Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Anaandika, Robert Heriel
Kuhani
Kuna watu wanafikiri Taikon ni mtu mwenye roho mbaya, bandidu, bedui nisiye na huruma wala upendo. Ati kwa sababu ninaongea ukweli na haki. Ndugu zangu nipo hapa kuzungumza uhalisia wa mambo. Sio kwamba najitoa kwenye haya ninayoyazungumza. Mimi pia ni sehemu ya niyasemayo.
Kijana, mama, baba mwenye watoto, hakikisha unapofanya maisha yako unajiandaa kikamilifu na maisha yako ya uzeeni. Kila mmoja anafainali yake. Hakuna mtu popote duniani atakayekufikiria fainali yako. Utake usitake.
Maisha yako ni jukumu lako mwenyewe hasa unapokuwa mtu mzima. Asije akakudanganya mtu kuwa umezaa, ndugu yangu usije ku-bet kwa namna hiyo. Kwamba watoto watanisaidia. Utalia na kusaga meno.
Jiandae, jidhatiti, jipange, weka akiba ya kutosha kwa ajili ya uzee wako, ili uwe na uzee uliomwema.
Uzee mwema huchangiwa kwa kiasi kikubwa na mapambano ya ujanani. Usizubae, usiwe mzembe, tupambane.
Ndio maana serikali imeanzisha mifuko ya kijamii ya kuweka akiba za uzeeni. Kumaanisha ukiwa mzee hakuna mwenye jukumu la kukutunza isipokuwa nguvu zako mwenyewe za ujanani. Hakuna wa kumlaumu uzeeni zaidi ya kujilaumu wewe mwenyewe kwa nafasi za ujanani ulizozichezea.
Kisheria hakuna mwenye wajibu wa kukutunza wewe, sio duniani, mbinguni, akhera, wala mbugani. Sisemi watoto wasisaidie wazazi wao hapana, nazungumzia uhalisia wa maisha ya ulimwengu huu. Mtu mpaka akufikirie kukusaidia basi jua naye mambo yake angalau yanaridhisha.
Huwezi ku-bet kuwa Wwatoto wako watakusaidia wakati hujui watoto wako watakuwa na maisha gani. Sio ajabu unaweza ukazeeka na watoto wako wakawa bado wanahitaji msaada wako, wapo hapohapo nyumbani hawajui wapi waende, nini wafanye.
Mwishowe wanakuua ili warithi hata kile kidogo ulichokichuma au wanakuua kwa kukulaumu kuwa kwa nini uliwazaa. Ingawaje ni kosa kisheria matendo wayafanyayo.
Sisi kama vijana tunapaswa kuelewa kuwa, nguvu nyingi tulizonazo sio nguvu za bure za kuzichezea hovyo kwa kufanya starehe zisizo na kichwa wala miguu, sio nguvu za kuzitumia katika mambo ya kijinga na kipuuzi.
Nguvu tulizonazo ni kwaajili ya kujikimu maisha ya sasa na kuweka akiba kwa ajili ya maisha ya baadaye. Ni roho mbaya kutegemea watoto wadogo uliowazaa wakutunze kwa nguvu zao badala ya kukutunza kwa nguvu zako mwenyewe.
Weka akiba ya mashamba, weka akiba ya viwanja, weka akiba ya nyumba hata za matope. Jenga nyumba huko vijijini sio lazima ujenge mjini.
Wakati unazeeka unapotoa urithi kwa watoto, ule urithi moja ya kazi za urithi ni kukutunza wewe mzee wao. Mfano, unampa mtoto nyumba au shamba au mradi fulani, unamwambia, mwanangu au ninti yangu, mimi sasa nguvu zimepungua, ninakukabidhi shamba hili ulilime utalisha familia yako lakini pia utakuwa ukinipatia kidogo utakachochuma.
