Tuwe makini, nahisi hii mitandao ya simu haina ulinzi wa uhakika

Tuwe makini, nahisi hii mitandao ya simu haina ulinzi wa uhakika

Napata meseji nyingi za utapeli kutoka kwenye namba za mtandao wa TTCL, sijajua shida ni nini, wameshindwa kuwadhibiti hao matapeli?! Mbona mitandao mingine imeweza.
 
Iko hivi, wazee wa tuma namba hii wanatuma msg kama 1000 randomly ina ujumbe mmoja mfano MWANANGU HIO HELA NITUMIE KWENYE NAMBA HII. Katika hizo msg 1000 hawezi kukosa moja ambayovitashabihiana na ujumbe huo. Bajati mbaya huyo mmoja katika 1000 unakuwa wewe.
 
Iko hivi, siku za nyuma kama wiki tatu zilizopita nilikuwa naongea na mama kweny simu, tulikuwa tunaongea kuhusu maswala ya kutumiana pesa, nikwambia ntamtumia muda si mrefu tukimaliza kuongea, cha kushangaza baada ya kukata tuu simu, kuna message ikaingia ya namba nyingine ngeni inasema "mwanangu tuma kweny hii namba 07xx xxx xxx".
Nikashtuka kidogo ila kwa kuwa najua mambo ya utapeli wa mitandao nikakausha.
Ila kilichonishangaza, kwann ile message mtu aliyetuma imeandika "mwanang" just momentarily baada ya kuongea na mama, muda uliotumwa hio message pamoja na context za hio message zilinishtua.

Nilimpigia simu mama akasema sio yeye, nikapotezea nikawaza maybe it's just a coincidence.

Second scenario, imetokea wiki iliyopita, nilikuwa naongea na demu flani ivi kweny simu, nayeye hivohivo tulikuwa tunaongea maswala ya kutumiana pesa. Cha kushangaza baada ya kuongea nae nilivokata simu tuu baada ya kama dakika moja ikaingia message "Tuma kweny namba 07xx xxxx xxx".

Nilivompigia akasema sio yeye na hajawahi miliki hio namba.
Nikawaza kuhusu precession ya ile message, mbona imetumwa muda muafaka kabisa, ila nikapotezea pia.

Leo imetokea tena, huyuhuyu demu amenicheki sema this time hatujaongea, tumetumiana tuu message nikamwambia sawa nakutumia.
From tulivoongea saa 12 jioni, saa 12 unusu message mbili zikaingia namba ngeni, ya kwanza "Ntumie basi hio hela" ya pili "tuma humu 07xx xxx xxx", kumuuliza anasema sio yeye.

Hii ya leo imenifikirisha sana na ndio imenifanya nikumbuke scenario za nyuma, kwann hizi message zinaingia just after kuongea na watu kuhusu kutumiana pesa, wanajuaje? Or is it just a coincidence??

Mi nadhani hii mitandao haina ulinzi, haina privacy kabisa, na nahisi kuna watu huwa wanatusikiliza na kusoma message zetu, this can't be a simple coincidence.

Sitautaja mtandao ninao tumia ila nina mpango wa kuuhama.

Nyie wenzangu vipi hamjawahi kutana na haya mambo??
Halotel
 
Back
Top Bottom