Tuweke rekodi sawa, Deo Mwanyika alihukumiwa kwa kukwepa kodi

Tuweke rekodi sawa, Deo Mwanyika alihukumiwa kwa kukwepa kodi

mumburya

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2012
Posts
321
Reaction score
448
Michango ya NSSF ya Deogratius Mwanyika, aliyekuwa Rais wa migodi ya Pangea, North Mara Exploration na Bulyanhulu, imelazimika kutumika kulipa sehemu ya fidia ya makubaliano maalum kwa Serikali baada ya kukiri kufanya makosa ya uhujumu uchumi.

Fedha kiasi cha TSh bilioni 1, kilichotwa na kuingizwa kwenye akaunti ya maalum ya fedha za serikali inayosimamiwa na Hazina iliyoko Benki Kuu ya Tanzania (BoT) mnamo Mei 11, 2020.

Makubaliano ya faini yaleta utata hadi Ikulu kuhusishwa

Makubaliano hayo yaliyokuwa na mvutano kiasi hasa katika kuafikiana kiasi cha fedha, Mwanyika akiomba kulipa Sh milioni 700 na serikali kupitia kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), ikisita kuridhia kiasi hicho hadi ilipohusishwa Ikulu mnamo Mei 4, 2020 na kuamua kilipwe kiasi cha TSh bilioni 1.5. Kiasi kingine imekubaliwa kilipwe ndani ya miezi sita.

Juni 17, 2020 Mwanyika aliachiwa huru na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, pamoja na wenzake wawili, baada ya Serikali kueleza kwamba Mwanyika amekubali kulipa fidia ya TSh bilioni 1.5. Mwanyika na wenzake wawili, Assa Mwaipopo, mkurugenzi wa migodi hiyo na Alex Lugendo, akiwa Meneja Uhusiano walikutwa na kosa la kukwepa kodi na kuamriwa na Mahakama kulipa faini ya Sh milioni 1.5 kila mmoja.

Kukamatwa na kukiri makosa

Mwanyika na wenzake walikamatwa Oktoba 17, mwaka 2018 na waliendelea kusota rumande gerezani Segerea jijini Dar es Salaam kwa zaidi ya miezi 21 hadi walipoamua kukiri makosa yao; kubwa likiwa ni kuhujumu uchumi. Washtakiwa awali walikuwa na mashtaka 39, lakini 38 yaliondolewa na kubaki moja; kukwepa kulipa kodi, ambalo lilipelekea kupata nafasi ya kulipa faini.

Mshahara wake

Uchunguzi umebaini kuwa Mwanyika aliyefanya kazi katika kampuni hiyo kubwa ya uchimbaji madini, hasa dhahabu kwa zaidi ya miaka 17 – akianzia Kahama Mining kabla ya kuamua kustaafu akiwa na cheo cha Rais wake kanda ya Afrika alikuwa na mshahara wa dola za Marekani 47,300 (sawa na Sh milioni 114) kwa mwezi.

Endapo Mwanyika alidumu katika nafasi hiyo kwa miezi 48 (miaka 4), atakuwa alikusanya zaidi ya Sh 1,104,000,000 (Sh bilioni 1.104). Sheria ya makato ya NSSF kwa wakati huo ilikuwa ikimlazimu mwanachama kulipa asilimia 10 ya mshahara wake huku mwajiri akitakiwa kulipa asilimia kama hiyo na kuingizwa kwenye michango ya mwanachama. Kiasi hiki kwa nafasi hiyo ni tofauti na kile alichohudumu na kuchangia NSSF kwa miaka 13 mingine akiwa na wawekezaji hao.

Mwanyika na michezo yake hatari na wawekezaji

Mwanyika katikati ya wawekezaji hao, alisifika “kupunguza munkari na machungu” kwa wananchi wanaozunguka mgodi wa North Mara baada ya kutokea mauaji ya watu watano na tuhuma za ubakaji zilizokuwa zikielekezwa kwa walinzi pamoja na baadhi ya askari wa Jeshi la Polisi waliopewa jukumu la kulinda mali za mgodi huo ulioko mkoani Mara.

