Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,583
- 27,838
- Thread starter
- #21
Hata kenya angalau kuna weusi wanazo hela. Lakini na wao ni yaleyale.
1. Hofu ya kupinduana.
2. Kuendeleza mali ya urithi.
3. Connection na watu wazito.
4. Kampuni zingine ni za vigogo ila hao wahindi/waarabu wapo kama pambo/cover/barakoa.
Nchi za kiafrika ambazo zilikuwa na waarabu/wahindi wachache zilipitia majanga ya kupinduana na vita za wenyewe kwa wenyewe.
Mfano fatilia historia ya.
1. Nigeria (walipinduana mno)
2. Ghana
3. Msumbiji (Frelimo vs Renamo)
4. Angola
5. Sudan ya kusini (Salva kiir vs Riek machar)
6. Rwanda
7. Congo DRC
8. CAR
9. Liberia
10. Sierra Leone
Zipo nyingi mno. Hofu ya kupinduana na vita imeleta haya mambo. Maana mtu akipata hela anawapa pesa maluteni kanali au mabrigedia au magenerali kisha wanapindua uongozi. Au wanaanzisha kikundi cha waasi ili kuingia madarakani.
Mfano nilifika Ghana, kule nako ni yale yale kuna Walebanoni ndiyo Wahindi wao, Uchumi wote uko chini ya Walebanoni, kusema kwamba Watanzania weusi ndiyo wanaomiliki Kampuni kubwa za Wahindi/ Waarabu kwa kujificha hilo sikubaliani nalo ila ninachojua wanakuwa na shea kidogo au hata wanapewa zawadi na Wahindi labda gari mpya au mtoto kusomeshwa nje halafu wanawapa Wahindi upendeleo.
Mfano akina Subash Patel ndivyo walivyotajirikia, lkn siyo kweli kwamba Waafrika weusi wanamiliki Kampuni za Wahindi ila wanatumiwa kuwapa Wahindi michongo ya Serikalini mfano Kiwanda kikibinafsishwa Wahindi wanaongea na wakubwa wanawapa zawadi wanapewa Kiwanda kwa bei ya kutupa, ...