Tuwe makini na yanayoendelea nchini, Viongozi wasio waaminifu wameamua kujichotea fedha za walipa Kodi watakavyo

Joined
Jan 9, 2026
Posts
40
Reaction score
196
Katika ulimwengu wa ukaguzi wa hesabu forensic auditing na intelijensia ya jinai (criminal intelligence) miradi mikubwa inayohusisha wageni mashuhuri kama Wasanii na wanamichezo, matukio ya kimataifa au kampeni kubwa za kuitangaza nchi inaweza kutumika kama kichaka au mbinu ya kutakatisha fedha (money laundering) au kufanya ufisadi iwapo hakuna mifumo madhubuti ya udhibiti.

Zifuatazo ni mbinu ambazo kiintelijensia hutumiwa na viongozi wasio waaminifu kutakatisha fedha kupitia matukio kama haya

1. Kukuza Gharama za Uendeshaji (Over-invoicing)​

Hii ni mbinu ya kawaida sana. Bajeti ya ujio wa mtu mashuhuri mfano Rio Ferdinand au mradi wa wizara inaweza kuongezwa kwa makusudi. Kwa mfano kama gharama halisi ya kumlipa na kumsafirisha mtu ni $100,000 bajeti inaweza kuandikwa kuwa ni $500,000. Hizo fedha za ziada zinazotoka serikalini huingia kwenye shell companies au mawakala ambao baada ya makato fulani, wanazirudisha kwa viongozi hao kama fedha halali.

2. Matumizi ya Makampuni Kivuli (shell companies and Proxies)​

Ili kuficha ukweli wa nani anafaidika na malipo ya serikali viongozi wahuni wanaweza kuanzisha makampuni ya udalali usafirishaji au ulinzi chini ya majina ya ndugu, marafiki, au washirika wa siri. Fedha za walipa kodi zinasafishwa kwa kulipwa kwenye makampuni hayo kwa kigezo cha kutoa huduma wakati wa ziara, na hivyo kuonekana zimepatikana kihalali.

3. Matumizi ya Fedha Taslimu (Cash Transactions)​

Matukio makubwa ya burudani na michezo mara nyingi yanahusisha mzunguko mkubwa wa fedha taslimu (viingilio, manunuzi ya papo kwa papo, n.k.). Hapa ni rahisi kuchanganya fedha zilizopatikana kwa njia haramu (kama rushwa au biashara haramu) na mapato halisi ya tukio, kisha kuziingiza kwenye mfumo wa benki kama mapato ya mradi au tamasha

4. Diplomatic or Cultural Cover​

Wakati mwingine, shughuli za kidiplomasia, kitamaduni, au kimichezo hutumiwa kama pazia la kuzuia vyombo vya uchunguzi (kama TAKUKURU au FIU) kuhoji matumizi kwa haraka, kwa kuhofia kuleta picha mbaya ya kidiplomasia au kisiasa. Hilo linatoa mwanya kwa walio ndani ya mfumo kusogeza fedha bila kukaguliwa mapema.

Jukumu la Idara za Usalama na Kiintelijensia​

Hapa ndipo umuhimu wa Intelijensia ya Kifedha (Financial Intelligence) na vyombo vya usalama unapokuja. Kazi ya maafisa wa intelijensia na wachunguzi ni
  • Kufanya Due Diligence (uchunguzi wa kina) wa mikataba yote inayofanywa kati ya wizara na mawakala wa nje
  • Kufuatilia mzunguko wa fedha (Follow the Money) ili kuona kama kuna akaunti za viongozi au watu wao wa karibu zinazopokea fedha baada ya malipo makubwa kufanyika.
  • Kuhakikisha kuwa Diplomasia ya Michezo inaleta tija halisi kwa taifa na sio kuwa mradi wa watu binafsi kujitajirisha.
Ni mtazamo sahihi wa kiintelijensia kuwa na mashaka na kila mradi mkubwa (professional skepticism) kila mzunguko wa fedha za umma unapaswa kutazamwa kwa jicho la tatu ili kulinda rasilimali za nchi
 
FIU wamchunguze makonda....au wakiona shaka wawajulishe EGMONT
 
Kwa ile riport ya CAG unajua kabisa ngariba ndo diwani wa kata...

Ngumu sana ukeketaji kukoma katani
 
ok 🐒
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…