Tuweke kumbukumbu zetu sawa, huu ndo uchumi wa Magufuli aliouacha, all facts! - Sehemu ya kwanza

Asante kwa elimu hii,mimi ni novice kabisa wa mambo ya uchumi,nilivyokuelewa ni kama baba wa familia fulani aanze mradi wa kujenga nyumba kubwa ya gharama ilihari chanzo vyake vya pesa ni haba na biashara yake ya duka ni ndogo huweza ku finance ujenzi huo,basi anaanza kukopa fedha toka kwa watu,familia inaanza kula chakula kwa kujibana,hata fedha za ada ya watoto zinaanza kupotea,watoto wanaanza kurudishwa toka mashuleni,daah! yaani hali si shwari kabisa.
 
NAIOMBA KWA UNYENYEKEVU MKUBWA SERIKALI YETU YA MAMA YETU MH RAIS SAMIA SULUHU HASSAN ISOME UZI HUU NA MAANDIKO MENGINE YANAYOFANANA NA HILI AMBAYO YANA CONSTRUCTIVE CRITICISM ILI KULINASUA TAIFA TOKA HAPA TULIPO.

MAMA OUR TRUST IS IN YOU.
 

kwa maarifa yangu limited ya kiuchumi

1. Magufuli alitumia mfumo wa kuchukua pesa kwa watu ili afanikishe anayoyataka..
Pesa ilizunguka serikalini sababu hata wajenzi na makampuni mara nyingi alitumia TBA na Jkt.

Hapa utaona tu haikuwa muujiza tax base kusinyaa, mzunguko wa pesa kuwa mdogo, mfumuko wa bei kushuka, na ile miradi mikubwa kuanzishwa kwa pamoja huku uhusiano na nchi wahisani kutetereka, ni lazma Debt to GDP ratio ingepanda kwa speed kali na uchumi kukua negatively

2. Kikwete alikuwa anaachia pesa kwa wananchi.. Alikuwa anaongeza mishahara, miradi ilihusisha sekta binafsi kwa upana zaidi na kodi haikukusanywa kwa kiwango wala efforts kubwa. Hii tu ilitosha kusababisha uchumi kupaa zaidi na ule mfumo wake wa kutembeza bakuli ambao ulipunguza mzigo wa kodi kwa wananchi na kutekeleza miradi yake pasipo kuwaumiza...

There was no way deni liwe kubwa sana kuliko kipindi cha Magufuli au mabenki yasitoe mikopo zaidi ilhali purchasing power ya watu ipo juu mtaani
 
Asante kwa darasa
 



Japo mimi sijawahi kuwa mshabiki wa Hayati Magufuli, ila leo ntajaribu kuwa objective sana, kwa faida ya watu wa pande zote mbili, wale wanaoponda na wala wanaosifia.
 
Huwa nawashangaa sana wanaomsia JIWE kwamba ametuacha imara wakati ametuumiza sana ,wasanii wao wanaangalia SGR tu ,wanaangalia "STEGOLAZ GOJI" tu huku wakidanganywa tunajenga kwa fedha zetu wenyewe kumbe wamekopa hadi hatari.
 
Tuache uwongo...

1. Anasema kipindi cha JK kuna meli 60 zilitia nanga na kushusha mizugo pasipo kurekodiwa. Tafadhali tujuze TAREHE au mwezi.

2: Unasema kipindi cha JK viwanja vya ndege vilikuwa havina scana na kupelekea mizigo kuingia pasipo kukaguliwa.
Huu ni Uongo ata shetani anauogopa.

Niseme tu toka awamu ya Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Jk na jpm teknolojia imekua ikikua siku baada ya siku na imerahisisha mambo mengi.
Mfano, Kipindi cha JK ndio ulianzishwa mfumo wa EFD katika ukusanyaji Kodi, na ilichukua miaka kadhaa kutoa mafunzo na kuusimika mfumo huu nchi nzima. Kipindi cha JPM
Mfumo huu ndio ulikuwa umekwishaenea na ulimrahisishia sana awamu ya 5 kukusanya kodi.
 
Aisee nimesoma uzi mwanzo mwisho.. Huyu mtu ni kama Mungu amemchukua kulinusuru Taifa

Tulikuwa tunaelekae kubaya sana nahisi kwenye umwagaji damu ,2020 uchaguzi ulijaa uharamia ,NEC ilikaa pembeni na "TEETH" ndio wakawa "NEKI" ili wapate wabunge wengi waje kubadili katiba ya kuondoa ukomo wa urais.
 

Uchambuzi Konki kabisa. Sijui washauri wake walikuwa akina nani hasa. Hakika tuna great thinkers. Keep it up Mkuu.
 
Tulikuwa tunaelekae kubaya sana nahisi kwenye umwagaji damu ,2020 uchaguzi ulijaa uharamia ,NEC ilikaa pembeni na "TEETH" ndio wakawa "NEKI" ili wapate wabunge wengi waje kubadili katiba ya kuondoa ukomo wa urais.
Mungu si Athumani. Akaweka natural Ukomo. Ya Mungu si ya Wanadamu. Iwe funzo la uchu wa jambo lolote.
 

Hii hapa siyo kweli kwa sababu kutokuongeza kwa mishahara kulisababisha inflation Tanzania ibaki kuwa ya chini sana. Aliingia madarakani kukiwa na 5.59% na wakati anaondoka inflation ilikuwa 3.56% Kwa hiyo madai ya gharama za maisha kupanda siyo ya kweli. Tatizo lililokuwepo na mzunguko hafifu wa fedha kutokana kna kudhibiti matumizi ya pesa za serikali. Uchumi wa Tanzania umekuwa unategemea sana pesa za serikali kuliko pesa za watu binafsi; serikali ikibana matumizi ya pesa zake basi watu wanalia hawana hela. Ilikuwa hivyo enzi za Mkapa mwanzoni, na enzi za magufuli. Serikali ikishaanza kulegeza usimamaizi wa matumiz yake basi ndipo unaona pesa zinakuw nyingi mitaani na inflation inaongezeka.

 
Mungu ametunusuru sana kumchukua jiwe
 
Mkuu kichuguu... Ongezeko LA bei ya bidhaa Tanzania limekuwa kubwa hasa ndani ya miaka hii sita.. Cement ilipanda maradufu.. Nondo zilipanda maradufu... Sukari ndio balaa.. Mafuta ya kula bei iliongezeka mno... Sasa hajaongeza mishahara lkn bei ya bidhaa ikapanda maradufu.. Zaidi ya yote hili LA vifurushi kupanda bei Jiwe alilibariki lilikuwa linasubiri muda tu lianze...aiseee hali ni mbaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…