Katika barua yake ya Machi 11, 2014 ikiwa na kurasa 12, kwa timu ya uchunguzi wa matukio hayo, Umoja wa Mataifa (UN) na wadau wengine wa madini duniani, Mwanyika aliandika barua ndefu kuelezea kilichotokea, hatua zilizochukuliwa na mgodi pamoja na Serikali ya Tanzania na kuahidi kukomesha mauaji na unyanyasaji mwingine dhidi ya binadamu kwa wananchi wanaozunguka na kufanya kazi maeneo ya migodi.

Baada ya hapo, Mwanyika akapewa majukumu makubwa aliyoendelea nayo hadi alipoomba kustaafu mapema kabla ya muda wake.

Ukwasi

Akiwa ni mtaalamu mbobezi wa sheria za madini, Mwanyika amewekeza zaidi kwenye biashara ya hoteli, akiwa na hoteli ya kisasa Njombe, kilimo cha miti na “real estate” jijini Dar es Salaam na Johannesburg nchini Afrika Kusini.

CHANZO: Mwanyika abomolewa akaunti NSSF, alipa TZS Bilioni moja
 
Hili ni tatizo kubwa sana sio Tanzania tu bali Afrika nzima. JPM ameanza lakini je, tutaendelea kuona kwamba utajiri na rasilimali za taifa hili zinainua maisha ya Mtanzania?
 
Hili ni tatizo kubwa sana sio Tanzania tu bali Afrika nzima. JPM ameanza lakini je, tutaendelea kuona kwamba utajiri na rasilimali za taifa hili zinainua maisha ya Mtanzania?

Huyu kateuliwa na CCM kugombea Ubunge Njombe Mjini, sasa soma hapa chini uone kuwa mbele ya JPM katiba ni karatasi tu;

67.-(1) Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika ibara hii, mtu yeyote atakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge endapo-

(a) ni raia wa Jamhuri ya Muungano aliyetimiza umri wa miaka ishirini na moja, na ambaye anajua kusoma na kuandika katika Kiswahili au Kiingereza;

(b) ni mwanachama na ni mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa;

(c) katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya Uchaguzi hakuwahi kutiwa hatiani katika mahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa kodi yoyote ya Serikali.
 
Huyu kateuliwa na CCM kugombea Ubunge Njombe Mjini, sasa soma hapa chini uone kuwa mbele ya JPM katiba ni karatasi tu;

67.-(1) Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika ibara hii, mtu yeyote atakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge endapo-

(a) ni raia wa Jamhuri ya Muungano aliyetimiza umri wa miaka ishirini na moja, na ambaye anajua kusoma na kuandika katika Kiswahili au Kiingereza;

(b) ni mwanachama na ni mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa;

(c) katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya Uchaguzi hakuwahi kutiwa hatiani katika mahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa kodi yoyote ya Serikali.
Sheria ya plea bargain inasemaje?
 
Huyu ni mhalifu aliye kubuhu na alikiri hadharani kui snitch nchi, alitakiwa sio kutimuliwa kwenye kugombea ubunge tuu bali kutandikwa mawe adi afe
 
sheria haiwezi kuizidi katiba
FYI hakuhukumiwa kwa hiyo katiba haiingii hapo. Soma vizuri kilichoandikwa ndio sababu wakaita plea bargain. Unarekebisha mambo na unaondoka msafi mahakamani ie huna doa. (Why, kwa sababu ile kodi aliyokuwa anataka kukwepa umekubali kuilipa ie 1.5 billion). Simple as that! Kila mtu anaendelea na maisha yake na if I am not mistaken kuna period unapewa usirudie huo nchezo. Re: Kabendera saga, si na yeye alilipa na kaondoka msafi anaendelea na maisha yake bali asirudie tena. (I presume kuna kipindi wanapewa kutokurudia).
 
FYI hakuhukumiwa kwa hiyo katiba haiingii hapo. Soma vizuri kilichoandikwa ndio sababu wakaita plea bargain. Unarekebisha mambo na unaondoka msafi mahakamani ie huna doa. (Why, kwa sababu ile kodi aliyokuwa anataka kukwepa kakubali kuilipa ie 1.5 billion). Simple as that! Kila mtu anaendelea na maisha yake na if I am not mistaken kuna period unapewa usirudie huo nchezo.

