywa gongo daily mpk usiku mnene ,lakini sikuwahi kusikia wana matatizo tunayopata huku mijini,tena nakumbuka kuna hata vizee unakuta kina miaka 70+ lakini pombe yake kuu ni gongo,sasa sijui hizi pombe za viwandani zina kitu gani cha ziada mpaka watu wanaumia hivi...
Gongo ya vijijini ni salama kuliko gongo hizi za kisasa. Gongo za kisasa nyingi zimeundwa na wahuni vichochoroni. Ukiona label ya Hennesy unajua bonge la gongo kumbe sumu.
 
Wasaalam, mnamo mwaka jana X Mass nilikunywa sana mpaka ikanipelekea kupata ulcers hivyo 25/12 na 1/1 ziinikuta kitandani naugumia maumivu nikajiapiza naachana na mipombe kali. Lakini nilivyopata nafuuu nikarudi tena.

Mwaka huu juzi 25/12 na 1/1 nazenyewe nimezilia kitandani the same case kama mwaka uliopita lakini nilipopata nafuuu nikaendelea tena.

Ila kilichonitisha juzi kati kaja balozi wa mtaa anachangisha rambirambi, nikatoa ila sikumuuliza chanzo cha kifo baadae niko kijiweni ndo washikaji wanasema huyu mtu alikufa kwa sababu ya pombe kali hawajamalizia hiyo story napewa taarifa mshikaji kuna mwingine tena huyu nimewahi kunywa nae mtaani kwangu kwa zamani naambiwa na yeye amekata moto kwa sababu ya vikali. Wakuu nimeogopa yaani bapa lote nilokunywa lilikata.

Kwa moyo wa dhati mi nimeamua kupunguza hii mikali japo bia siziwezi ila napunguza hii mikali taifa bado linanitegemea.

Na nyie nawaasa kama unapenda mikali hakikisha unakula vizuri japo hata huyo aliyekata moto alikuwa vizuri kiuchumi na hela ya kula hawezi kosa lakini ndo hivyo tena.
Taifa halikutegemei, bali wewe ndiye unayelitegemea.

Kiuhalisia wanaokutegemea wewe ni wale wanaopata riziki kutoka kwako, yaani mkeo, watoto ima wazazi wako.

Maneno hayo ya kutegemewa na taifa, tukiwa vijana yalitutia viburi vya kijinga sana.

Lakini kiuhalisia taifa ndiyo tunalolitegemea, sababu ukifa ama kufukuzwa kazi hata leo, taifa haliwezi kujua kuwa lina msiba ama limepungukiwa na kitu.
 
Jamaa yangu alitapika damu kwenda hospital ni vidonda vikali vya tumbo!
Akaapa kwamba anacha pombe kali😂😂😂 ndo kaongeza mwendo...

Chakula anakula kwenye vibakuli!!

Dokta jirani tumemsafirisha mwezi uliopita kwenda huko Kanda ya kati,pombe kali ilimtoa uhai. Kaacha watoto na mjane mnono sana
...'Mjane mnono sana'.
 
Taifa halikutegemei, bali wewe ndiye unayelitegemea.

Kiuhalisia wanaokutegemea wewe ni wale wanaopata riziki kutoka kwako, yaani mkeo, watoto ima wazazi wako.

Maneno hayo ya kutegemewa na taifa, tukiwa vijana yalitutia viburi vya kijinga sana.

Lakini kiuhalisia taifa ndiyo tunalolitegemea, sababu ukifa ama kufukuzwa kazi hata leo, taifa haliwezi kujua kuwa lina msiba ama limepungukiwa na kitu.
Mkuu ninaposema hivyo simaanishi bila mimi Taifa halisongi bali linaweza kunitumia katika nyanja tofauti
by the way upo sahihi ulichosema
 
Back
Top Bottom