Tuweke rekodi sawa, Chini ya Hayati Nyerere na Magufuli, Rasilimali za nchi zilikaa katika mikono salama

Tuweke rekodi sawa, Chini ya Hayati Nyerere na Magufuli, Rasilimali za nchi zilikaa katika mikono salama

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
21,625
Reaction score
33,688
Salaam, Shalom!!!

Kiongozi katika eneo, au JAMII, Nchi nk nk, Huwa ni reflection ya watu anaowaongoza Hasa alikotoka!!

Nimewahi kuishi mikoa Fulani kijana anapata shida kidogo tu ya pesa, Badala ya kuvumilia na kuumiza KICHWA, Yuko radhi auze vyote alivyo navyo, ikibidi hata viatu alivyovaa Ili kutatua shida hiyo, wakati mwingine hata Si shida, ni starehe, KAZI ngumu hawafanyi watu wa JAMII hii!!

Nimeishi pia Kanda Fulani ambazo mzazi au vijana hufundishwa kutafuta na kumiliki Mali, kama ni wafugaji, kwao ni fahari kuona mifugo ikiongezeka, Nia Yao ni kuhakikisha vizazi vijavyo vinafaidi Mali hizo Mali hizo, ikiwa ni wakulima, mashamba watanunua hekari nyingi Kwa ajili ya wajukuu na vitukuu nk nk.

Turudi kwenye mada, uongozi chini ya mwalimu Nyerere na Magufuli, pesa ya umma iliheshimiwa, wezi waliogopa kufuja Mali na raslimali za nchi, viongozi Hawa walihakikisha wanarudisha umiliki wa Raslimali za nchi zimilikiwe na wazawa. Tukaona Mabilionea kwenye Tanzanite wakiibuka, migodi nk nk

Tunajua yaliyotokea katika Awamu zingine, Awamu ya pili ndipo milango ilifunguliwa, wakaingia WEMA Kwa waovu vurugu mechi zikatawala,

Roliondo ikaenda chini ya Mzee Mwinyi,

NBC ikauzwa Kwa Bei ya nyanya, migodi ikabinafsisgwa Kwa wageni chini ya Hayati Mkapa,

Chini ya Mzee wa msoga, Gesi yetu ikaenda, madini yakabinafsishwa nk nk

Funga KAZI sasa ni Ile Awamu ya mpito, yaani ni kuuza na Kugawa na kukopa, na ni miaka michache tu, lakini spidi ya kuvuruga na kutapanya raslimali za nchi ni haielezeki!!

Ushauri: Tupate Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi na KATIBA mpya kabla ya Uchaguzi wowote Ili kuwafunga kengele viongozi wajao, wasijeharibu kama hao niliowaangazia hapo juu.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Karibuni🙏
 
Tafafhali sana Nyerere huwezi kumfananisha na yeyote iwe ndani au nje ya nchi kwa suala La kulinda mali za Umma. Case closed
Case closed,

Wewe ni hakimu?

Anyway, Mwl Nyerere kamwe hawawezi kulinganishwa na Magu, hata mada pia haikuwaweka katika level Moja, Bali ni viongozi wa mfano.
 
Umeongea kweli tupu

Awamu fulani inaongeza speed ya kuuza na kubinafisisha kila kitu tena kwa mamia ya miaka

Bandari, Ngorongoro, mwendokasi, SGR iko njiani pia,
 
Wakati wa utawala wa Magufuli ni maliasili yapi ya Tanzania yalilindwa bila kuchezewa? Pesa zipi za UMMA hazikuibwa.
Bandari ililindwa na mapato yakiongezeka na Mzigo ulitoka bandarini Kwa Kasi kubwa.
 
Funga kazi ya kuharibu Kila kitu ni awamu ya Samia suluhu hasani.kila kitu kimeharibiwa.2025 rais mpya atapata shida sana kuirudisha kwenye mstari.Bora huu Muungano wa kihuni usingekuwepo maana umetuletea li jitu la hovyo.
 
Umeongea kweli tupu

Awamu fulani inaongeza speed ya kuuza na kubinafisisha kila kitu tena kwa mamia ya miaka

Bandari, Ngorongoro, mwendokasi, SGR iko njiani pia,
Yaani Hadi SGR na ndege ambazo wamezikuta, wanapanga kuzibinafsisha Ili wapate Chao.

Yaani Kuna Awamu viongozi wanakusanya,

Lakini Awamu zingine KAZI Yao ni kutapanya!!

KAZI IPO!!
 
Funga kazi ya kuharibu Kila kitu ni awamu ya Samia suluhu hasani.kila kitu kimeharibiwa.2025 rais mpya atapata shida sana kuirudisha kwenye mstari.Bora huu Muungano wa kihuni usingekuwepo maana umetuletea li jitu la hovyo.
Kule pwani, vijana KAZI ngumu hawataki,

Ni starehe Kwa sana, utapeli na deal za madawa na kusafiri.

Watu hao hawaangalii future ya vizazi vijavyo.
 
Siyo kuzaliwa tu, nilijiunga jamiiforum kabla ya Magufuli kuingia madarakani achilia mbali kuzaliwa.
Unawaongeleaje Bakresa na Mo kuja mbio kutaka wapewe SGR wasimamie, mradi ambao ni mkopo hata robo hatujafika?
 
Kuhamisha wanyama kutoka serengeti mpaka kwenye zoo yake binafsi,stupid idea
 
Kuhamisha wanyama kutoka serengeti mpaka kwenye zoo yake binafsi,stupid idea
Sasa uhamisho huo ni WA ndani!!

Hatukuwahi kuona ndege Toka uarabuni zikitua kupakia twiga na wanyama wengine kwenda huko JANGWANI!!
 
Funga kazi ya kuharibu Kila kitu ni awamu ya Samia suluhu hasani.kila kitu kimeharibiwa.2025 rais mpya atapata shida sana kuirudisha kwenye mstari.Bora huu Muungano wa kihuni usingekuwepo maana umetuletea li jitu la hovyo.
Wewe unaleta chuki binafsi
 
Unawaongeleaje Bakresa na Mo kuja mbio kutaka wapewe SGR wasimamie, mradi ambao ni mkopo hata robo hatujafika?
Hivi mkuu, ni mradi gani serikali iliendesha ikarudisha gharama ya uwekezaji? Kama Bakresa anaendesha boti zake kwenda Zanzibar na tunaona huduma ni nzuri sana kwanini asiwekeze hapo kwenye SGR?

FERI za Kigamboni tunashindwa, Magari yaendayo haraka serikali wameshindwa, usafiri za Meli kwenye Maziwa tumeshindwa, usafiri wa ndege tunapata hasara kila kukicha...Sasa unataka mifano gani ili ukubali kuwa SGR nayo tunaenda kushindwa?

Serikali kufanikiwa ni pale itatenganisha biashara na siasa, haiwezekani wanasiasa wanapandishwa kwenye ndege ya biashara kwenda kwenye vikao au ziara.

TANESCO, TTCL, MAJI ....Story ni ndefu sana.
 
Back
Top Bottom