Tuwe wakweli, ukiondoa Wahindi na Waarabu tunabakia na nini Tanzania?

Hoa watu wote wana international network, huwezi fikia kiwando chao kama uko local, lazima tuwe wa kimataifa zaidi.
 
Tunabaki na WACHINA (rafiki zetu wa damu)
 
Tafuta pesa,Mengi hakuwa Mhindi,
Laiser wa tanzanite sio muhindi,Diamond sio muhindi,Kusaga&Luge sio wahindi,
New africa hotel ni ya mbongo Tena hakufika hata la Saba,
Sahara media inayomiriki Star tv,sio ya Mhindi,
Acha fikra mfu,zichange akili,hakuna wa kukuonea huruma hapa duniani.
 
Hili swali nishawahi kumuuliza Babu yangu. Aliniambia chanzo ni Nyerere. Kwa kuwa Nyerere aliogopa kuwa weusi wakiwa na hela watampindua kijeshi. Kwa hiyo ni hofu ya kupinduliwa imesababisha yote. Mfano akina Kambona walipanga kumpindua.
Si kweli. Hii ni colonial legacy. Wakati wa ukoloni Asians walikuwa kisheria ndio wafanyabiashara. Popote alipotawala Muingereza hii ndio system. Waafrika ilikuwa ni wajakazi/watwana. Mfumo huu uliendelea baada ya uhuru, wahindi wakiwa na mizizi ya biashara na connection kwenye utawala. Sisi waswahili wazazi walihimiza usome kisha uajiriwe serikalini. Ingawa sasa hivi overtime social adjustment inatokea. Waafrika wanaovertake business community.
 
Bongo nyoso
 

Nafikiri labda haujaelewa maana ya hii Mada ungeuliza kwanza, sijasema kwamba hakuna matajiri weusi Tanzania, ila wachache na hawamiliki uchumi wa Tanzania kumbuka Wahindi Tanzania hawafiki laki 2 wakati sisi tuko zaidi ya milioni 45, kwa maana nyingine Wahindi tuseme labda kinadharia wakisimamimisha kila kitu hapa Tanzania tunakwenda chini kama nchi lkn Waafrika weusi matajiri uliowataja hata wakijitoa ghafla hakuna mtikisiko wowote utakaouona mkubwa, hivyo sijaandika hii Mada kwa lengo baya la kubeza weusi wenzangu wanaojituma na hongera kwao, bali ni uhalisia kwani tuko tegemezi kama watu weusi hata ndani ya nchi yetu wenyewe na hii ni karibia kwa kila kitu, ...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…