Au mwanangu nimekupa ng'ombe na mifugo hii ili uingalie, hali yangu unaiona, utatunza familia yako lakini pia utanitunza mimi baba yako au mama yako au utamuangalia na mdogo wako mdogo ambaye bado mambo yake hayajakaa vizuri.
Hiyo ndio maana ya mzazi, sio umgeuze mtoto wako kuwa mzazi wako wakati wewe ndiye uliyemzaa. Huo ni uhuni.
"Mwanangu au binti yangu, ujana wangu haukuwa na bahati njema, nilihangaika sana kuwatunza kama wajibu wa mzazi kwa mtoto, mpaka mkakua, nilijiwekea akiba yangu kwenye akaunti ya benki kiasi cha milioni 15 sio nyingi sana. Naomba ukazichukue utafute chochote cha kufanya ili unitunze mimi baba/mama yako, na uendeshe familia yako. Uniapie kwa Mungu wangu kuwa hautaitumia akiba yangu vibaya kwa mambo ya upuuzi bali utaizalisha, tena uniapie kuwa hautanidhulimu jasho langu mwanangu/binti yangu."
Hapo unakuwa na sababu na haki ya kutunzwa na mtoto kupitia jasho lako, sa sio vinginevyo. Sio useme, nimekuzaa sijui nimekulea, sijui nilikusomesha, hivyo lazima unilipe au unitunze. Huo ni uhuni, huo ni wajibu wako.
Labda useme hivi; Mwanangu, nilikuwa nawajibu wa kutunza na kukulea mara nilipokuzaa, nikakusomesha wote huo ni wajibu wangu ili kukufanya uwe na maisha bora, lakini sikuwa na wajibu wa kukutafutia kazi au biashara, suo sio wajibu wangu.
Ila nikakutafutia kazi kwenye kampuni fulani, nikahonga mpaka pesa ili uingiemo huko, ndipo ukapata hiyo kazi. Sasa nakuomba mwanangu, binti yangu, uniapie kwa Mungu wangu kuwa hautoniacha bila chochote kidogo ili unitunze mimi baba/mama yako kwa sababu nilitoa akiba yangu ya uzee ili upate kazi na unajua sio wajibu wangu kukutafutia kazi.
Haijalishi maisha yangu vipi yataenda, lakini ukweli huo uzingatiwe.
Nafahamu maisha kuna wakati wapo watu hupambana kila wawezavyo lakini hushindwa kuyaendesha maisha yao wala kujiwekea hata akiba ya uzeeni. Hao ni Exceptional cases.
Mambo muhimu kwa vijana;
i. Nasisitiza vijana tusikae hivihivi, tufanye kazi.
ii. Tuweke akiba hata kama ni kidogo.
iii. Tukipata laio mbili tatu tununue mashamba kama sehemu ya urithi wa kuwapa watoto wetu ili watumie urithi huo kututunza uzeeni.
iv. Tufanye mazoezi ili miili yetu iwe na afya njema nyakati za uzee.
V. Tule vyakula bora na tusitumie madawa au vitu vinavyoumiza mwili.
vi. Tuzijenge familia zetu ziwe bora kwa kujidhibiti kwa tabia mbaya na hatarishi, kudhibiti tabia za wake zetu, kisha tabia za watoto wetu.
VIi. Tujenge maadili, uadilifu, ukweli na haki. Mambo ya kutishia watoto kwa mambo ya uongouongo kwa maslahi yetu tuachane nayo.
VIII. Tuwasaidie wazazi wetu kama ishara ya upendo, lakini wazazi wasichukulie msaada huo kama wajibu na haki kwao.
Pia usiwe mzigo, kusaidia wazazi ila iwe kutoka moyoni. Kuonyesha shukrani na jinsi tunavyojivunia kuwa na wazazi kama wao. hayo mambo ya kutishana ni mambo ya kipuuzi, yakome
Niwatakie sikukuu njema.
Ni yule kuhani asiyemung'unya maneno,
Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es Salaam.