..ingekuwa hivyo basi plea bargain isingekuwa inarekodiwa na Mahakama.

..washtakiwa wangekuwa wanamalizana na DPP na kurejea majumbani kwao.

..actually kwa uelewa wangu Hakimu anaweza kuikataa plea bargain kama akiona inakwenda ndivyo-sivyo.

..na kwasababu inamhusisha Hakimu, basi kinachotokea baada ya plea bargain ni HUKUMU.
 
..plea bargain ni kukubali kuwa una hatia.
Unakubali hatia lakini hakuna hukumu! Ndio makubaliano hayo, ie unapunguza usumbufu na mahojiano ya hapa na pale then unalipa gharama zote za mahakama na ulichotaka kuiba then mchezo umekwisha. Kwa Tanzania utaona ni kitu cha ajabu lakini nchi nyingi tu zilizoendelea ni jambo la kawaida kwa sababu ukihukumiwa unakuwa na doa flani hivi.

Chacha mkuu umeshindwa kumwuliza TL? Yeye si ndio mwanasheria wenu?
 
Unakubali hatia lakini hakuna hukumu! Ndio makubaliano hayo, ie unapunguza usumbufu na mahojiano ya hapa na pale then unalipa gharama zote za mahakama na ulichotaka kuiba then mchezo umekwisha. Kwa Tanzania utaona ni kitu cha ajabu lakini nchi nyingi tu zilizoendelea ni jambo la kawaida kwa sababu ukihukumiwa unakuwa na doa flani hivi.

Chacha mkuu umeshindwa kumwuliza TL? Yeye si ndio mwanasheria wenu?

..plea bargain inakupunguzia ukali wa adhabu, haikuondolei makosa, au kukusafishia rekodi.

..unaweza kuingia plea bargain ili upewe adhabu ya kifungo cha maisha, badala ya adhabu ya kunyongwa.
 
..ingekuwa hivyo basi plea bargain isingekuwa inarekodiwa na Mahakama.

..washtakiwa wangekuwa wanamalizana na DPP na kurejea majumbani kwao.

..actually kwa uelewa wangu Hakimu anaweza kuikataa plea bargain kama akiona inakwenda ndivyo-sivyo.

..na kwasababu inamhusisha Hakimu, basi kinachotokea baada ya plea bargain ni HUKUMU.
Tuwekee basi utaratibu wa plea bargain kwa Tanzania. Vile vile tuwekee hukumu aliyopewa. Maana mimi hukumu sikuiona.
 
Tuwekee basi utaratibu wa plea bargain kwa Tanzania. Vile vile tuwekee hukumu aliyopewa. Maana mimi hukumu sikuiona.

..sina details za ndani kiasi hicho.

..inawezekana suala hili likafika mahakamani.
 
..sina details za ndani kiasi hicho.

..inawezekana suala hili likafika mahakamani.
As far as I know hakuna hukumu hapo, ndio sababu alilipa huo mpunga. CCM wasingeweza kufanya ujinga kama huo kwa sababu sheria zipo na lazima zifuatwe na raia wote bila kujali dini wala itikadi. Tusubiri maana kama hukumu ipo I am sure Chadema/mpinzani atakayeshindwa atakata rufaa tu.
 
Hili ni tatizo kubwa sana sio Tanzania tu bali Afrika nzima. JPM ameanza lakini je, tutaendelea kuona kwamba utajiri na rasilimali za taifa hili zinainua maisha ya Mtanzania?
Zitaendelea kuwainua watanzania wanaosifu na kupiga vigereger tu
 
Zitaendelea kuwainua watanzania wanaosifu na kupiga vigereger tu
Yaani Hospitali zote zilizojengwa pamoja na wanafunzi wote wanaosoma na umeme wote kwa kila Mtanzania na usafiri wa uhakika ni kwa wale tu wanaosifia? Pengine unayaona maisha ya Tanzania tu na hujasafiri kwenda kwenye nchi nyingine, kama umesafiri basi umesafiri nchi moja tu ambayo unaifahamu. Siku hizi ukitaka kwenda Airport ukiwa Dar Es Salaam sio lazima utumie masaa 3-4. Siku hizi Tanzania ukiwa mgonjwa sio lazima usafiri kwenda kutibiwa India.

