Tuwe objective: Mbowe ana sababu gani za kuendelea kuwa mwenyekiti wa CHADEMA

Tuwe objective: Mbowe ana sababu gani za kuendelea kuwa mwenyekiti wa CHADEMA

Jana nimemsikia Mh. Lissu mwanzo mpaka mwisho
Nikiri kuwa sijasikia kama Freeman atagombea.
Nafahamu kwamba kwa heshima yake kama angekuwa hagombei anawaachia "vijana" basi angeshatoa taarifa mapema kidogo.
Kwa hiyo anaweza kugombea

Sasa nimekuwa najiuliza kama Mbowe ataamua kugombea uenyekiti atakuwa na sababu gani za kuamua kuendelea kuwa mwenyekiti kwa zaidi ya miaka 20.

Declaration of Interest
Namuunga mkono Lissu kuwa Mwenyekiti kwa sababu nzuri alizozitaja jana

View: https://x.com/Ntobi_/status/1867809110693179758?t=JY_wVN5r5LQwmiy57z1GKg&s=19
 
Common sense ipi hapo?
Ya kulinganisha Nyakati za nchi imetoka kupata uhuru na huu wakati wa sasa.
Ni kama Lissu alifilisi hii hoja. Alisema kabla hivi hoja ilikuwa sahihi kwa sababu ya uchanga wa chama. Lakini sasa kuna Chadema kila mahali, huwezi kuona wewe pekee ndio unafaa.

BTW weka sababu za Mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti kwa zaidi ya 20yrs. Atakuwa na nini kipya ambacho hajakifanya
 
Kukubalika na wanachadema
 
..mabadiliko gani ataleta Lisu, mifumo iliyomyima haki zake ni ile ile inapambana na chadema, mabadiliko aliyoahidi TLS alipochaguliwa kuwq Rais wa TLS alitimiza?
Jukwaa la Uwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani ni tofauti na jukwaa la TLS lenye wanachama wasiozidi hata 2000!.
Mwenyekiti wa CHADEMA ni mtu mwenye ushawishi kote nchini na nje ya nchi (kupitia balozi zilizoko nchini).
 
..kwa hiyo uongozi ni ushawishi peke yake? kichaa akisoma udaktari na umefika hospitali na case ya kufanyiwa surgery..utakubali akufanyie upasuaji..? Mwalimu alipokubali mfumo wa vyama vingi uanze, wangapi walisema uanze na wangapi walisema usianze..
Usipumbazwe na idadi angalia mantiki/substance ya jambo!
 
Jana nimemsikia Mh. Lissu mwanzo mpaka mwisho
Nikiri kuwa sijasikia kama Freeman atagombea.
Nafahamu kwamba kwa heshima yake kama angekuwa hagombei anawaachia "vijana" basi angeshatoa taarifa mapema kidogo.
Kwa hiyo anaweza kugombea

Sasa nimekuwa najiuliza kama Mbowe ataamua kugombea uenyekiti atakuwa na sababu gani za kuamua kuendelea kuwa mwenyekiti kwa zaidi ya miaka 20.

Declaration of Interest
Namuunga mkono Lissu kuwa Mwenyekiti kwa sababu nzuri alizozitaja jana
Lissu VS Mbowe
Wenje VS Heche????
 
Masikio ya mbuzi hayasikii mpaka yachemshwe ndo yanasikia. Mbowe akae pembeni hasiwe kama masikio ya mbuzi, mbona ccm mwenyekiti anaachia ngazi baada ya miaka 10. Hata huko nje wanapishana baada ya muda fulani.
 
Anaweza akawa hana sababu ila kiukweli Mbowe ana kalba ya uongozi na sio mtu wa mihemko sana.
 
Hoja ya kuwaachia "vijana" ni hoja dhaifu.Mbowe ana miaka 63 na Lissu ana miaka 56.Hakuna kijana hapo kuna wazee wawili waliopishana umri kidogo.
 
