Tuweke rekodi sawa, Chini ya Hayati Nyerere na Magufuli, Rasilimali za nchi zilikaa katika mikono salama

Tuweke rekodi sawa, Chini ya Hayati Nyerere na Magufuli, Rasilimali za nchi zilikaa katika mikono salama

Hao unaowakandia wasingefanya ubinafsishaji leo hii
1. Ungekua bado unakula ugali wa mahindi ya njano
...
Hayo ni maoni Yako pia yaheshimiwe.

Ila kumbuka kuwa, Nchi yetu ilikuwa na viwanda Nchi nzima na wananchi waliajiriwa na kuishi vizuri kuliko sasa.
 
Hata Iddi Amini alitunza Rasilimali na kufukuza Wahindi na kuua Waganda je ilisaidia nini?
Wengine wanakusanya na kuacha akiba,

Wengine wanakuja kutapanya.

Unaliongeleaje hili?
 
Hayo ni maoni Yako pia yaheshimiwe.

Ila kumbuka kuwa, Nchi yetu ilikuwa na viwanda Nchi nzima na wananchi waliajiriwa na kuishi vizuri kuliko sasa.
Proof kwamba wananchi waliishi vizuri? Hebu mtafute mhenga yoyote humu akuhadithie watu walivyokua na maisha magumu mwishoni wa Utawala wa Nyerere.
 
Proof kwamba wananchi waliishi vizuri? Hebu mtafute mhenga yoyote humu akuhadithie watu walivyokua na maisha magumu mwishoni wa Utawala wa Nyerere.
Kwamba wamasai ngorongoro baada ya kutimuliwa kwao wanaishije?
 
Kwamba wanadai ngorongoro baada ya kutimuliwa kwao wanaishije?
Hii ndio proof kwamba watu waliishi vizuri wakati wa Nyerere? Hebu mie nkalale, unakuta najibizana na dogo wa la saba unapotezea watu muda.
 
Mkuu umezaliwa kipindi cha ukweli na uwazi nini?

Shujaa Magu hata Nyerere haoni ndani bhana wee...
Wewe utakuwa umeadithiwa na hukumsikikiza vizuri alikua anakupa story. Uliwahi kusikia viongozi walikua wanasikiliza taarifa ya habari mara kwa mara kujua katumbukiwa au la.

Uliwahi kusikia watu wamekimbia nchi? Uliwahi kusikia visa vya wahunumu uchumi?.

Unajua kisa Cha JK na Lowasa. Mzee alikua Hana zero tolerance.

Unajua tumejua madini ya Gold, diamond, etc tangu kabla ya uhuru Mzee alikataa kusichimbwe mpaka tuwe na uwezo.

Hebu soma taarifa za miaka hiyo kama unafahamu kashfa yeyote ya ubadhitifu.

Unalinganisha na mtu mwaka Moja 1.6trillion zilipotea kina Polepole wakaanza kutoa hesabu za ajabuajabu.

Mwacheni Nyerere apumzike
 
Kwa mujibu wa Lissu Magufuli alificha Mamilioni ya US Dollars kwake Chato.
Na Kwa mujibu wa Lissu huyo huyo, amemtaja Nabii Magufuli kuwa katika kutunza raslimali za nchi, aliitendea HAKI Nchi yetu.

Sasa chagua upande upi wa Lisuu uufuate.
 
Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿
Mada yako ni 'chokonozi , lakini ni mada nzito sana hii.

Niache tu mstari mmoja kabla sijafunga vidole:
Awamu inayo amini kabisa kwamba waTanzania hawawezi kufanya chochote kubadili hali zao; hiyo ni awamu inayotupeleka utumwani.
 
Na Kwa mujibu wa Lissu huyo huyo, amemtaja Nabii Magufuli kuwa katika kutunza raslimali za nchi, aliitendea HAKI Nchi yetu.

Sasa chagua upande upi wa Lisuu uufuate.
Alikuwa amedhibiti kila kitu vikiwemo vyombo vya habari kwahiyo hata kama alikuwa anauza nani angejua? Mtu aliweza kuchezea pesa za Kodi kujenga Kiwanja cha Ndege kwake na kutumia kampuni ya Mayanga ya Jamaa yake.
 
Mada yako ni 'chokonozi , lakini ni mada nzito sana hii.

Niache tu mstari mmoja kabla sijafunga vidole:
Awamu inayo amini kabisa kwamba waTanzania hawawezi kufanya chochote kubadili hali zao; hiyo ni awamu inayotupeleka utumwani.
Kitaumana,

Yaani Rabbon na vizazi vijavyo tutawaliwe na waarabu ambao ukifuatilia maelfu ya ndugu zetu waliopelekwa utumwani uarabuni mabaki na vizazi vyao havijulikani vilienda wapi, ndo hao warudi tena!!
 
Alikuwa amedhibiti kila kitu vikiwemo vyombo vya habari kwahiyo hata kama alikuwa anauza nani angejua? Mtu aliweza kuchezea pesa za Kodi kujenga Kiwanja cha Ndege kwake na kutumia kampuni ya Mayanga ya Jamaa yake.
Sasa kujenga kiwanja nchini hiyo ni vizuri !!

Kutumia kampuni za ndani ya nchi ktk ujenzi ni BUSARA na Uzalendo huo,

Halafu kuhusu Uzalendo wa Magu, umeamua kumkwepa Lisu aliyemkubali?
 
Sasa kujenga kiwanja nchini hiyo ni vizuri !!

Kutumia kampuni za ndani ya nchi ktk ujenzi ni BUSARA na Uzalendo huo,

Halafu kuhusu Uzalendo wa Magu, umeamua kumkwepa Lisu aliyemkubali?
Huyu Mama pia hajauza Bandari kaikodisha tu.
 
TUNDU Lissu: Magufuli alikuwa Mzalendo, hakuuza bandari zetu!!
Hayo siyo maneno ya rahisi rahisi kuzungumzwa na mtu kama Tundu Lissu, akimuelezea mtu Magufuli, ambaye katika hali ya kawaida ya kibinaadam kabisa usingetegemea kuyasikia. Hapa hakuna kupakana mafuta kwa chupa.
 
Huyu Mama pia hajauza Bandari kaikodisha tu.
Kaikodisha Kwa Bei Gani?

Kwamba unapingana na Lissu ambaye amedai tangu Nchi ipate uhuru, hajawahi kuona mkataba mbovu, wa hatari kana IGA ya bandari?
 
Kaikodisha Kwa Bei Gani?

Kwamba unapingana na Lissu ambaye amedai tangu Nchi ipate uhuru, hajawahi kuona mkataba mbovu, wa hatari kana IGA ya bandari?
Mikataba ya Serikali ya CCM haijawahi kuwa mizuri na huyu Mama ni muendelezo tu.

Na ni kwanini Magufuli alikasirishwa zaidi na Lissu hadi kufikia kutaka kumuua?!

Kitu ambacho si Kikwete wala huyu Mama hawakukifanya?!
 
Back
Top Bottom