Kuanzia December ukiwa na safari ya kwenda Morogoro sio lazima upande basi unaweza kutumia SGR? Zile kelele za ma-generator kila duka zimekwisha. Kukatika umeme imekuwa ni hadithi. Wale watoto ambao na wao walikuwa marais hawapo tena.
 
Wacha1

Plea Bargaining system to be introduced in Tanzania
  • The Bill introduces plea bargaining in criminal cases
  • Procedures for plea bargaining agreement articulated
  • Consequences of plea bargaining stipulated in the Bill
  • Plea bargaining agreement to be registered for it to be effective
  • Some offences ineligible for plea bargaining
  • Circumstances to set aside a verdict founded on plea agreement enumerated
In a bid to ensure timely delivery of justice, reduce backlog of cases, as well as reducing inmate congestions in prison facilities, the Government of Tanzania has issued a Bill whose aim is, among others, to introduce plea bargaining in criminal cases. The Bill was tabled in the last session of the National Assembly for first reading and will formalize what has been practiced for a while.

Plea bargaining has been defined in the Bill to mean an arrangement between a prosecutor and accused whereby the accused pleads guilty to a particular offence or a lesser charge in exchange for a more lenient sentence or an agreement to drop other charges.

The Bill obliges a public prosecutor to conduct plea bargaining with the accused person after consultation with the victim/investigator and before pronunciation of judgment. However, the accused is also permitted to initiate plea bargaining by notifying the Court, but the Court is prohibited to participate in plea negotiation between a public prosecutor and the accused.

The Bill makes it mandatory for the plea agreement to be in writing and to fully state the terms of the agreement, the substantial facts of the matter and all other relevant facts of the case and any admissions made by the accused person. It must also be read and explained to the accused in a language that he understands, must be accepted by the accused and be signed by the prosecutor, the accused and his legal representative (if any).

A plea agreement is required to be registered by the Court for it to be binding, and the Court will convict the accused person accordingly. However the Court is vested with powers to reject a plea agreement so long as there are adequate reasons to do so.

Additionally, prior to registration of plea agreements, the Bill makes it necessary for the Court to inform the accused person of the below consequences:
  • registration of plea agreement will lead to a waiver of a right to full trial
  • the right to appeal will only be permitted to the extent or legality of sentence
  • the prosecution has the right, in the case of prosecution for perjury or false statement, to use any statement against the accused, which is in the agreement
Further, plea bargaining shall not be exercised in sexual offences whose punishments exceed five years or involve victims under eighteen years; treason and treasonable offences; possession or trafficking in narcotic drugs whose value is above ten million shillings; terrorism; possession of Government trophy whose value is above ten million shillings; or other offence as the Minister may publish in the Gazette.

Finally, for the purposes of protecting public interests, the Director of Public Prosecution may apply to the Court to set aside conviction and sentence that was obtained on the grounds of fraud or misrepresentation pursuant to a plea bargaining. Equally, the accused person may do the same if the plea agreement was procured involuntarily or by misrepresentation.

When passed, this Bill will be similar to plea bargaining laws in neighbouring Kenya and Uganda that have assisted in reducing the number of criminal cases.

source: FB Attorneys – Law firm in Tanzania
 
Wacha1

Plea Bargaining system to be introduced in Tanzania...


''The Bill makes it mandatory for the plea agreement to be in writing and to fully state the terms of the agreement, the substantial facts of the matter and all other relevant facts of the case and any admissions made by the accused person. .............................................................

Finally, for the purposes of protecting public interests, the Director of Public Prosecution may apply to the Court to set aside conviction and sentence that was obtained on the grounds of fraud or misrepresentation pursuant to a plea bargaining. ......................................................................................''

Kama ilivyo hapo juu, ukitaka kuhukumu vizuri lazima uipate hiyo ''agreement'' kama huna utakuwa unaleta majungu tu humu. Kama nilivyosema mwanzo CCM sio wajinga wanafahamu wanachokifanya, why? Kwa sababu wanayo hiyo agreement na wanafahamu kuna nini? Vile vile sehemu ya pili DPP inawezekana kabisa aliomba mahakama ''ku-set aside conviction''.

Kama una facts zimwage.
 
Back
Top Bottom