Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndiyo wataje hadi bei ya Lita 5 nazotaka kuagiza? Wamejuaje kama na shida na Lita tano? Halafu muda huo huo nimetoka kumaliza mazungumzo ya kuuziwa Lita tano. Hapana nasisitiza Kuna kitu hakipo Sawa.Coincidence tu. Matapeli wanarusha sms kila mara, ilitokea wamerusha sms ukiwa umemaliza maongezi na mama yako.
Probably hii ni halotelIko hivi, siku za nyuma kama wiki tatu zilizopita nilikuwa naongea na mama kweny simu, tulikuwa tunaongea kuhusu maswala ya kutumiana pesa, nikwambia ntamtumia muda si mrefu tukimaliza kuongea, cha kushangaza baada ya kukata tuu simu, kuna message ikaingia ya namba nyingine ngeni inasema "mwanangu tuma kweny hii namba 07xx xxx xxx".
Nikashtuka kidogo ila kwa kuwa najua mambo ya utapeli wa mitandao nikakausha.
Ila kilichonishangaza, kwann ile message mtu aliyetuma imeandika "mwanang" just momentarily baada ya kuongea na mama, muda uliotumwa hio message pamoja na context za hio message zilinishtua.
Nilimpigia simu mama akasema sio yeye, nikapotezea nikawaza maybe it's just a coincidence.
Second scenario, imetokea wiki iliyopita, nilikuwa naongea na demu flani ivi kweny simu, nayeye hivohivo tulikuwa tunaongea maswala ya kutumiana pesa. Cha kushangaza baada ya kuongea nae nilivokata simu tuu baada ya kama dakika moja ikaingia message "Tuma kweny namba 07xx xxxx xxx".
Nilivompigia akasema sio yeye na hajawahi miliki hio namba.
Nikawaza kuhusu precession ya ile message, mbona imetumwa muda muafaka kabisa, ila nikapotezea pia.
Leo imetokea tena, huyuhuyu demu amenicheki sema this time hatujaongea, tumetumiana tuu message nikamwambia sawa nakutumia.
From tulivoongea saa 12 jioni, saa 12 unusu message mbili zikaingia namba ngeni, ya kwanza "Ntumie basi hio hela" ya pili "tuma humu 07xx xxx xxx", kumuuliza anasema sio yeye.
Hii ya leo imenifikirisha sana na ndio imenifanya nikumbuke scenario za nyuma, kwann hizi message zinaingia just after kuongea na watu kuhusu kutumiana pesa, wanajuaje? Or is it just a coincidence??
Mi nadhani hii mitandao haina ulinzi, haina privacy kabisa, na nahisi kuna watu huwa wanatusikiliza na kusoma message zetu, this can't be a simple coincidence.
Sitautaja mtandao ninao tumia ila nina mpango wa kuuhama.
Nyie wenzangu vipi hamjawahi kutana na haya mambo??
Tumshukuru mama kwa hiloAwamu ya 6 imetusabidhia wezi mitandao hajawahi tokea.
Ni mitandao yote inafanyiwa surveillance kwa hio labda uanzishe mtandao wako mwenyewe yaan mitandao yote ipo chini ya uangalizi na Namba zote zilizosajiriwa kwa wale mabwana zinafuatiliwa hata upige chafya wanajua, kwa hio wanaofanya hivyo ni kule kule kwa wale mabwana Ila ukiwaambia km kawaida watasema sio waoSitautaja mtandao ninao tumia ila nina mpango wa kuuhama.
Acha uongo wizi upo kitamboAwamu ya 6 imetusabidhia wezi mitandao hajawahi tokea.
Msiwapake matope mitandaoni ya simu,Natamani kusema kwamba wafanyakazi wa huko mitandaoni wanashirikiana na matapeli
Inawezekana kabisa, lakini vipi kwa mtu anayekutumia ujumbe mahususi kabisa na mazungumzo yako uliyetoka kuzungumza kupitia simu.?Msiwapake matope mitandaoni ya simu,
Hawa jamaa matapeli wanachofanya ni kubet tu na kubahatisha namba tofauti tofauti..
Hivi mfano mtu akiandika sms kwa watu 200 "POLE SN KWA MSIMBA" ikaenda kwa watu 200 itakosa watu waliofiwa?
Una akili mkuuMsiwapake matope mitandaoni ya simu,
Hawa jamaa matapeli wanachofanya ni kubet tu na kubahatisha namba tofauti tofauti..
Hivi mfano mtu akiandika sms kwa watu 200 "POLE SN KWA MSIMBA" ikaenda kwa watu 200 itakosa watu waliofiwa?
Kweli hela inatafutwa kwa nguvuHuku ndiko tulikofikia
Mimi Kuna mtu nilimtumia hela yaani namba ni yenyewe na jina lake ni lenyewe ila nilivyobonyeza OK meseji ikaingia kwenye Simu yangu " Umetuma kiasi cha shilingi 100,000/= kwenda kwa Mama Samia..." Nilidata sana....Mbonaa tutakomaa mpk CCM watoke madarakani😔😔maaana n wizi wa wazi wazi kbs huu
Msela kakujengea au sioMimi nilitumiwa ujumbe akidai yeye ni mwenye nyumba,ananiambia nilipe kodi wakati siishi sehemu inayolipia kodi
Wezi wapo kila mahali
ccm wanachukua hela zao za uwanachama. si hamtaki kuwa wanachama muichangie ada za uanachama. wamebinu mbwinu na kampuni za simu 😸Kuna kitu hakiko sawa coz mimi juzi nimeongea na sister maswala ya pesa sasa wakati najiandaa kutuma ghafla ikaingia msg tuma kwa namba hii ikabidi nishtuke na nilivyompigia akasema sio yeye.
Kuna kauchunguzi inabidi tukafanye hapa ila nnauhakika Kuna kitu hakiko sawa, thou sijajua ni kwa namna gani wanafanya hizi trick.
Shukran mkuuUna akili mkuu
Unajuwa kama unaweza ukarecodiwa hata na unayefanya nae mazzungumzo?Inawezekana kabisa, lakini vipi kwa mtu anayekutumia ujumbe mahususi kabisa na mazungumzo yako uliyetoka kuzungumza kupitia simu.?
Bado hujanijibu swali langu, nimetoka kuzungumzia ununuzi wa pikipiki Kisha nakata simu halafu Napokea ujumbe unaohusiana na pikipiki muda huo huo. Najaribu kumrudia hewani muuzaji anasema hajatuma ujumbe wowote Kwangu na makubaliano yetu ni kama awali.Unajuwa kama unaweza ukarecodiwa hata na unayefanya nae mazzungumzo?
Kwani zile connection za video za sex za watu wakiwa falagha zinavuja vp?pia kuna watu wa usalama pia wapo kazini.
Unapaswa uwe na tahadhari kwa kila jambo mkuu.
Niamini mimi mkuu hawa jamaa wana bet namba na ujumbe muhimu ambao ktk watu 50 lazima atapatikana mmoja.
Jiulize mfano wewe kwa siku umeahidi watu wangapi kuwatumia pesa?
Halafu uone sms inasema ile pesa weka huku huweziingia kwenye mfumo? Ukapigwa pesa?
Hizi sms mwanzo watu wamepigwa sn.