Sifa alizotaja Lissu jana..ni sifa gani hakuwa nayo wakati Mbowe anagombea uenyekiti mara ya kwanza? Km vile viungo vya mwili vinavyohitajiana na uongozi kwenye kundi ni hivyo hivyo, mkono hauwezi kufanya kazi za kichwa..Lissu hawezi kazi/majukumu ya kuwa Mwenyekiti..anaweza kuwa msaidizi..ukizitambua kazi za kichwa cha mnyama, hizo ndio sifa za Mbowe kuwa Mwenyekiti Chadema..tujifunze kujua vyama vina maelekezo ya waliobeba maono wakati kinaanzishwa vzr kuyazingatia kuliko jazba za ujana..kwa anayesoma vitabu pekee vyenye umri mrefu kupita vitabu vingine vyote..vina mifano ya kutahadhalisha jamii kufuata msimamo wa vijana au kusikiliza maneno yao..9 kati ya 10 yana mwelekeo wa uharibifu na si kujenga.
Kwa karne hii, kujadili eti kuna kiongozi ameshakaa kwenye madaraka kwa muda wa miaka 20 na bado anataka kuongeza iwe 25, ni aibu. Haya mambo yalikuwa yanafanyika miaka ya 1960 na 1970. Miaka ya sasa, binadamu tumeshastaarabika na tumetumia experince na kujua kuwa uongozi usipobadishwa mara kwa mara kunakuwa na disadvantages nyingi kuliko advantages.
 
Nadhani tungesubiri kidogo ili labda Kama Mbowe atatangaza kugombea ndio tuanze kujadili
Mwambie Mbowe aje atoe tamko, anatutesa sana sisi wapenzi wa chama chake. Aje atoe msimamo wake kieleweke na tusonge mbele, kukaa muda mrefu bila tamko lake, anatutesa kwa kweli.
 
Kwa karne hii, kujadili eti kuna kiongozi ameshakaa kwenye madaraka kwa muda wa miaka 20 na bado anataka kuongeza iwe 25, ni aibu. Haya mambo yalikuwa yanafanyika miaka ya 1960 na 1970. Miaka ya sasa, binadamu tumeshastaarabika na tumetumia experince na kujua kuwa uongozi usipobadishwa mara kwa mara kunakuwa na disadvantages nyingi kuliko advantages.
..suala si miaka mingi au michache, kwanza elewa mahitaji, pili pima utayari..aina ya watu mlivyo, rasilimali mlizo nazo, nguvu na mbinu za adui kuwaumiza na tatu pima umbali mliotembea na umbali mnahitaji kufika kule mnakwenda..! Mambo ya ukomo wa uongozi yanafanyika pale palipo na ulinganifu, vitu vingi viko sawa..ni kuonyesha ustaarabu wa jamii inayotaka kusonga mbele.
 
..watu wa aina hii ndio Lissu anashauriwa nao..
Screenshot_20241215_102412_YouTube.jpg
 
Hii ni hoja mufilisi kabisa, inashangaza kutolewa na watu kama hawa. Wanakosaje common sense za kutofautisha nyakati?

Hata Nyerere alisema wapambe ndio walikuwa wanashadadia aendelee kubaki ili wazidi kula. Kina Ntobi wasifanye tukawafikiria hivyo.

Lakini, sababu za Mbowe kuendelea kubaki ni Nyerere kukaa miaka 20+ madarakani?
Mzee ulimwengu amenajisi sifa yake kwa kuja na hoja mfu kama hii.
 
Hoja ya kuwaachia "vijana" ni hoja dhaifu.Mbowe ana miaka 63 na Lissu ana miaka 56.Hakuna kijana hapo kuna wazee wawili waliopishana umri kidogo.
Mkuu hata wewe umeshindwa kuelewa matumizi ya neno Vijana? Wala usilinganishe umri. Mbowe kama kaka mkuu itoshe sasa kwa sababu ameshatutendea kadri ya uwezo wake kwa muda mrefu.
 
Back
Top Bottom