Tuwe objective: Mbowe ana sababu gani za kuendelea kuwa mwenyekiti wa CHADEMA


View: https://x.com/Ntobi_/status/1867809110693179758?t=JY_wVN5r5LQwmiy57z1GKg&s=19
 
Common sense ipi hapo?
Ya kulinganisha Nyakati za nchi imetoka kupata uhuru na huu wakati wa sasa.
Ni kama Lissu alifilisi hii hoja. Alisema kabla hivi hoja ilikuwa sahihi kwa sababu ya uchanga wa chama. Lakini sasa kuna Chadema kila mahali, huwezi kuona wewe pekee ndio unafaa.

BTW weka sababu za Mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti kwa zaidi ya 20yrs. Atakuwa na nini kipya ambacho hajakifanya
 
Kukubalika na wanachadema
 
..mabadiliko gani ataleta Lisu, mifumo iliyomyima haki zake ni ile ile inapambana na chadema, mabadiliko aliyoahidi TLS alipochaguliwa kuwq Rais wa TLS alitimiza?
Jukwaa la Uwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani ni tofauti na jukwaa la TLS lenye wanachama wasiozidi hata 2000!.
Mwenyekiti wa CHADEMA ni mtu mwenye ushawishi kote nchini na nje ya nchi (kupitia balozi zilizoko nchini).
 
Jukwaa la Uwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani ni tofauti na jukwaa la TLS lenye wanachama wasiozidi hata 2000!.
Mwenyekiti wa CHADEMA ni mtu mwenye ushawishi kote nchini na nje ya nchi (kupitia balozi zilizoko nchini).
..kwa hiyo uongozi ni ushawishi peke yake? kichaa akisoma udaktari na umefika hospitali na case ya kufanyiwa surgery..utakubali akufanyie upasuaji..? Mwalimu alipokubali mfumo wa vyama vingi uanze, wangapi walisema uanze na wangapi walisema usianze..
Usipumbazwe na idadi angalia mantiki/substance ya jambo!
 
Lissu VS Mbowe
Wenje VS Heche????
 

Masikio ya mbuzi hayasikii mpaka yachemshwe ndo yanasikia. Mbowe akae pembeni hasiwe kama masikio ya mbuzi, mbona ccm mwenyekiti anaachia ngazi baada ya miaka 10. Hata huko nje wanapishana baada ya muda fulani.
 
Anaweza akawa hana sababu ila kiukweli Mbowe ana kalba ya uongozi na sio mtu wa mihemko sana.
 
Hoja ya kuwaachia "vijana" ni hoja dhaifu.Mbowe ana miaka 63 na Lissu ana miaka 56.Hakuna kijana hapo kuna wazee wawili waliopishana umri kidogo.
 
Kwa karne hii, kujadili eti kuna kiongozi ameshakaa kwenye madaraka kwa muda wa miaka 20 na bado anataka kuongeza iwe 25, ni aibu. Haya mambo yalikuwa yanafanyika miaka ya 1960 na 1970. Miaka ya sasa, binadamu tumeshastaarabika na tumetumia experince na kujua kuwa uongozi usipobadishwa mara kwa mara kunakuwa na disadvantages nyingi kuliko advantages.
 
Nadhani tungesubiri kidogo ili labda Kama Mbowe atatangaza kugombea ndio tuanze kujadili
Mwambie Mbowe aje atoe tamko, anatutesa sana sisi wapenzi wa chama chake. Aje atoe msimamo wake kieleweke na tusonge mbele, kukaa muda mrefu bila tamko lake, anatutesa kwa kweli.
 
..suala si miaka mingi au michache, kwanza elewa mahitaji, pili pima utayari..aina ya watu mlivyo, rasilimali mlizo nazo, nguvu na mbinu za adui kuwaumiza na tatu pima umbali mliotembea na umbali mnahitaji kufika kule mnakwenda..! Mambo ya ukomo wa uongozi yanafanyika pale palipo na ulinganifu, vitu vingi viko sawa..ni kuonyesha ustaarabu wa jamii inayotaka kusonga mbele.
 
Mzee ulimwengu amenajisi sifa yake kwa kuja na hoja mfu kama hii.
 
Hoja ya kuwaachia "vijana" ni hoja dhaifu.Mbowe ana miaka 63 na Lissu ana miaka 56.Hakuna kijana hapo kuna wazee wawili waliopishana umri kidogo.
Mkuu hata wewe umeshindwa kuelewa matumizi ya neno Vijana? Wala usilinganishe umri. Mbowe kama kaka mkuu itoshe sasa kwa sababu ameshatutendea kadri ya uwezo wake kwa muda mrefu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…